Elections 2010 CHADEMA wambwaga MO Singida mjini!

MGOMBEA urais wa Chadema, Dk.Willibrod Slaa na mkewe mpya, Josephine Mushumbusi, watafunguliwa kesi wakidaiwa fidia ya Sh bilioni moja na mume wa ndoa wa Josephine, Aminiel Mahimbo.

Kesi hiyo itakayofunguliwa leo katika Mahakama Kuu inawataka Slaa na Josephine kulipa fidia hiyo kutokana na mgombea huyo kudaiwa kumnyang'anya mke Mahimbo na Josephine kuvunja mkataba wa ndoa ya mke na mume mmoja.

Mwanasheria wa Mahimbo, Abduel Kitururu, aliwaambia waandishi wa habari jana Dar es Salaam, kuwa kesi hiyo imeshaandaliwa ikiwa ni pamoja na vielelezo vyote; vyeti vya ndoa, vya kuzaliwa watoto wawili na picha za ndoa.

Alisema, mteja wake anadai fidia ya Sh milioni 200 za usumbufu aliopata baada ya Slaa kumtangaza mkewe wa ndoa kuwa mchumba wake, huku akijua ni kinyume cha sheria.

Alisema Sh milioni 800 ni hasara za jumla ambazo wanaamini madhara aliyopata yanalingana na gharama hizo na anastahili kulipwa kabla hajafungua kesi nyingine kwa mujibu wa sheria ya ndoa, itakayoshughulika na masuala ya talaka na malezi ya watoto.

"Kwa sasa tunafungua kesi ya madai ya fidia kutokana na Dk. Slaa kumnyang'anya mteja wangu mkewe wa ndoa na kumtangaza kwenye majukwaa kuwa ni mkewe na pia Josephine kuvunja mkataba wa ndoa uliosainiwa kanisani na si suala la sheria ya ndoa," alisema Kitururu huku akionesha nakala ya cheti cha ndoa ya Mahimbo na Josephine.

Alisisitiza kuwa kesi hiyo haitahusu sheria ya ndoa wala malezi ya watoto, kwani kwa mujibu wa sheria, aliyeoa au kuolewa kidini kwa ndoa ya mke na mume mmoja, haruhusiwi kuoa wala kuolewa wakati mwenziwe yuko hai, labda ndoa hiyo ikibatilishwa na kuwa ya wake wengi.

"Ndoa ni mkataba na mmoja anapouvunja anapaswa kumlipa fidia mwenzake … mteja wangu anapaswa kulipwa fidia kwa Josephine kuvunja mkataba na suala hili halina uhusiano wowote wa kisiasa, bali imetokea kama ajali tu wakati huu siasa zikipamba moto," alisema kuondoa hisia kuwa suala hilo lina uhusiano na kampeni za kisiasa zinazoendelea.

Alisema mteja wake alifika katika ofisi yake kuitaka kufungua kesi hiyo ya madai dhidi ya Slaa na Josephine, kutokana na kunyang'anywa mke wa ndoa waliyofunga katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama na kufungishwa na Mchungaji Lewis Hiza wa kanisa hilo.

Alisema wakati huo, Mahimbo alikuwa na miaka 30, Josephine akiwa na miaka 26 na mashahidi wao wa ndoa walikuwa ni Sam Paul na Roselyn Paul na baada ya ndoa hiyo, walipata watoto wawili Upendo mwaka 2003 na Precious mwaka 2007.

Alidai katika ndoa yao waliishi Kimara Baruti na mwanzoni mwa mwaka huu, Josephine alianza safari za mara kwa mara na mumewe kuamini ni za kikazi lakini Aprili mwaka huu, aliondoka nyumbani kwao na watoto.

Kitururu alidai kwamba Mahimbo alifanya uchunguzi na kubaini kuwa wawili hao wanaishi hotelini na kwenda kuona watoto wake, na akaelezwa na mmoja wa wafanyakazi hotelini hapo kuwa mkewe anaishi na Slaa mbali ya hivyo Slaa amekuwa akimtangaza katika mikutano ya kampeni kuwa Josephine ni mkewe, wakati bado hajaachana na mumewe.

