CHADEMA waweka bayana msimamo wao juu ya yaliyowasibu ma-Sheikh Ponda na Farid

Kwa kichapo kile hawawezi tena kurudia hawa jamaa,hata hivyo kauli hizo za chadema zina ukweli.hapo ndipo nawakubali sana chadema kwa kutumia udhaifu wa adui.viva CDM
 
Chadema haiwezi kuongoza Tanzania na huu ni ushahidi tosha....wanamuunga mkono gaidi ponda kipindi hiki tunateseka.....mbwa kabisa
 
dhah! kama chadema ndo wameongea hivi yani wajue hata kula yangu hawaipati tena na kadi yao narudisha, kwaiyo walitaka wawaache hao wahuni waendelee na hizo vurugu bila kuchukuliwa hatua sio???? mmeniboa chadema from 2 day i hate all of you.

Sa unarudisha ya nini kwanini usiichane tu kuokoa muda??Unairudisha ili nani apewe wakati inajina lako?!

Ndo nyie mnanunua sumu ili ujiue, afu unadai chenji.
 
Wamepima wakaona mbali sana.kura za zanzibar zinaamua nani anakua rais wa Tanzania.kwa chadema kupata hata asiliamia 30 za kura zao inawapeleka karibu na ndoto zao za kukamata dola.ukichukulia kua wameshakubalika kwa jamii wakristo.

sio kwamba CDM ni chama cha Wakristo, bali tunajua kwamba kinaungwa mkono na watu wasomi na waelewa wa mambo. Viongozi wake hawakurupuki bali huwa na busara katika kutatua mambo.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekutana na waandisihi wa
habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam leo, ambapo wajumbe wa Kamati Kuu, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando, wameweka waziwazi msimamo wa chama hicho kuhusiana na mgogoro kati ya waislamu na serikali na kukamatwa kwa Sheikh Farid huko Zanzibar.

Wanasheria hao wa CHADEMA wamesema kuwa kitendo cha serikali kumnyima dhamana Sheikh Ponda ni kinyume cha katiba na kwamba Chadema kama chama kinachojiandaa kuchukua dola, hakiwezi kuvumilia kuona haki za raia zikivunjwa.

“Tunaweza kuwa miongoni mwetu, wapo watu wanaomchukia Sheikh Ponda, lakini hatuwezi kuficha ukweli kwamba Sheikh Ponda kama raia wa Jamhuri ya Muungano au mkazi wa Jamhuri hii, anayo haki ya kusikilizwa na kupewa dhamana. Makosa ambayo Sheikh Ponda ameshitakiwa yanadhaminika kwa mujibu wea sheria, hivyo ni makosa kwa serikali kufanya hila kumnyima dhamana kiongozi huyu wa kidini,” ameeleza Marando katika mkutano huo.

Marando alifika mbali zaidi kwa kusema tatizo lililopo sasa kati ya serikali na waislamu, limetokana na hatua ya serikali kuwalazimisha waislamu wote kuwa waumini wa Bakwata, chombo ambacho wengi wanakiona kinatumika kuwakandamiza.

Naye Profesa Safari alionya matumizi ya nguvu za kijeshi yanayotumiwa na serikali kwa kisingizio cha kulinda amani, huku akieleza kuwa matumizi ya kijeshi siyo suluhu ya kutatua matatizo yaliopo.

Kuhusu kukamatwa kwa Sheikh Faridi na kumzuia kwa siku tatu, wanasheria hao wamesisitiza kuwa kitendo hicho hakikubaliki.

“Kitendo cha kumkamata na kumshikiria Sheikh Faridi, huku serikali na vyombo vyake vikisema havihusiki, wakati ukweli ni kuwa alikuwa anashikiliwa na watu wa USALAMA wa TAIFA, ni uharamia mkubwa unaopaswa kulaaniwa na wote wanaolitakia mema taifa hili,” ameeleza Marando.

Kuhusu uvunjwaji wa makanisa, Profesa Safari amesema CHADEMA kimelaani hatua hiyo iliyotokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi. Amewataka waislamu kuvuta subira.

Hata hivyo, Profesa Safari amesena matatizo yanayotokea sasa, yameletwa na CCM kutokana na hatua yao ya kuwatumia baadhi ya waislamu kupandikiza mbegu ya udini nchini.

Jamani hawa jamaa wamesema wamesema mengi, lakini kwa sasa yanatosha kueeleza hayo.

CHADEMA wameegemea sana kwa waislam, waislam walitakiwa kupambana na Serikali na siyo wakristo maana sisi wote bado ni maskini hivyo kuchomeana nyumba za ibada ni kurudishana nyuma
 
Wafuasi wengi wa chadema wana weledi wenye kutaka maendeleo. Mambo ya dini na ukabila singles hizo zilisha expire....

Leta nyingine.

