Nimemsikia Sheikh Ponda akisema kuwa hakubaliana na Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka muswada wa umri wa ndoa kuwa miaka 18

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,536
27,030
IMG_20230407_083230_067.jpg

Leo nimemsikia Sheikh Ponda akisema kuwa hakubaliana na Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka muswada wa umri wa ndoa kuwa miaka 18. Anadai kuwa ni kinyume na dini ya Kiislamu kwa sababu miaka 18 ni sera ya Wakatoliki.

Kusema kweli kwa maneno haya nimeanza rasmi kumdharau Sheikh Ponda kwa sababu nchini Saudi Arabia, nchi ambayo ndo kitovu cha imani ya dini ya Kiislamu ulimwenguni umri wa ndoa ni miaka 18.

Sasa Sheikh Ponda sijui anasema Uislamu gani? Ifike kipindi sasa watu waache kutumia dini kuendekeza tabia zao za kipuuzi. Serikali iko sahihi kuweka umri wa ndoa kuwa miaka 18.

Screenshot_20230405-212527_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom