CHADEMA, Wanaharakati waalikeni waungwana mpatanishwe

Dr. Slaa ni mwanasiasa mwanaharajati anayejitambua. Huyu SI mwanasiasa usu wala mwanaharakati usu. hao wote wameelezewa humu:

Tuzitambue tofauti za vyama vya upinzani (ACT, CHADEMA, CUF, nk) na Wanaharakati

Ni sahihi kabisa usemavyo:

1. Mwanasiasa mwanaharakati huwa uanaharakati wake haukomi kwani Serikali madarakani haiwezi kufanya yote waystayo wananchi.

2. Mwanasiasa mwanaharakati anayejitambua atashutumiwa wanasiasa usu kwani ni nia yenu kutaka kumtumia kama grader kufikia malengo yenu.

Kumhusu mwanasiasa mwanaharakati ni haya hapa:

a) Kwenye katiba mpya na bandari: Atataka katiba mpya sasa. Biashara ya bandari haipo, sasa na hata milele.
b). Atasimama na wananchi siku zote.
c). Huyu si kigeugeu. Agenda za wananchi kwake ni za kudumu.
d). Akiitisha maandamano atakuwapo mstari wa mbele. Yuko tayari kufa au hata kufungwa badala au kwa niaba ya wananchi wake.
e) Siyo mnafki, ni muwazi na anachosema au ukimwangalia, (usoni) ana maanisha.
f) Ni kipenzi cha watu.
g) Hushawishi kwa nguvu za hoja si kwa hoja za nguvu.
h) Huyu huwa na wafuasi wa dhati, siyo wafuasi wa kulipwa (chawa). Hoja zake zajiuza. Hahitaji kukingiwa kifua.
I) Amedhamiria. Lugha yake, adui huielewa Kwa ukamilifu wake.
Huyo Dr.Slaa ni kigeugeu, hana anachokisimamia na hajitambui, labda uzee. Alikuwa chadema baada ya kuiona ana nguvu kuliko chama akaanza kukitikisa, alipoona hakitikisiki alijiondoa kwa mbwembwe akidhani CHADEMA ingekufa, haikufa. Sasa karudi badala kufanya yanayomuhusu na hilo dubwasha lake la sauti ya watanzania, anataka kuihujumu chadema.
Hana maana tena, na hana sifa unazompa. Unapoteza muda wako kwa huyo Dr.Slaa.
 
Umeondika kama nabii au supernatural au umeongea nao. Ukiambiwa thibitisha utaweza? Je ni Slaa, mwanaharakati aliye na taabu na CDM pekee siku za Hapa karibuni?

Kwani kina huko nje nako, hapa ndani
napo imekuwa je?

Waungwana wanasemea ukienda kunyoa, vinyozi 5 wote una taabu nao shida inaweza kuwa ni kichwa chako!

Kwa vile hatuna access na supernaturals, hudhani hawa:

"Sheikh Ponda, Askofu Bagonza, Askofu Niwemugizi, Prof. Shivji, Askofu Mwamakula (pole zake kwa msiba) nk, nk, kwenyo jopo la upatanisho wangetuvusha kutoka kwenye huu umimi:

1664543999224~2.jpg
 
Back
Top Bottom