Sidhani Lowasa kama ni mchafu sana kiasi hicho kama tunavyotaka kuaminishwa, kwangu mimi kosa kubwa la Lowasa ambalo namhukumu nalo, ni kwakuwa alishiriki kwa kiasi kikubwa katika mipango ya kumweka Kikwete madarakani na huku akichafua wengine kupitia mtandao wao walioubuni enzi hizo, na Sitta akiwemo. Kuhusu suala la Richmond, jamani ifike mahali sasa na EL naye aseme hadharani Richmond alihusika vipi. M/kiti wa kikao cha baraza la Mawaziri ni Rais, sasa kuendelea kukaa kimya kwa EL ndiyo ataendelea kujichimbia kaburi. Ok ametubu kama Mwigamba alivyosema na viongozi wakapima akaja CDM na akawa mwanachama wa kawaida, je akataliwe? na wote mnaomhukumu kiasi hicho kila mtu ajitazame ni msafi kiasi gani. Kwetu sisi wakristo Biblia inatuambia kuwa hata yule mwana mpotevu baada ya kutapanya mali za baba yake, akagundua kosa, akajuta, akarudi kwa baba yake, je baba yake si alimpokea?