CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

Ukitoa vifaa vya kijeshi hizo manati na visu chadema mnawinda ndege siku hizi?

Hayawahusu, tuwinde au yawe mapambo. Hata wamasai wanaolinda getini wana marungu,visu na majambia sembuse redbriguard wanaolinda mamia ya raiya na viongoz wa chama. Nasema hivi wanatakiwa wawe na SMG ndio watafanya kaz yao barabara.
 
Hayawahusu, tuwinde au yawe mapambo. Hata wamasai wanaolinda getini wana marungu,visu na majambia sembuse redbriguard wanaolinda mamia ya raiya na viongoz wa chama. Nasema hivi wanatakiwa wawe na SMG ndio watafanya kaz yao barabara.

Chadema ni janga la taifa hakifai hasa kwa sisi wapenda amani
 
wakuu naomba mwenye nako kale ka picha ka mguu wa kuku ka kada maarufu wa ccm alikopandanako jukwaan huko tabora wakati wa kampeni za 2010 atuwekee humu jukwaan ili watanzania waone na walinganishe nani anamilki silaha za kijeshi
 
Wana Ukumbi,

Baada ya mkuu wa jeshi la polisi nchini kuvipiga marufuku vyama vyote vya siasa kuhusu kuwa na makundi ya kujihami katika vyama hivyo, CHADEMA wamekaidi agizo hilo halali la polisi na wameendelea kuwatumia Red Brigedi katika chama chao!

Jambo ambalo CHADEMA hawakutarajia ni kuwa, polisi wana vyanzo vyingi vya taarifa, hivyo mmoja wa makamanda wa CHADEMA alifikisha taarifa kwa jeshi la polisi juu ya uwepo wa vifaa vya kivita ndani ya ofisi ya makao makuu na pia kuna mpango wa kusambaza vifaa hivyo kote nchini.

Zifuatazo ndio picha za vifaa hivyo na jinsi CHADEMA ilivyojipanga kuandaa waasi ikitokea imeshindwa uchaguzi mkuu! Yale yanayotokea Kongo yataletwa Tanzania kama serikali haitachukua hatua juu ya jambo hili.

attachment.php


Baada ya vijana wa CHADEMA kuwekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi wakiwa na vifaa hivyo vya kijeshi.

attachment.php


1.jpg


Vifaa hivyo vikiwa vimekusanywa kwa pamoja na jeshi la polisi ambapo awali vilikuwa vimefichwa maeneo mbalimbali ndani ya ofisi ya CHADEMA na vingine vikiwa tayari kwa kusafirishwa kwenda mikoani.

attachment.php


Hapa pia tunaweza kujionea wenyewe jinsi CHADEMA walivyojipanga kuivuruga amani yetu kwani hakuna chama cha siasa kinachoweza kuwa na zana hatari za aina hii ofisini!

KWA WALE MNAODHARAU VISU KUTUMIKA KAMA SILAHA ZA KIJESHI, HEMU TAZAMENI HIVI VISU AMBAVYO NI MAALUMU KATIKA JESHI LA MARAKENI NA UTUMIKA PIA VITANI.



attachment.php



Pia itakumbukwa ni hivi karibuni tu kuna magaidi walikamatwa Morogoro wakiwa na vifaa vifuatavyo: silaha za sub machine guns, milipuko ya kulipulia majengo majambia, manati, bendera nyeusi, sare za jeshi nk. Hivyo kuna uwezekano mkubwa magaidi hao wakawa na uhusiano na vijana hawa wa CHADEMA. Hivyo jeshi la polisi halina budi kufanya upelelezi wa kina ili kuzuia vitendo vya kigaidi nchini.

Kuna tofauti ya vifaa vya jeshi na vile vinavyofanana na vya jeshi ndugu! tukianza na hivyo visu vimejaa majumbani mwa watu na hata madukani ukipita huku na kule,kunako elekea mtawazuia hadi wamasai wasitembee na sime viunoni na pengine mtatuzuia tusiwe na visu majumbani mwetu! hayo mabuti nenda soko lolote la mitumba utayakuta kedekede ni maamuzi ya mtu kuvaa kiatu anachotaka, hizo manati zimejaa kibao mijini na vijijini nakushangaa hata manati unasema ni kifaa cha jeshi! hizo geta ni zakuendeshea pikipiki au wakati unafanya mazoezi kujikinga na magoti au engo za mikono! wewe mwenyewe hao polisi wakiamua kukuvamia na kukukagua basi utawekwa chini ya ulinzi maana utakutwa na vifaa vingi mmno vya jeshi kwa mantiki yako ya kubatiza kila nyenzo kwajina la VIFAA VYA JESHI!
 
Hizo ni mbinu chafu za kuichafua chadema,mwaka huu tutasikia mengi mfamaji haachi kutapatapa.
 
Polisi wanadharirisha nchi. Yaani majeshi yetu yanatumia visu vya vitunguu na manati?
 
Hizo ni propaganda za ccm hata aibu awaoni kabisa watanzania saizi tunajua mbivu na mbichi siyo zamani mlikuwa mnatuendesha Kwa sababu mlikuwa mnamiliki TV wenyewe
 
Mkuu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!, kati ya vifaa vyote hivyo ulivyoonyesha, kuna kitu gani hapo cha kijeshi?!. Kama ni hivyo, mbona hata mimi hivyo vyote ninavyo na zaidi ya hivyo?!.
Mimi nilidhani wamekutwa na AK 47, Machine guns, hand grenades, night vision binoculars, cynide capsules, masanduku ya TNT etc, lakini wamekutwa na hizo botts na shield za waendesha boda boda ndio vifaa vya kijeshi?!.

Hili jeshi letu la polisi sasa linakuwa too sensational!.

Na kama kuna kitu kitamkosesha Kova u IGP ni sensationalism!.

Pasco
umeongea ukweli kabisa jeshi la polisi linazidi kujithalilisha kabisa hivi kweli ccm mmefikia hatua hii.
cc Pasco
 
Last edited by a moderator:
hii issue imepangwa kijinga sana na watu wasio na akili timamu...Ahmed msangi anajulikana kuwa na mahaba na CCM na ni mmoja wapo wa waliomteka ULUMBOKA na kibanda....hapo hakuna kesi kwa tunaojua sheria vizuri...

Tanzania ndiyo nchi ya pekee inayoendeleza siasa za kijinga jinga dhidi ya vyama vya upinzani.


nyambafu CCM na mawakala wao....mwaka huu hata iweje lazima mtoke IKULU....
 
Ile habari sijui imeripotiwa vipi, maana nimeshindwa kutofautisha habari ya mkono wa Albano na hizo zinazoitwa silaha za kijeshi.

Uhuni wa genchi la pliz...... Hata mimi niliona na nilikasirishwa sana na huyo reporter!
 
Acha uongo hizo ni habari mbili tofauti ila zimeripotiwa kijanja kijanja kuwadanganya watu kama nyie.

Ok hebu tuambie basi ukweli maana mnapenda kusikia tu yale mnayopenda kuyaskia na inaonyesha unajua mengi sana kuliko huyo ripota
 
Back
Top Bottom