CHADEMA wanaweza kupoteza jimbo la Moshi Mjini

CHADEMA wanaweza kupoteza jimbo la Moshi Mjini

uko sawa ila umeharibu ulipojaribu kulinganisha na Yesu
utakuwa umevurugwa wewe, huwezi kuwa uko serious
Hapa moshi hata Yesu agombee CCM hlf chadema waweke jiwe..basi watu wanachagua jiwe..MOSHA H A P I T I.
 
Uchaguzi wa 2005 nilikuwa Moshi na nilikuwa naishi maeneo ya Pasua na nilishuhudia mpambano wa Philemon Ndesamburo (CHADEMA) na yule mama mwanasheria Elizabeth Minde (CCM)

Kwa namna CCM walivyokuwa wanatembeza pesa kununua voters, ilikuwa balaa tupu kiasi kwamba yule mama alijiaminisha kuwa kashinda hata kabla ya kura kupigwa!!

La haura!....wachagga wa Moshi mjini ni noma sana, walishai delete CCM ktk vichwa vyao!!

Yule mama hakuamini matokeo yake na aliishia kulazwa Hospitali ya rufaa ya KCMC!!

Kwa siasa za Moshi mjini, sitegemei CCM kushinda si ubunge tu bali hata viti vitatu tu vya udiwani manispaa pale, sidhani kama watapata!!
 
Paka sasa upepo WA moshi MJINI unaonesha Davis mosha wa chama cha mapinduzi CCM anakubalika kwa vijana NA wazee..vile vile dhana ya ukabila inaweza kujitokeza baina ya wagombea hawa..sijui kama wachaga watakubali kuongozwa na mpare?Abel sere 4m moshi town

Unaongelea moshi mjini ipi?
#borakumchagua #mkosakabila kuliko ccm.
Team mabadiliko..
Team lowasa
 
Upuuzi kudhani kwamba utajiri ndiyo kigezo cha kupata ubunge. /Uongozi.

Ndicho ccm wanachotegemea kuwa Davis atapita ? Ndesa pesa kasimama na miguu miwili. ccm moshi mjini ni delete futa kabisa.
 
Paka sasa upepo WA moshi MJINI unaonesha Davis mosha wa chama cha mapinduzi CCM anakubalika kwa vijana NA wazee..vile vile dhana ya ukabila inaweza kujitokeza baina ya wagombea hawa..sijui kama wachaga watakubali kuongozwa na mpare?Abel sere 4m moshi town

CCM Moshi? you're joking, right?

yatakuwa ni sawa na maajabu ya kukuta viroba vya konyagi kuseviwa ndani ya msikiti / kanisa haya!
 
Kweli Mosha kajipanga, ukikanyaga mjini lazima u-feel uwepo wake. Kajaza mabango kila nguzo, mabango yaliyoandaliwa kwa ustadi sana. Big up Mosha, huyo ndo uanaume.

mabango?!yaani Jafari hata asipoweka bango kashapita maana kazi aliyoifanyia Moshi kwa kipindi kifupi alipokuwa meya hawezi kukosa kura!mabango aliyaweka Sarakana bana ile 2010,muulize kilichompata? moshi hawachaguagi mtu asiyeishi moshi
 
hilo hata Mimi nimeliona Davis mosha yupo vizuri kwani ukawa wamemuweka nani

sasa wewe unasema Mosha yupo vizuri bila kujua anashindana na nan?unaakili wewe?Mosha akashindane na wauza ngada huko sio kushindana na mtu aliyefanya maajabu hapa moshi kwakubadilisha mji huu kuwa kama ulivyo leo!!!Moshi ni ya Jafari hata kura zirudiwe mara kumi
 
Kila jimbo la upinzani, unajifanya wewe ni mkazi wa hapo, Jana ulikuwa unajitaja kama mwana Arusha!
Njia ya muongo ni fupi!

Mbona hata wewe ulikua unasema lema hawezi kutetea kiti chake. Saivi upo na lema bega kwa bega. Bwana msalani njaa mbaya sana. Umepoteza utu wako pamoja nA akili yako sababu ya njaa
 
Hapa moshi hata Yesu agombee CCM hlf chadema waweke jiwe..basi watu wanachagua jiwe..MOSHA H A P I T I.

Aisee tubu, Nina ushuhuda wa watu waliodhihaki hilo jina wakafa, kuna mwanamziki alikuwa jukwaani akasema yeye ni femous than Jesus Christ, hakufika nyumbani alipata ajali akafa na wengine wengi, please tubu
 
Hapa moshi hata Yesu agombee CCM hlf chadema waweke jiwe..basi watu wanachagua jiwe..MOSHA H A P I T I.

Kuna jinsi nyingi za kuelezea hisia, ila hapa umekosea, naomba utubu, labda kama wewe sio mkristo na kama sio mkristo tubu pia, nakuomba maana binafsi nimeogopa
 
Hapa moshi hata Yesu agombee CCM hlf chadema waweke jiwe..basi watu wanachagua jiwe..MOSHA H A P I T I.

Unawezaje kumdhihaki Kristo kiasi hiki?? Mungu akusamehe, naomba toba kwa niaba yako
 
[QUOTES=Prosoo;13897091]Hapa hata Yesu agombee moshi CCM hlf chadema waweke jiwe..basi watu wanachagua jiwe..MOSHA H A P I T I.[/QUOTE]
 
Hapa moshi hata Yesu agombee CCM hlf chadema waweke jiwe..basi watu wanachagua jiwe..MOSHA H A P I T I.

Huyu naye ni Mtanzania na anajiona naye ni sehemu ya watu wenye akili timamu, kwanini mnakuwa na mihemko na mahaba ya kijinga kiasi hiki? Yesu na misiasa yenu ya kijinga anaingiaje hapa. Hebu jisikie aibu kwa mtu mzima kukosa adabu kwenye masuala ya dini hata kama wewe ni mpagani
 
Mimi binafsi naona kati ya ngome (majimbo) ya CHADEMA kote nchini, kazi nzito na ngumu itakuwepo Ubungo na Moshi mjini, kwa mtazamo wangu naona yataenda CCM

Sijui kuhusu Ubungo, ila kwa Moshi mjini kwenda CCM ni ndoto za mchana hizi, in English tunaziita Illusions!!!
 
Huyu naye ni Mtanzania na anajiona naye ni sehemu ya watu wenye akili timamu, kwanini mnakuwa na mihemko na mahaba ya kijinga kiasi hiki? Yesu na misiasa yenu ya kijinga anaingiaje hapa. Hebu jisikie aibu kwa mtu mzima kukosa adabu kwenye masuala ya dini hata kama wewe ni mpagani

mbona na wewe kama umepagawa vile!!
 
Davis ndo kiboko ya chadema..."Mwenyekiti" akisikia hilo jina anatafuta kichaka kuchimba dawa
 
Back
Top Bottom