CHADEMA wanamwogopa Anne Makinda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA wanamwogopa Anne Makinda?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SubiriJibu, Aug 20, 2011.

1. S

SubiriJibu JF-Expert Member

#1
Aug 20, 2011
Joined: Jun 26, 2009
Messages: 1,128
Likes Received: 779
Trophy Points: 280
Tundu Lissu alikuja na mkakati mzito wa kumshataki Spika Anne Makinda kwenye Kamati ya Maadili kwa kitendo chake cha kumzuia asijibiwe swali alilomuuliza Waziri Mkuu kuhusu mauaji a Nyamongo.

Spika Anne Makinda aliingia kwenye mtego wa swali kwamba lilikuwa liko mahakamani kwa vile Tundu Lissu mwenyewe ni mshitakiwa wa kesi hiyo.

Lakini ukweli ni uliothibitishwa na Tundu Lissu ni kwamba hakuwa na kesi ya mauaji na hivyo SPika alilidanganya bunge kusema Tundu Lissu ana kesi. Vilevile SPika alimpendelea Waziri Mkuu Pinda kwa kumzuia asijibu swali lile.

Kesho yake tu tukaona Tundu Lissu amejaza magazeti kwamba anadhamiria kuapeleka kesi kwenye Kamati moja ya Bunge nadhani ya Maadili. Haikupita wiki akapeleka na magazeti yote yakaandika SPIKA ASHITAKIWA KWENYE KAMATI.

Swali langu ni kwamba, siku zimepita na bunge ndiyo hivyo liko katika dakika zake za mwisho katika mkutano huu wa bajeti. Tundu Lissu ameamua kuwa kimya ghafla na inawezekana bunge liishe tusijue kilichoamriwa na kamati ile.

Hii inamaanisha kwamba huenda Tundu Lissu na CHADEMA kwa ujumla wana lao jambo. Kama ni kweli walionewa mle bungeni mbona tunawasikia kimya tu.

Nakumbuka walianza na kulalamika Sofia Simba kuchaguliwa kamati ya SADEC bila kuhojiwa na hivyo kuvunjwa kwa kanuni. Vikafuata visa vingi kama Spika kukalia ushahidi zaidi ya mara tano ukiwemo wa Lema, Zitto, Wenje nk.

Walau kidogo Tundu Lissu tumeona akifisha malalamiko yake kwenye Kamati. Wengine hawachukui hatua zaidi zaidi ya kusikia wana-chadema wanaishia kulalamika tu kwenye vyombo vya habari.

Mimi nimeanza kuwa na wasiwasi na tatizo lililomo kwa wabunge wa CHADEMA. Hawajatuonyesha kwamba SPika akiukalia ushahidi ni hatua gani utaichukua. Tundu Lissu hajatuonyesha kwamba Kamati isipokaa atachukua hatua gani inayofuata.

Vinginevyo basi CHADEMA inajitengenezea mazingira ya kuonekana kwamba ni chama kilichokata tamaa na kuishia kutangaza maonevu badala ya kuashughulikia. Na kwa hili ni wazi kabisa wabunge wa CHADEMA wanamuogopa SPika hata kama kwa maneno hawataki kusema hivyo.

Na kama maandamano ndiyo strategy yao basi kwene maandamano wajieleze ni hatua gani huko bungeni ambazo wameshachukua dhidi ya Spika ndipo tuone kama inapaswa tuwasaidie kuzikamilisha kwa maandamano.

Nishie hapa mengine nitajadili zaidi kutokana na michango ya watu.

2. F

FJM JF-Expert Member

#2
Aug 20, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 8,088
Likes Received: 90
Trophy Points: 145
Kama wewe ni mfuatiliji mzuri utagundua kuwa tangu siku Lissu aliposema kuwa CHADEMA wanamshitaki Spika Makinda kwenye kamati ya uongozi, huyu Spika kabadilika kabisa. Yale mapembe yaliyokuwa yanaota kwa kasi ya kutisha yamepotea katika mazingira anayojuwa mwenyewe Spika!

Ni juzi tu Spika kaitaka serikali kutoa tamko juu mgao wa umeme na hii ilitokana na hoja wa Wenje kuwa mgao wa umeme ujadiliwe. Hii ni tofauti kabisa na alivyokuwa huko nyuma huyu mama!

