Chadema wamtimua m/kiti wa serikali ya mtaa

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Chama cha demokrasia na maendeleo jimbo la ukonga, kimetekeleza kwa vitendo sera yake ya kutaka viongozi wa umma wawe na uadilifu usiotiliwa shaka na jamii wanayoiongoza. Ktk kutekeleza hilo kwa vitendo, Kamati ya utendaji ya Jimbo hilo limethubutu kuchukua hatua za kinidhamu na kumsimamisha uanachama M/Kiti wa serikali ya mtaa wa Yange yange, kata ya Msongola manisipaa ya Ilala kwa utovu wa nidhamu.

Kamati ya utendaji ya Chadema jimbo la ukonga, lilifanya kikao cha dharura jana tarehe 21/06/2011 na kumsimamisha uanachama Mr Colman ambaye ni m/kiti wa serikali ya mtaa wa Yange yange, kata ya msongola manisipaa ya ilala kwa kuvunja kanuni za chama na sheria za nchi na kukipaka chama matope mbele ya jamii.

M/kiti huyo alisimamaishwa kutokana na makosa yafuatayo.
1) Hivi karibuni amekumbwa na kashfa ya kupiga watu 2 kinyume na sheria za nchi na kanuni za chadema. Colman alimpiga nurse wa Kituo cha afya kilichopo pale Yange yange na afisa mtendaji mstaafu wa kata ya Msongola kwa nyakati tofauti. Tuhuma ambazo ziliandikwa sana na magazeti ya mwananchi, majira nk.

2) Ameshindwa kushirikiana na wajumbe wenzake wa serikali ya mtaa kupitia Chadema na hivyo kujifanyia mambo yake mwenyewe, huku akigombana nao wajumbe hao mara kwa mara.

3) wakati wa uchaguzi wa Mwaka 2010, akiwa m/kiti wa serikali ya mtaa kupitia Chadema, alimpigia debe diwani wa CCM kata jirani ya Kivule kinyume cha sera, kanuni na katiba ya Chadema. Kosa hili alikiri akasamehewa huko nyuma.

Kutokana sababu hizo, Kamati ya utendaji limemsimamisha rasmi uanachama m/kiti huyo kwa kutumia katiba ya chadema (5.4 Kifungu kidogo cha 3) kuanzia 21/06/2011 na kwa maana hiyo, amekosa pia sifa ya kuwa mkiti wa serikali ya mtaa.

My take, Habari hii inakuja wakati ambapo m/kiti wa Taifa Mr Freeman Mbowe na wabunge wenzake wameibana serikali bungeni kuhusu Posho, huku kukiwa na tetesi kwamba Dr Wilbrod Slaa anajiandaa kwenda kukijenga Chadema Pwani akianzia na wilaya ya Kisarawe. I am anxiously waiting for 2015.
 
Chadema wanatakiwa kufunga usajili wa wote wanaotoka Magamba na kufanya usajili wa walalahoi
 
Contradiction na sera za chama. Wapiganaji! mlitegemea waweje? Mnanshangaza!
 
chama makini ni kile kinachojali na kufata katiba yao. Big up CHadema. Uamuzi at fingertips
 
Contradiction na sera za chama. Wapiganaji! mlitegemea waweje? Mnanshangaza!

Hapo lazima ushangae, kwakuwa ndani ya chama cha magamba hamna uthubutuhata wa kuwapa barua za kujieleza watuhumiwa wa ufisadi sembuse kuwasimamisha!!??

Ombeni msaada chadema, iwasaidie kuwakabidhi barua mapacha watatu na kisha baadae kuwatimua ndani ya magamba.
 
Inatufundisha kuwa makini zaidi katika kuwapata viongozi safi na bora...hii ni challenge ukizingatia chama kinakua kwa kasi na watu wanatake positions,Usafi wa mtu ni muhimu sana.
 
Back
Top Bottom