Akizungumzia suala hilo, Slaa alisema hana wasiwasi na kufunguliwa kesi na kutaka Mahimbo aulizwe wakati anaporwa mkewe yeye alikuwa wapi.

Alidai kuwa hizo ni kampeni chafu za kutaka kumharibia katika kipindi hiki na kwamba zinafanywa na CCM na kudai kuwa chama hicho kimemnunulia gari Mahimbo ili amchafue.
 
haya ni maamuzi ya haki, wameamua kwa kufata kanuni, hawa ni weledi kwa hapa kwa mujibu wa CHADEMA

ila wangeamua vyengine basi wamechaguliwa na rais ambaye ni CCM kwa hio hawawezi kuiangusha CCM. nyinyi ni watu wa ajabu









bibie wa mambo ya pwani mbona hueleweki?
 
MO aendelee na biashara yake ya kulangua mazao ya wakulima kwa bei nafuu wakati wa mavuno ya kuyauza nje ya nchi - huku kwenye siasa ana ajenda gani ya siri? ana uchungu na wana Singida na taifa hili kwa ujumla? mwaka huu kazi anayo.

Hivi ile statement ya mkulu ya kuwaambia wanasiasa wachague kati ya biashara au siasa ilifikia wapi? Unajua haya mambo mawili kuyaendesha pamoja ndiyo sometimes unaambiwa mara ni conflict of interest and so on. MO hawezi poteza muda wake bure, kuna raha ya kuimarisha biashara hapa lo! Akienda Bungeni wala hatafungua mdomo wake na mwisho wa siku atalipwa allowances, salary and gratuity at the end!!
 
mi mi nilifikiri muheshimiwa MO ametolewa kwenye kinyang`anyiro! ..? nilitaka kustuka! kwani singida ingepoteza mpiganaji muhimu sana bungeni
Upiganaji wa MO ni wa namna gani wakati yupo Bungeni?
 
haya ni maamuzi ya haki, wameamua kwa kufata kanuni, hawa ni weledi kwa hapa kwa mujibu wa CHADEMA

ila wangeamua vyengine basi wamechaguliwa na rais ambaye ni CCM kwa hio hawawezi kuiangusha CCM. nyinyi ni watu wa ajabu

mkuu umesomeka, ikishindwa ccm ok, ikishindwa chadema, mama yangu hakuna hakiiiiiiiiiiiiii
 
mkuu umesomeka, ikishindwa ccm ok, ikishindwa chadema, mama yangu hakuna hakiiiiiiiiiiiiii


chadema hawako fair, na si watu wa demokrasia wao wanajiita wanaharakati na wapenda haki, haki gani hawa wanayoizungumzia?


niwe mkweli CCM ni chama dola lkn ni wasikivu, si kuwa hawafanyi rafu la. wanafanya ila wakienda kwenda kwenye sheria na ikaamuliwa kuwa wamekosea sawa hawana malalamiko hukubali na kuanza mwanzo.

wameambiwa wasitumie zile banners zinahusiana na ikulu wameacha na hawatumii.


ila siku hawa wenzetu wangepata dola nadhani si CUF, si TLP, si CCM na wala vyama vyengine vingepata haki ya lolote ktk nchi hii


hawa ni wahuni tu
 
MO alitaka apite bila kupingwa ili afanye biashara zake pole sana MO mda ukifika ubungwe utakushinda.:glasses-nerdy::becky:
 
wanyaturu bana wananishangaza sana.gabachori anakamua wao bado wapo kwenye usingizi wa pono.:becky::becky::becky::becky:
 
Pengine hiyo ni njia ya NEC kung'ata na kupuliza.wanaenda kinyume wanapuliza kwanza kabla ya kung'ata.
 
This is very true brother, frankly I just dunno why these Guys do whatever in their power just to make sure they don't face competition from others! Their is a say that " If you are alone in the class, every examination you will emerge the first"!

They do whatever is in their power to avoid compeitition because it is costly to compete in Tanzania's elections. By avoiding the competition you avoid having to hand out takrima to voters to buy their votes. So it make perfect business sense to avoid competition.
 
..huyu jamaa amemwaga mapesa kibao huko Singida. Chadema wamuachie jimbo tu.
 
Back
Top Bottom