3. W

We know next JF-Expert Member

#3
Aug 20, 2011
Joined: Sep 9, 2010
Messages: 664
Likes Received: 1
Trophy Points: 35
Naweza kuamini kuwa kamati ya maadili ya Bunge ilimkalisha kitako Mama Makinda na kuzungumza naye hilo suala. Nasema hivyo kwa sababu, hata kile kitendo chake cha wiki iliyopita kusema kuwa hawezi tena kuhudhuria vikao vya kichama vya CCM ili asije akasombwa na uwajibikaji wa pamoja na kuharibu kazi yake ya Spika. Lakini pia, si busara sana kujua Kamati ya maadili ya Bunge imezungumza mambo gani na hatua gani zimechukuliwa. Navyo fahamu, kamati hii inashughurika moja kwa moja na Nidhamu ya Wabunge, kwa mantiki hiyo si rahisi kutoa kila jambo linalojadiliwa huko, na ninadhani kuna vifungu vya sheria vinavyowataka kufanya hayo mambo yao kwa siri. Isitoshe, nidhamu binafsi ya mtu ni siri ya muajiri wake, unless inavuka mipaka na kutakiwa kuwekwa hadharani. Nina imani Mama Makinda aliwekwa kikao.

4. h

hoyce JF-Expert Member

#4
Aug 20, 2011
Joined: Oct 26, 2010
Messages: 1,119
Likes Received: 14
Trophy Points: 135
Mtoa hoja anajua ukweli wote na ni mfuatiliaji, bali anataka kuwachochea wabunge wa chadema walipuke nje ya kanuni, ili waidhalilishe. Wachangiaji wote wa mwanzo mmetoa mawazo mazuei, ya kweli kuhusu kinachoendelea. Hongera wange wa (chadema kwa kuleta mabadiliko.

5. f

fukunyungu JF-Expert Member

#5
Aug 20, 2011
Joined: May 16, 2011
Messages: 726
Likes Received: 29
Trophy Points: 45

asante mkuu.

6. Mwamikili

Mwamikili JF-Expert Member

#6
Aug 20, 2011
Joined: Mar 24, 2011
Messages: 416
Likes Received: 14
Trophy Points: 35
nipeni majina ya wajumbe wa hiyo kamati!

7. Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

#7
Aug 20, 2011
Joined: Nov 25, 2010
Messages: 31,797
Likes Received: 36,829
Trophy Points: 280
Subiri siku ambayo Lissu atasoma bajeti ya wizara yake kivuli husika utapata majibu ya maswali yako na m'badala wa imaginations zako zooote.

8. Mwita25

Mwita25 JF-Expert Member

#8
Aug 20, 2011
Joined: Apr 15, 2011
Messages: 3,840
Likes Received: 18
Trophy Points: 0

Wewe changia hoja kuu na siyo kuanza kumponda mtoa mada. Mara tena unaanza kusifia wachangaiaji wengine. Sasa tukuelewe vipi?

9. Calnde

Calnde JF-Expert Member

#9
Aug 20, 2011
Joined: Oct 7, 2008
Messages: 1,373
Likes Received: 8
Trophy Points: 0
Mtoa hoja kama wengine wote walivyosema anaufahamu ukweli. Labda niseme kwamba bunge ni moja wapo ya mihimili mitatu ya dola. Kwa

maana hiyo bunge limejiwekea utaratibu wa kuadabishana katika mfumo wa mashtaka kama ilivyo mahakama. Sasa ukishapeleka kesi mahakamani

huwezi kuandamana ili jaji atoe maamuzi. Na wakati mwingine hatuambiwi the actual decision kutokana na mfumo wa nidhamu ulivyo. Mimi nadhani

hatupaswi kumlalamikia aliyeshtaki kwanini ama hatupi maendeleo ya kesi yake au jaji anayepaswa kuamua hatoi maamuzi. Nadhani yule

anayeamua ndo anapaswa kuhojiwa!

