Elections 2010 CHADEMA wambwaga MO Singida mjini!

AmaniKatoshi

Senior Member
Mar 31, 2009
158
14
Wadau kuna tetesi kuwa CHADEMA wameshinda rufaa dhidi ya MO huko singida mjini, mwenye taarifa tafadhali....
 
MGOMBEA wa CCM katika Jimbo la Singida Mjini, Mohamed Dewji ambaye alitangazwa kuwa mbunge mteule baada ya msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo kukubali pingamizi lake dhidi ya wapinzani wake, amepata mpinzani kutoka Chadema baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kutengua pingamizi hilo.

Kwa mujibu wa barua ya Nec iliyotumwa kwa mgombea wa ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, Isango Hadu, tume hiyo imemrudisha mgombea huyo katika orodha ya wagombea wa ubunge wa jimbo hilo.

Barua hiyo iliyotumwa tangu Septemba mosi mwaka huu kupitia kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo, Yona Maki imeeleza kwamba kikao cha Tume cha Agosti 30 ndicho kilitoa uamuzi huo na kueleza sababu za kurudishwa kwa mgombea huyo wa Chadema.

Katika pingamizi lililowekwa na mgombea huyo wa CCM, ilidaiwa kuwa Hadu hakuwa amependekezwa na Chadema siku alipochukua fomu lakini Nec ilisema ilipata ufafanuzi kutoka Chadema makao makuu kabla ya kufikia uamuzi huo.

Pia Dewji alidai kuwa katika fomu za mgombea huyo wa Chadema, alikuwa na shaka na saini za wadhamini kwa kuwa kisehemu hicho cha majina ya wadhamini, hakikukaguliwa na msimamizi wa uchaguzi.

Hata hivyo Nec imesema sehemu hiyo ya wadhamini ilijazwa kwa ukamilifu na wadhamini walitimia. Pia msimamizi wa uchaguzi hakutoa sababu za kutoipitia na hivyo hakukuwa na tatizo.

Dewji amekuwa mgombea wa pili wa CCM aliyetangazwa kupita bila kupingwa kupata mpinzani baada ya mgombea wa Jimbo la Nyamagana, Lawrence Masha kupata mpinzani kutoka Chadema pia
 
the only way you can rate yourself is when you have serious competition!
 
haya ni maamuzi ya haki, wameamua kwa kufata kanuni, hawa ni weledi kwa hapa kwa mujibu wa CHADEMA

ila wangeamua vyengine basi wamechaguliwa na rais ambaye ni CCM kwa hio hawawezi kuiangusha CCM. nyinyi ni watu wa ajabu
 
mi mi nilifikiri muheshimiwa MO ametolewa kwenye kinyang`anyiro! ..? nilitaka kustuka! kwani singida ingepoteza mpiganaji muhimu sana bungeni
 
usiwe na khofu kijana anashinda tu,

hawa chadema hawana uwezo wowote kazi kelele
 
Mpiganaji kivipi ? sikumbuki lini nilimuona akiongea bungeni.......labda mpiganaji wa Taifa Stars
 
the only way you can rate yourself is when you have serious competition!

This is very true brother, frankly I just dunno why these Guys do whatever in their power just to make sure they don't face competition from others! Their is a say that " If you are alone in the class, every examination you will emerge the first"!
 
haya ni maamuzi ya haki, wameamua kwa kufata kanuni, hawa ni weledi kwa hapa kwa mujibu wa CHADEMA

ila wangeamua vyengine basi wamechaguliwa na rais ambaye ni CCM kwa hio hawawezi kuiangusha CCM. nyinyi ni watu wa ajabu

Si kweli kama unasoma katikati ya mistari na ukiacha ushabiki, maamuzi haya yametolewa kwa kueleza pia sababu kwa nini wametoa maamuzi haya! sio wale wengine wanasema tu maamuzi ni haya, on what ground wameamua hivyo hawasemi, sasa kwa nini watu wasione wameonewa, si unajua ule msemo maarufu wa wanasheria kuwa" Haki sio tu itendeke, bali ionekane pia imetendeka"! Hivi kwa majibu haya ya rufaa ukiacha ushabiki, hupati shaka na maamuzi ya awali?
 
Kweli kabisa nashindwa kuielewa CCM au Wagombea wa CCM wakati wote wanasema wanakubalika anapotokea mpinzani wanaanza kumlima vijembe kama mnakubalika na hamna upinzani yanini kua na woga naamini kabisa kila katika ushindani kunapokua na mshindani au washindani ndipo tuanapopatata mshindi bora.kama hakuna mshindani kunauwezekano mkubwa kupata viongozi wabovu na dhaifu MUNGU IBARIKI TANZANIA
the only way you can rate yourself is when you have serious competition!
 
This is very true brother, frankly I just dunno why these Guys do whatever in their power just to make sure they don't face competition from others! Their is a say that " If you are alone in the class, every examination you will emerge the first"!
hahahahaaa! nimekutwanga thanks kule!!!

Hivi kwanini ccm inatumia nguvu nyingi sana kumnadi handsom wao?
 
Si kweli kama unasoma katikati ya mistari na ukiacha ushabiki, maamuzi haya yametolewa kwa kueleza pia sababu kwa nini wametoa maamuzi haya! sio wale wengine wanasema tu maamuzi ni haya, on what ground wameamua hivyo hawasemi, sasa kwa nini watu wasione wameonewa, si unajua ule msemo maarufu wa wanasheria kuwa" Haki sio tu itendeke, bali ionekane pia imetendeka"! Hivi kwa majibu haya ya rufaa ukiacha ushabiki, hupati shaka na maamuzi ya awali?

ndugu yangu ww una amini kuwa kuna maamuzi katika mambo haya ya uchaguzi hutolewa bila ya sababu? si kweli hata siku moja, sababu mnakuwa hamzipendi na maamuzi mlikuwa nayo mifukoni sasa yakitoka mengine ndo huwa si watenda haki haki haijaonekana kutendeka na mengine mengi

nyny wahuni tu
 
usiwe na khofu kijana anashinda tu,

hawa chadema hawana uwezo wowote kazi kelele

nani ana kelele kati ya chadema na ccm
ushindi wa mezani ndo mnautaka?
Muulize masha anavyohaha baada ya mgombea wa chadema kurudi.
 
MO aendelee na biashara yake ya kulangua mazao ya wakulima kwa bei nafuu wakati wa mavuno ya kuyauza nje ya nchi - huku kwenye siasa ana ajenda gani ya siri? ana uchungu na wana Singida na taifa hili kwa ujumla? mwaka huu kazi anayo.
 
Back
Top Bottom