Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,982
![]()
Tujikumbushe miezi michache iliyopita!
Haaaaa haaaa! Mnatukumbusha mbali wandugu! Mukama na Nnauye nao wametuchanganya sana, mpaka sasa sijaelewa business ya "magamba" ilikuwa inahusu nini hasa!
![]()
Tujikumbushe miezi michache iliyopita!
Yale yale ya Osama kauawa au la? Mbona mwili hauonyeshwi? Haya endeleeniMh. Mbowe angeitisha press baada ya kupeleka ripoti ya mahesabu kwa CAG, ... na yawe yamekaguliwa!
na CCM mabango yote tshirt khanga na kofia helkopta 3 na gharama magari ya kusomba watu hadi ktk mikutano yao wametumia shs ngapi? Coz nahisi hiyo gharama yote ya CDM inalingana na gharama ya mabango tu
Magari ya mitumba yaitikisa CHADEMA
Leon Bahati
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekiri kwamba suala la ununuzi wa magari yaliyotumika lilizua mjadala kwenye kikao chake cha Kamati Kuu kilichomalizika Jumatatu wiki hii.
Maelezo ya mvutano huo yalitolewa jana na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya gazeti hili toleo la Jumatatu kuandika juu ya suala hilo.
Hata hivyo, Dk Slaa alisisitiza kuwa mvutano huo ulikuwa wa kawaida hasa ikizingatiwa kuwa ni suala ambalo haliepukiki penye mjadala wa watu wengi akisisitiza kwamba demokrasia ndiyo iliyoamua.
Gazeti hili liliripoti kuwa mkutano huo ulitokana na baadhi ya wajumbe kupinga na wengine kuunga mkono suala la ununuzi wa magari yaliyotumika yenye thamani ya Sh480 milioni.
Baadhi ya waliokuwa wanapinga mkakati huo walisema kuwa ulikuwa unalenga kumnufaisha Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye alikuwa achukue nafasi hiyo kukiuzia chama magari ambayo tayari ameyatumia.
Miongoni mwa wajumbe wa Baraza hilo, Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo walinukuliwa wakisema kwamba isingekuwa sahihi kwa chama hicho kinachopinga ufisadi kufanya ufisadi kwa kununua magari chakavu wakati wamekuwa wakiibana serikali.
Akitoa ufafanuzi huo jana, Dk Slaa alisema msuguano huo ulikuwa ni wa kawaida na ulikuwa sehemu ya kuwezesha demokrasia kuchukua mkondo wake. Alikiri kuwa kwenye mchakato huo, Mbowe ana magari matatu ambayo chama kinataka kuyanunua.
Alisema hoja hiyo ilimalizika kwa Baraza kuamua kuwa Mbowe aendelee kushawishiwa ili akubali kukiuzia chama magari hayo. Alielezea kuwa magari hayo aliyanunua na yakaanza kutumiwa na chama kwenye kampeni za uchaguzi uliopita.
"Magari hayo Mheshimiwa Mbowe aliyanunua kwa ajili ya biashara zake lakini kwa kuwa chama kilikuwa katika matatizo ya usafiri, akakubali kuyatoa yakisaidie ili baadaye tumrejeshee," alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa magari mawili yanaendelea kutumiwa na chama hivyo ni vyema wayanunue.
Kuhusu chama hicho kununua vitu vilivyotumika wakati kimekuwa kikiipinga vikali serikali kutumia vitu vilivyotumika, Dk Slaa alisema njia inayotumiwa na Chadema iko wazi zaidi ukilinganisha na ile ya serikali.
Alidai kuwa kwenye michakato ya ununuzi serikalini kuna mazingira mengi yanayoruhusu ufisadi hasa katika kujadili bei lakini suala la kununua magari ya Mbowe, suala kama hilo haliwezi kupata nafasi.
Mshahara wa Dk Slaa
Katika hatua nyingine, Mbowe alisema kuwa chama hicho kimeamua kumlipa Dk Slaa mshahara na maslahi yanayolingana na anayopata mbunge.