10. Laurence

Laurence JF-Expert Member

#10
Aug 20, 2011
Joined: Jun 11, 2011
Messages: 3,106
Likes Received: 37
Trophy Points: 145

Hivi wewe haitokei siku ukaongea vitu vyenye mantiki? nina wasiwasi na elimu yako na uwezo wako wa kufikiri,mbona huyo jamaa kazungumza vizuri tuu au wewe kila kitu kibaya kwako? hebu badilika wewe

11. Calnde

Calnde JF-Expert Member

#11
Aug 20, 2011
Joined: Oct 7, 2008
Messages: 1,373
Likes Received: 8
Trophy Points: 0
Hiyo nayo ni staile yake yakuchangia! Au kuna mwongozo wa namna ya mtu kurespond hoja? As long as haja offend mtu we have to be positive

with his/her comments

12. Rejao

Rejao JF-Expert Member

#12
Aug 20, 2011
Joined: May 4, 2010
Messages: 9,239
Likes Received: 244
Trophy Points: 160
Hivi bado tu mnatumia energy yenu kuwadiscus hawa Chadema?
Hawana msaada wowote kwa mwananchi! kazi kuandamana tu na kufanya vurugu ambazo wanaishia kuumia wenyewe!

13. mopaozi

mopaozi JF-Expert Member

#13
Aug 20, 2011
Joined: Nov 17, 2010
Messages: 3,290
Likes Received: 105
Trophy Points: 160
Makinda ameogopa kuendelea kupoteza umaarufu wake kama supika wa kike tz angeendelea cdm wangemtoa uspika!!

14. zomba

zomba JF-Expert Member

#14
Aug 20, 2011
Joined: Nov 27, 2007
Messages: 17,081
Likes Received: 49
Trophy Points: 0
Unaharibu hapo kwenye nyekundu, unatoa ladha ya jibu lako lote.

15. Mwita25

Mwita25 JF-Expert Member

#15
Aug 20, 2011
Joined: Apr 15, 2011
Messages: 3,840
Likes Received: 18
Trophy Points: 0

wewe nawe unaingia humu ili kufuatilia comments zangu au kuchangia hoja? Unawezaje kuwa na wasiwasi na kiwango changu cha elimu ilihali we mwenyewe unatumia masabuli kufikiri!

16. Radhia Sweety

Radhia Sweety JF-Expert Member

#16
Aug 20, 2011
Joined: Aug 10, 2011
Messages: 4,448
Likes Received: 345
Trophy Points: 180

Achana naye huyo inaelekea visabuli vyake vyembamba sana

17. K

Kieleweke Member

#17
Aug 20, 2011
Joined: Jun 23, 2009
Messages: 79
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Mtoa hoja kawapotosha wote na nyinyi mkaingia kichwakichwa. Kwanza kabisa Kamati ya Maadili ilikuwepo kipindi cha Spika Pius Msekwa ikiongozwa na Mh. Simpasa. Wanaokumbuka kamati hii iliwahi kungia mzozo na mama mmoja sijui yuko wapi siku hizi aliitwa Mama Terry. Kamati hii ilikufa kipindi cha Spika Samwel Sitta hivyo bungeni sasa hivi hakuna kitu kinaitwa Kamati ya Maadili.

Kamati iliyopo ni Kamati ya Kanuni za Bunge na ndiyo Kamati ambayo Tundu Lissu aliamua kumshtaki huko Spika Anne Makinda kwa kutumia kifungu 5(4) cha Kanuni za Bunge za toleo la mwaka 2007.

Kwanza mtoa mada na nyinyi mlitakiwa mpitie thread iliyojadil haya kwa kina hadi tukaona jinsi Spika anavyoweza kuondolewa bungeni hata kama ni mbunge mmoja tu kaleta hoja ya kuonewa na waliobaki wote wanampenda. Wengi wanakimbilia kuangalia wingi wa wabunge wa CCM lakini tulilijadili sana hili kwenye thread hii: {www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/160091-tahadhari-kwa-anne-makinda.html}. Hivyo mtoa mada asiturudishe kule tulikokwishaelewa labda kwa wasiopenda thread zilizoenda shule.

Mkuu, unaweza kuonekana kuwa una busara za hali ya juu katika kuelemisha. Lakini kwa anayjishughulisha kutafiti atakubaini kuwa wewe ni mpotoshaji wa hali ya juu kwa sababu unaongea unayofikiria na si ukweli uliotafitiwa.

