CHADEMA wanamwogopa Anne Makinda?

Hivi bado tu mnatumia energy yenu kuwadiscus hawa Chadema?

Hawana msaada wowote kwa mwananchi! kazi kuandamana tu na kufanya vurugu ambazo wanaishia kuumia wenyewe!

masaburi mengine haya.napita tu.

Kama wewe ni mfuatiliji mzuri utagundua kuwa tangu siku Lissu aliposema kuwa CHADEMA wanamshitaki Spika Makinda kwenye kamati ya uongozi, huyu Spika kabadilika kabisa. Yale mapembe yaliyokuwa yanaota kwa kasi ya kutisha yamepotea katika mazingira anayojuwa mwenyewe Spika!

Ni juzi tu Spika kaitaka serikali kutoa tamko juu mgao wa umeme na hii ilitokana na hoja wa Wenje kuwa mgao wa umeme ujadiliwe. Hii ni tofauti kabisa na alivyokuwa huko nyuma huyu mama!
unamaanisha kuwa Mh.Lisu ameshamshkisha adabu???

Naamini Makinda alikalishwa kuonywa tabia ya upendeleo aliyo kuwa anaionyesha wazi wazi, siku hizi kaanza kubadilika kwa kuakataa miongozo ya akina Lukuvi na wengine toka magambani. Kuwaruhusu wabunge wa upinzani waongee bila kukatishwa katishwa kwa miongozo uchwara. pia nilifurahi alipo mtolea uvivu Waziri Mkuu kwa kukaa anapiga soga na wabunge wawapo kwenye kikao, alimwambia kama hataki kusikiliza bora aondoke aende ofisini wamfuate huko.

Mtoa hoja anajua ukweli wote na ni mfuatiliaji, bali anataka kuwachochea wabunge wa chadema walipuke nje ya kanuni, ili wajidhalilishe. Wachangiaji wote wa mwanzo mmetoa mawazo mazuri, ya kweli kuhusu kinachoendelea. Hongera wabunge wa (chadema kwa kuleta mabadiliko.

Hongera walionisahihisha kwa kunikumbusha kwamba ile ilikuwa ni Kamati ya Kanuni za Bunge wakati mimi nilikosea kwa kusema Kamati ya Maadili ambayo haipo.

Ni kweli ninaujua ukweli wote ambao ambao na nyinyi mnaujua kwamba Tundu Lissu alitutamkia kwamba amemfikisha Makinda kwenye Kamati ya Kanuni. Kwa mdomo wake Tundu Lissu alitamka kwamba Spika atatakiwa kulitangazia bunge uamuzi wa kamati hii kwa hili suala lake.

Kesho yake SPika Anne Makinda nae akahojiwa akarudia na yeye kusema kuwa yeye kama Spika anawajibika kulitangazia bunge uamuzi uliofikiwa na Kamati hii kwa mujibu wa Ibara5(5) ya bunge.

HIvyo Tundu Lissu na Anne Makinda kwa hili wanazungumza lugha moja kwamba uamuzi ule wa Kamati ni lazima utangazwe, tena hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni na wala si kwa mujibu baadhi ya wachangiaji wa JF ambao kwa upofu wa kuzijua Kanuni wanadhani ni siri au kukumbushia hili ni kuwataka CHADEMA wavunje kanuni na wajiabishe.

Kuna jamaa katuletea Kanuni za bunge kwenye hii post. Aliyejipa nafasi ya kuacha kukurupuka na kuzisoma amejihakikishia mwenyewe kuwa ile Kanuni 5(5) inasema hivi:

(Spika atawajibika kuitisha kikao cha Kamati ya Kanuni za Bunge na kulijulisha Bunge kuhusu uamuzi utakaotolewa na Kamati hiyo)

Hapa ndipo penye ugomvi wangu na hawa wabunge wa CHADEMA hasa Tundu Lissu. Kanuni hii inaonyesha wazi kuwa Tundu Lissu alipoenda kwenye vyombo vya habari kututangazia adhma yake ya kumshitaki Spika, na akatutangazia kuwa Kanuni hii inamwajibisha Spika kulitangazia bunge kilichojiri Kamatini, basi Tundu Lissu huyohuyo asifiikiri wote tutasahau na kuacha kulifuatilia jmabo hilo hadi mwisho.