Alisema hiyo ni kwa sababu chama hicho ndicho kilichokuwa kimemshawishi aache kugombea ubunge katika Jimbo la Karatu, Arusha ambako alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda na kumtaka agombee urais ambao mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete alitangazwa kuwa mshindi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbowe alisema uamuzi huo ulifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na vikao vikuu vya chama hicho, kama vile Kamati Kuu na kisha kuidhinisha malipo hayo.
"Itakumbukwa kuwa Mheshimiwa Dk Slaa hakuomba nafasi ya kugombea uraisi, aliombwa. Tunajua alikuwa mbunge na alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda tena nafasi hiyo, lakini akakubali ombi la chama," alisema Mbowe na kuongeza: "Hii siyo mchezo!
Uamuzi wa namna hiyo ni wa kujitoa. Ndiyo maana Kamati Kuu ikakubali apate mshahara na marupurupu sawa na yale ya mbunge."
Mbunge anakadiriwa kuwa anapata mshahara pamoja na marupurupu yanayokaribia kufikia Sh7 milioni kwa mwezi.
Chadema kilitumia Sh1.3 bilioni kusaka urais 2010
Akizungumzia Uchaguzi Mkuu uliopita, Mbowe aliwaambia waandishi wa habari kuwa chama chake kilitumia Sh1.3 bilioni katika kampeni za uras.
Alivitaja vyanzo vya fedha hizo kuwa ni Sh 338.9 milioni za ruzuku, Sh 235.9 milioni kutoka kwa marafiki, Sh32 milioni michango mbalimbali ya wanachama na mali mbalimbali za watu zenye thamani ya Sh719.7 milioni.
mbowe ni fisadi na huu ushahidi tosha. hii ngo yao inamtajirisha.
slaa anapata milioni 15 kwa mwezi wasitudanganye. kalegezwa na mbowe ili asipige kelele ufisadi wa mbowe.
mbowe ni fisadi na huu ushahidi tosha. hii ngo yao inamtajirisha.
slaa anapata milioni 15 kwa mwezi wasitudanganye. kalegezwa na mbowe ili asipige kelele ufisadi wa mbowe.
mbowe ni fisadi na huu ushahidi tosha. hii ngo yao inamtajirisha.
slaa anapata milioni 15 kwa mwezi wasitudanganye. kalegezwa na mbowe ili asipige kelele ufisadi wa mbowe.
katibu mkuu wako makama anapata billion ngapi?
Umeuliza swali nzuri.
je, wakati mbowe anatoa hayo magari yalikuwa mitumba? Mbona husemi Chadema imeongeza kura ngapi kutokana na magari mapya ya mbowe wakati huo. Ila leo tumeshapata kura na ruzuku malipo yamekuwa nongwa. Huu nao ni upuuzi.
Ikiwa CHADEMA walitumia magari ya Mheshimiwa Mbowe sioni sababu za msingi kwanini magari hayo yasinunuliwe na chama nadhani sasa napata mwanga kwanini Zitto na Mbowe hawatapikika chungu kimoja kuna kila dalili za kukomoana baina ya kambi ya Zitto na Mbowe bahati mbaya Mbowe badala ya kuunda mtandao wa viongozi wenye akili anamkibilia Lema lohooo salalee.
Mwanzo nilidhani CHADEMA walitaka kununua magari chakavu kumbe ni magari waliyotumia na kuwapatia mtaji mkubwa wa wabunge na madiwani kibao achilia mbali kura kibao za urais!.Niko tayari kusahihishwa ugomvi mkubwa baiana ya Mbowe na Marehemu Chacha Wangwe ni matumizi ya fedha za chama,wangwe akitaka fedha zisambazwe majimboni.
Unajichosha bure jali familia yako kwanza achana na ya Mbowe na Slaa.aibu mitumba ya dowans lakini mitumba ya mbowe ni gari mpya
fisadi mbowe kamlambisha slaa milioni 15 ili akae kimya yeye akichota mapesa kwa kutumia mitumba
Njie watu wa ajabu kweli mbona hamhoji kwa nini magari yake yalitumika bure wakati wa kampeni.