CHADEMA wako tayari kumpokea Lowassa

Sio kutubu tu bali pia atatakiwa kurudisha vyote alivyojipatia kwa njia ya haramu ndipo sasa tufikirie kumpatia uanachama.

Hata hivyo sisfikirii na sitegemei hata kidogo kumuona Lowasa akijiondoa ccm. Hawezi ku survive nje ya ccm na yeye hilo analitambua sana, hawezi kufanya kosa la ku cross borders.
Kwa sasa huonekani JF....na kwa sasa ndiye mmiliki wa chadema ambayo wewe ni mwanachama...kwa sasa full aibu...performance ya chadema hadi bungeni imeshuka...kalagabaho!
 
STIDE,

..Lowassa akabidhiwe kadi ya CDM baada ya kufanya yafuatayo:

1.azunguke nchi nzima na ripoti ya Tume ya Mangula, ile ambayo ilielekeza JK afukuzwe CCM.

2.azunguke nchi nzima na kuwaeleza wananchi na kuwaomba radhi kutokana na fitina na majungu yaliyowezesha wana mtandao kuingia madarakani mwaka 2005.

3.aeleze kile ambacho Dr.Mwakyembe alikificha katika ripoti ya Richmond ili kutokuiabisha serikali. aeleze nani alikuwa akimpa maelekezo na baraka za kukiuka maamuzi ya vikao na kulazimisha Richmond kupewa mkataba.

4.aeleze wahusika wa Dowans ni kina nani.

5.akubali kustaafu rasmi siasa akiwa ametubu madhambi yake kwa wa-Tanzania.
Brother upo... Msalimie Mwita Maranya
 
Brother upo... Msalimie Mwita Maranya

..nipo mkuu.

..naugulia machungu ya kubadili gia angani.

..lakini vilevile sina uhakika kama kwa kampeni zile za ccm tungeweza kuwashinda au kufanya vizuri zaidi ya hivi tulivyofanya.

..nyuma ya pazia tulishauri mambo mengi, ambayo tulidhani yangesaidia, lakini hayakufanyiwa kazi.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Arusha, Samson Mwigamba, amesema kuwa yeye yuko tayari kumpokea hata Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, endapo ataamua kufanya uamuzi wa kubadilika na kujiunga na CHADEMA.

“Lowassa akiamua kuondoka CCM ni lazima atakuwa na sababu za kufanya hivyo, lakini na sisi ni lazima atatueleza juu ya tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazoelekezwa kwake, tutamsikiliza, tukimwelewa hatutakuwa na sababu ya kumnyima uanachama,” alisema.

Source: Tanzania Daima

My take: Nimeanza kuamini kuwa inawezekana kabisa Lowassa anaandaliwa mazingira ya kusafishwa.
Du! . Kuna watu waliona mbali! .
Pasco
 
...Sidhani kama CHADEMA watakuwa tayari kufanya makosa makubwa kiasi hicho ya kumpokea fisadi EL. CCM ndio inakufa taratibu wengi wao wanatafuta pakutokea kabla magamba hakijazikwa rasmi.

Hakuna ubaya kuwapokea watakaotoka magamba lakini mafisadi wote ndani ya magamba na wala/watoa rushwa kamwe wasiruhusiwe ndani ya CHADEMA.
Hahahaha BAK nakukumbusha tu enzi hizooooooo, yaani mlivyomisukule hata hamjitambui kabisa.
 
Back
Top Bottom