Nimeshasema Kamati aliyotumia Tundu Lissu ni Kamati ya Kanuni za Bunge kwa kutumia Kanuni 5(4). Na wakati Tundu Lissu anatutangazia ushitaki wake alitusomea na kanuni 5(5) ambayo inamlazimisha Spika kutangaza maamuzi ya Kamati hiyo, na hivyo wewe unayesema kuwa maamuzi ya Kamati hii ni siri sijui unawaza kwa kutumia kiungo gani cha mwili wako wakati wenzako tunawaza kwa kutumia ubongo unaotufanya tukimbilie kusoma Kanuni za Bunge.

Hata Spika Makinda angekuwa anasoma JF halafu akaona hii point yako naamini angeishia kukushangaa kwani alipoulizwa swala hili na waandishi hakujibu kama unavyotuaminisha hapa. Alijibu kuwa yeye ni mwenyekiti wa Kamati hiyo lakini ktk hii kesi ya Tundu Lissu, kifungu 5(6) cha Kanuni za Bunge kinamlaimisha yeye na Naibu Spika wasiwe wajumbe wa Kamati na Kamati itachagua Mwenyekiti atakayeendesha kesi hiyo.

Anayetaka kuthibitisha nimeamua ku-attach Kanuni za bunge the latest version (2007) kwenye hii post yangu.

Majina si tatizo Tundu Lissu ni mwanasheria aliyebobea. Lakini kama unataka majina ya wanakamati hii basi hapo juu tayari una majina ya Anne Makinda na Job Ndugai ambao ni Spika na naibu wake ambao kwenye kesi hii hawatakuwemo.

Kwanza kwa mujibu kwa Kanuni za Bunge kwenye "Nyongeza ya NANE", Kifungu 3(1) Kamati hii inatakiwa kuwa nawajumbe wafuatao:

(a) Wajumbe watakaoteuliwa na Spika;
(b) Kiongozi wa Upinzani au Mwakilishi wake;
(c) Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Mwakilishi wake.

Hapo kwenye RED huhitaji kujua maana huyo ni Freeman Mbowe ambaye anaingia kwa nafasi yake hiyo. Kwenye bluu unajua ni Jaji Werema.
Waliobaki 13 ni kama ifuatavyo na utagundua kuwa ni kamat iliyosheheni wanasheria:

01: Tundu Lissu
02: Mustapha Akunaay
03: Felix Mkosamali
04: Hamad Rashid Mohamed
05: Habib Mnyaa
06: George Simbachawene
07: Anna Abdallah
08: Nimrod Mkono
09: Angela Jasmine Kairuki
10: Andrew Chenge
11: Makani Matala
12: Pindi Chana
13: William Lukuvi​

Sijajua kama unataka kupindisha hoja hii nzito kwa kujadili majina au la. Tutaona lengo lako kadiri michango inavyowasilishwa. Siwezi kuwapangia CHADEMA maamuzi lakini binafsi pia nina shauku kubwa ya kujua ni nini hatima ya kesi hii maana hii ni mara ya kwanza Spika anashtakiwa kwenye Kamati tangu tupate uhuru na hivyo tujumuike kujua hatima hii itakuwaje.

18. Shine

Shine JF-Expert Member

#18
Aug 20, 2011
Joined: Feb 5, 2011
Messages: 11,514
Likes Received: 16
Trophy Points: 0

Mkuu kama hujaona msaada wao tupe msaada wa magamba aka makamba

19. mchillo

mchillo JF-Expert Member

#19
Aug 20, 2011
Joined: Oct 13, 2010
Messages: 433
Likes Received: 15
Trophy Points: 35
Acha kukejeli watanzania wewe. Naona umevimbiwa sumu ya ufisadi mithili ya panya. Wenye msaada ni CCM iliyosheheni vibaka kuanzia juu hadi chini? Msitukumbushe machungu ya ufisadi mlioufanya ulioidunisha nchi yetu kwa miango kadhaa sasa; wenyewe mkijitapa kwamba eti mnaupaisha uchumi. Kumbe ni uchumi wenu, vimada na watoto wenu. Ipo siku mtafanywa mtapike vyoote mlivyofakamia. Mlaaniwe nyinyi na CCM yenu.

20. Michael Scofield

Michael Scofield JF-Expert Member

#20
Aug 20, 2011
Joined: Jul 30, 2011
Messages: 1,218
Likes Received: 5
Trophy Points: 135
I think kieleweke, kaeleweka.

Loading...