Na mwisho wa jambo hilo si matakwa yangu mimi mleta mada. Msomaji asiekurupuka ameona wazi ni matakwa ya Kanuni kwamba Spika anatakiwa alijulishe bunge na ndipo watanzania tuone je Spika alidanganya bune au la. Na kama alidanganya bunge basi kumbe siku ile alimpendelea Waziri Mkuu. Hicho ndicho mimi njaa yangu tangu Tundu Lissu alipotutajia adhma yake.

Kanuni hii ingekuwa imetimizwa kwa Spika kulitangazia bunge uamuzi wa Kamati basi wote tungejua ni nani mkweli kati ya Tundu Lissu na Anne Makinda.

Labda niwakumbushe ili tuwe pamoja kimawazo kwamba mbona Kamati hii ya Kanuni za BUnge ilishughulikia kwa spidi kali suala la Tafsiri ya Kambi rasmi ya Upinzani. hOja ile ilishughulikiwa na ndani ya siku mbili ikatoa majibu kwamba tafsiri ya CHADEMA si sahihi na kwamba tafsiri ya kina Kafulila (NCCR) na wapinzani wengine ni sawa na ndipo kina Cheyo na Mrema wakapumua hadi kuongoza kamati zile mbili.

Iweje sasa kwa hili la SPika kushitakiwa kwenye Kamati ileile lichukue zaidi ya miezi watanzania tusitangaziwe uamuzi wakati hataKanuni inasema ni lazima tutangaziwe.

Jamani tukomae hadi tujue mwisho wake! Wenye uelewa zaidi watushuhie data. Kuna wabunge ambao ni JF members watuchushie data. Watu tuna hamu ya kujua ni nani alilidanganya bunge kati ya Tundu Lissu na Anne Makinda.

mi nadhani ungetuhamasisha tuutafute ukweli mpk tujue aliyeuza twiga na ndege wetu kwa waarabu tuwakamte kisha tuwaadhibu, lkn uhamasisho kwa ishu ya lisu na spika? mh.... We una lako na wabunge wa cdm ila fresh endelea kuhoji.

mi nadhani ungetuhamasisha tuutafute ukweli mpk tujue aliyeuza twiga na ndege wetu kwa waarabu tuwakamte kisha tuwaadhibu, lkn uhamasisho kwa ishu ya lisu na spika? mh.... We una lako na wabunge wa cdm ila fresh endelea kuhoji.

Kama uelewa wako umefikia kiwango cha mwisho ni bora ukae kimya uwapishe thinkers kibao ambao hawajosaoma hi na wanaweza kutoa majibu.

Hao wanyama walioibiwa issue isingeibuliwa huko bungeni ungeropoka nini leo hapa. Kabla ya kuhoj hao wanyama waliotoroshwa basi tuambie kwanza majibu ya waliohoji kuhusu Kagoda, Meremeta na wenzao tumepata majibu gani ya kuridhisha.

Ni rahisi sana kutuaminisha kuwa unaipenda CHADEMA wakati ukweli kamili unaujua kwamba hapa Tundu Lissu akikomaa basi Spika Anne Makinda lazima akisahau kile kiti na ndipo itakuwa adabu kubwa kwa yeyote atakayekikalia kiti kile.

Hili la ni gumu kwako kuling'amua unaishia kudhani kwamba Tundu Lissu kuhimizwa kazi hiyo ya kumuondoa Makinda kwa jinsi hii ya kitaalamu unadhani ni kuwa na jambo kwa wabunge wa CHADEMA.

Soma na tafakari. Data zipo tele humu.

Ninaungana na baadhi wanaosema kuwa mleta hoja anaujua ukweli wote. Ila siunganii hata kidogo na wanaoiangalia kwa ufinyu. Mimi ninaongezea kwamba hoja iliyo mezani inahitaji utulivu mkubwa na kama huna uzoefu na shughuli za bunge unaweza kuishia kuielewa kijuujuu.

Binafsi imenikumbusha Case Study yangu kwenye Political Science ambapo nili-centre research angu kwenye Legilastures.