Mumba, nimekuwa nikunga mkono CDM kwa miaka yote hii, na nimekuwa JF kwa muda mrefu, kila mara nimekuwa nikikemea pale ninapoona mashabiki wa CDM wakielekea katika mlengo wa udini, lakini katika hii wiki iliyopita nimejifunza kuwa kumbe wafuasi wengi wa CDM ni wadini tena wabaya sana, mpaka wa kuombea Waislamu kuaawa, na mimi hilo siwezi kukubaliana nalo kamwe.
 
Chadema sio chama chakidin nicha siasa.na watanzania wote wanakitegemea kiwakomboe toka ndan ya uchafu wa ccm.din zote ni ndugu mimi nimwisilam nimeoa kwa wakristo kamwe siwez pipana na mama mkwe wangu hawawez tugawa hata.hongera chadema kwa tamko laukweli mtupu sisi tunawategemea sanaa
 
Hukunielewa kumbe
mimi nawazungumzia CHADEMA...
sijasema Ponda asipewe dhamana
wala sijasema ni sahihi kukamatwa..

my point was deep down Chadema wana sapoti serikali
but hawawezi sema hadharani,since kisiasa hawataeleweka
so wameongea kujikosha
sasa nimekuelewa ila kama chama cha siasa duniani kote walichofanya ni sahihi kama chama cha siasa japo sio sahihi kusema wameisapoti serekali, na mimi nimezunguza kitaalamu hapo awali (Kisheria)
 
Naipenda sana chadema na pia ninaiamini kuliko chama kingine chochote cha kisiasa hapa nchini. Lakini katika hili, siwaungi mkono. Japo najua huu unaweza kuwa mtaji mkubwa wa kisiasa kwao. Hivyo naona wanatumia logic kuzidi kujijengea umaharufu kitu ambacho ni kizuri kwa sisi wapenzi wa cdm.
 
Wewe ni mdini Dana na hulitakii taifa lako mema au wewe msomali mwenzetu? Kila Siku unasema Chadema chama cha wakristo Leo CDM wanalinda na kusimamia haki za waislam wanazoporwa na bakwata wewe unasema huwa support je unakumbuka ni lipi unalo support CDM? Ulitaka CDM waseme msimamo wao ni kuchoma misikiti? CDM ni chama makini sio genge la wahuni au watumiwa Kama nyie Naunga mkono Hoja CDM Kwa hili mko juuuuuuuuu


Kwa hili am not supporting chadema wale majaaa hawafai chadema tulieni mtajiaibisha hakuna atae enda mtaaani tena

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Nimependa sana tamko hili la CHADEMA maana lingekuwa ni la kuzidi kumkandamiza yule hayawani Ponda basi wale wote wanaoichukia CHADEMA wangepata nafasi ya kuchonga zaidi....``Unawaona hawa CHADEMA hakuna siku wanaweza kusimama kumtetea Muislamu nchi hii, wanawachukia sana Waislamu angekuwa ni Padri kakamatwa kauli ya CHADEMA isingemkandamiza Mkristo mwenzao``...Hongereni sana CHADEMA....

Sifagilii hata kidogo yaliyofanywa na Ponda kama sheria zinaruhusu apewe dhamana basi Serikali impe dhamana na masharti makali yakiambatana na dhamana hiyo, akivunja masharti hayo basi arudishwe lupango mara moja.


CDM ni chama kinachojua kucheza na jukwaa la wananchi kama ni uwanjani ni timu inayojua kucheza na jukwaa. Kiukweli ni kauli ni tamko zuri sana wangetoa kabisa PDF ili watu walisome lote.
 
dhah! yani kama chadema ndo wameongea haya maneno kuanzia leo siwataki tena na kura yangu hawataiona, na hili likadi lao narudisha yani wanawatetea hawa wahuni, kwaiyo walitaka waendelee kufanya maandamano na kudumisha vurugu sio??? kumbe ni bora hata hiyo ccm, eti ponda awekewe dhamana kwaiyo ndo mnaingia lasmi kum defend huyo gaidi????? yani chadema mmeniboa mbaya and from 2 day i hate all of you.

Wewe ni mdini, ulitaka waseme walichofanya askari kupiga kila mtu mwenye kanzu barabarani ni sawa? Utawala wa sheria, haki za binadalu hazina excuse ukizivunja lazima watu waseme, sheria iko kwa ajiki ya kutoa haki kwa kila mtu! Kama sheria inasema ponda alistahili kupata dhamana itaendelea kuwa hivyo tu lazima itimizwe!
 
Kweli we fisadi mtoto! Hivi una jua maana ya gaidi?

Kama umesoma vyema tamko hilo limeeleza wazi kuwa pamoja na makosa aliyo nayo bado ana haki ya kupewa dhamana!

Na swala la kuwa gaidi sijui umelitoa wapi?

Chadema haiwezi kuongoza Tanzania na huu ni ushahidi tosha....wanamuunga mkono gaidi ponda kipindi hiki tunateseka.....mbwa kabisa
 
Back
Top Bottom