Kwanza kabisa naomba niwarejeshe kwenye kaulimbiu ya JF, inasema, "The Home of Great Thinkers". Ukweli niliougundua ni kwamba tuna wana JF wengi sana humu ambao si great thinkers. Naomba nizungumzie mambo mawili tu:
Kwanza tunachofanya humu ndani ni kisa tulichosimuliwa zamani kwamba baba mmoja alikutwa na mkewe akinoa panga. Mke akamuuliza unanoa panga la nini, yeye akajibu hivi: "Ninanoa hili panga ili nikafyeke shamba halafu nilime pamba nikivuna na kuiuza nitanunua ng'ombe wawili: mweusi na mweupe. Yule mweusi hata wewe unaweza kumkamua lakini mweupe nitakuwa namkamua mimi tu". Mke akasema haiwezekani mweuupe umkamue peke yako. Hata mimi nitakuwa namkamua. Mme akasema haiwezekani umkamue ng'ombe wangu. Wakabishana mpaka wakapigana. Ndicho ninachokiona humu ndani. Watu wanatoa macho kiasi kwamba baadhi wangekuwa karibu yule aliyemtukana eti Tuntemeke Mwigamba aondoke atuachie chama, labda angeweza hata kumpiga. Tunatoleana macho utadhani Lowassa katangaza kuingia CDM na sasa tunabishana ama tumpokee ama tuache. Kumbe inawezekana jamaa hana hata mpango huo!
Jambo la pili naomba tusome tena hii nukuu hapa kama Mwandishi wa gazeti alivyomnukuu Mwigamba:
"Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama,"
Kama mmesoma hayo maneno ya Mwigamba between lines, hamna sababu ya kumshambulia kiasi hicho. Hajasema kwamba leo hii inaweza kutokea tu EL akaja akaomba kuingia CDM na yeye kama mwenyekiti wa mkoa akampokea. Amesema lazima aeleze sababu za kufanya hivyo na akatumia neno la wingi "na sisi" ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama. Maneno yake yanaonyesha collective responsibility kwamba watakuwa jopo la viongozi. Watamuuliza kwamba unataka kuja CHADEMA lakini una tuhuma hizi na hizi. Wakiridhika na maelezo yake ndo wataamua kama viongozi si yeye kama mwenyekiti wa mkoa. Naomba niwaulize swali mnaotumia msuli mkubwa kupinga EL kuja CDM kwa vyovyote vile. Hivi akija na uthibitisho kwamba madudu yote yamefanywa na Mkapa na Kikwete. Yeye kafanywa mbuzi wa kafara kwa ajili ya kuiokoa serikali isidondoke kama alivyofanyiwa gavana wa zamani wa benki kuu Daudi Ballali, hivi akaja na ushahidi wa kile alichokitamka Mwakyembe kwamba kuna vitu walificha ili serikali isidondoke na vitu hivyo kumbe EL akafanikiwa kuonyesha kwamba ni ushahidi kwamba ufisadi wote wa Richmond ni wa JK na si wa kwake Lowassa. Hivi akija akakiri na kutubu kwa kuonyesha ushahidi wa baadhi ya vitu alivyovifanya kwa kulazimishwa na system kwa ajili ya chama na akavijutia na kuviungama na kuwaomba radhi wananchi, akasema ametoa maisha yake kama serikali itamuua kama ilivyommaliza Ballali yuko tayari ili mradi ukweli wote uwe hadharani, hivi mtakataa kumpokea awe mwanachama wa CHADEMA. Try to use your bongos badala ya kutumia misuli kupinga kila kitu kwa ushabiki.