Ukweli ni kwamba suala hili la Tundu Lissu ni maji mazito kwa Spika yoyote duniani. Mimi ninaamini kama kuna kosa ambalo Anne Makinda analiwaza kila siku basi ni hili la kuingilia jibu la Waziri mkuu siku ile na hatimaye akajikuta ameonea waziwazi kumlinda Mizengo Pinda ambaye ukweli ni kwamba siku ile asingekuwa na jiu zaidi ya kujiuma. Mauaji ya Nyamongo serikali ilikuwa imekaa tu bila tamko au action yoyote. Sasa, hapa Pinda angejibu nini!

Hivyo hapa kosa la Anne Makinda hapa ni kujibu swali kitu ambacho si kazi ya Spika maana kiutaratibu Spika haulizwi swali. Wabunge wako mle ili kuuliza serikali yao na si kupata majibu toka kwa Spika. Majibu ya SPika ni yale yanayohusu utaratibu wa kuendesha mjadala kwa kufuata Kanuni.

Sasa Spika Anne makinda akachukua majukumu kinyume na bado akakosea. CCM wakawa wamependelewa na CHADEMA wakawa wamebaguliwa.

Kinga ya mle bungeni ni iwapo suala halihusiani na kuvunjwa Katiba. Spika hawezi kuchukua bastola akampiga risasi mbunge wa CHADEMA mle ukumbini halafu useme eti ana kinga. Akifana hivyo anakuwa ameua na kwenye Katiba hii ni kukaidi haki ya kuishi. Hivyo kwa mujibu wa Katiba Spika huu anatakiwa ajiuzuru hata kama asilimia 100 ya wabunge wanamtaka. Kwa sababu bunge haliko juu ya Katiba eti hata SPika akiivunja bsi kwa wingi wao watamrudisha.

Maamuzi ya Spika au bungeni huwezi kuyapinga kama yameendeshwa kwa msingi wa kanuni za mle bungeni. Lakini yanaweza kabisa kupingwa mahakamani kama yamejengwa kwa msingi kwamba ama Spika au mbunge au bunge zima limekiuka katiba.

Hapa ni wazi Spika Anne Makinda amekiuka Katiba kwa kufanya upendeleo. Hii kesi si ya juujuu. Inawezekana tunapiga kele hivi lakini Tundu Lissu amelipangia muda wake suala hili. Lakini sisi JF hatuna haja ya kumsubiri maana tunajadili kuongeza ujuzi wetu.

Mimi ninachoweza kulaumu ni kwa nini wabunge wengine wasimiminike kwanza kwene Kamati hii ili ktakachofuata baadaye kifuate. Mfamo, Lema na Zitto, Spika kaukalia ushahidi wao aliowalazimisha waulete wakamletea. hadi leo kimya. Hapa Zito, Lemma na wengine tunatakiwa ama tuwashinikize na wao wamfikishe huyu mama kwenye kamati hii ndipo tuone moto ule wakti Tundu Lissu akisubiri Kamati ikizidi kuleta kujivuta bila kuitishwa basi alipeleke suala hili mahakamani.

Spika Anne Makinda si mwanasheri lakini naamini anayajua haya yote ninayofafanua humu. Ninachohisi anaweza kabisa asiitishe Kikao cha kamati hii kwa kipindi chote cha Uspika wake yaani hadi 2005. Ilivokaa hii kuitisha maana yake yeye ajiandae kuondoka kitini. Itakuwa ni moja ya scandal chache sana duniani SPika kuondolewa kitini na bunge lenye minority opposition.

Tundu Lissu akae akilijua hili, kwamba asitarajie Spika Anne Makinda aitishe kamat hii. Badala yake ameanza kuonyesha kuwabebabeba wapinzani mbinu ambayo imeshawadanganya hata baadhi humu JF huku akijua kuwa kesi ya Tundu Lissu ni mwiba asioweza kuuepuka.

Nawasilisha.

Wewe changia hoja kuu na siyo kuanza kumponda mtoa mada. Mara tena unaanza kusifia wachangaiaji wengine. Sasa tukuelewe vipi?
na

kwani mchango we unautafsiri vipi, kwani hata huko bungeni ili kupitisha hoja lazima upate support na ndivyo nilivyoona mimi hapa. Huyu mtoa mada alipaswa atuambie utaratibu ni upi unaofuatwa na kuonesha kuwa hawa cdm hawaufuati katika kumaizia hoja wanzozianzisha! Lini mara ya mwisho aliposikia kamati ya maadili imetoa nje kile ilichozungumza?

na

kwani mchango we unautafsiri vipi, kwani hata huko bungeni ili kupitisha hoja lazima upate support na ndivyo nilivyoona mimi hapa. Huyu mtoa mada alipaswa atuambie utaratibu ni upi unaofuatwa na kuonesha kuwa hawa cdm hawaufuati katika kumaizia hoja wanzozianzisha! Lini mara ya mwisho aliposikia kamati ya maadili imetoa nje kile ilichozungumza?

Tatizo kubwa la magamba ni kwamba pamoja na vijisent vyao lakini ni wabahiri na hawapendi kutumia watu brilliant kamwe. Iwe ni kwenye media, iwe ni maofisini wanatumia vilaza hasa hawa waliopitia vyup vya kata hata kama ni vile vya ng'ambo ili kukamilisha kazi yao ya kupeleleza.

Wewe umetumwa kuja kupeleleza humu JF badala ya kutumia akili unatumia makalio kutuambia habari za Kamati a Maadili wakati huwezi kumtaja mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa sababu bunge halina Kamati ya maadili.

Fikiri kwanza kabla ya kuboneza keyboard, hap wamejaa magenious hata kama hawasemi. Post hii imesomwa na watu zaidi ya 1,100 hivyo si lazima tuone ni aina gani ya ignorance uliyo nayo.

Naishia hapa nisije maana nikiendeleea utanifanya nipigwe ban.

Wewe changia hoja kuu na siyo kuanza kumponda mtoa mada. Mara tena unaanza kusifia wachangaiaji wengine. Sasa tukuelewe vipi?
kumbe unajua kiswahili fasaha kasoro hapo kwenye red,.lakini sio sawa na kile kiingereza chako cha kuandika ukiwa umeshikilia dictionary mkononi

Actually cdm hawamwogopi makinda kinacho endelea ni mchakato tu kwani hata ikibainika kuwa Tundu Lissu alionewa itapotezewa tu kama ilivyopotezewa ya Lema na Pinda. KIGUMU CHAMA CHA MAGAMBA

mi nadhani ungetuhamasisha tuutafute ukweli mpk tujue aliyeuza twiga na ndege wetu kwa waarabu tuwakamte kisha tuwaadhibu, lkn uhamasisho kwa ishu ya lisu na spika? mh.... We una lako na wabunge wa cdm ila fresh endelea kuhoji.

Wale ambao ama hamkuizingatia au mlishindwa kuielewa hii thread yangu naona baadhi mnakimbizana kumshambulia Zitto Kabwe ambaye kama Waziri kivuli wa Fedha amesifia Spika Anne Makinda na anawashangaa waliouponda uongozi wake. Thread mnayofukuzana nayo sasa ni hii hapa chini:

{www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/167077-zitto-apingana-na-chadema-ampongeza-spika-anne-makinda-kwa-uongozi-mahiri.htmlhttps://www.jamiiforums.com/jukwaa-...za-spika-anne-makinda-kwa-uongozi-mahiri.html}

Nadhani mnavyozidi kufukuzana huko mimi kiasi fulani nimefarijika na kupata majibu kidogo kuwa inawezekana Tundu Lissu na CHADEMA hawana mpango kabisa kuiendeleza ile kesi japo walikuja na sauti nyingi kwamba ni lazima wapate matokeo ya kesi ile kwa nini Spika anaukali ushahidi wa Lema, Zitto na kwa nini yeye mwenewe Tundu Lissu alizuiwa swali lake kwa Waziri mkuu.

Endeleeni kupambana huko kwenye thread ile lakini ukweli nilioueleza unabaki palepale kwamba CHADEMA au Chama chochote wasidhani kila mmoja ni bingwa wa kusahau. Ukitueleeza kuwa umemshitaki Spika au nani tupo ambao ni wafuatiliaji hadi siku ya mwisho.

Mimi sasa naweza kubadili kwamba kumbe si kwamba CHADEMA wanamuogopa Anne Makinda bali kumbe wanamkubali japo sina hakika kama wamesamehe kwa sababu hawajatutangazia.

Wewe changia hoja kuu na siyo kuanza kumponda mtoa mada. Mara tena unaanza kusifia wachangaiaji wengine. Sasa tukuelewe vipi?

Nampenda sana Mwita maana hoja zake mara zote ni za kuchangamsha wana-jamvi. Hongera sana Bwana Mwita.

Back
Top Bottom