CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi Ofisini!

Hizi silaha zipo kila nyumba nenda kariakoo visu kibao vimepangwa mashoka kibao
 
Ukienda taasisi yoyote utakuta walinzi mchana hawana silaha usiku wana silaha ikiwemo visu tena vikubwa tu yani sime manati ,rungu, nondo nk. Hata majumbani mwetu ukija uvunguni kwangu utakutana na panga kali sana na rungu na ukivamia lazima ukutane na hizo silaha zikiwa active. Nenda hata shule za msingi za serekali utakuta walinzi wakiwa na silaha kama hizo .This is 2015 mambo ya 1995 hayawezi kupata nafasi tumeshatoka gizani tupo kwenye mwanga

Kwa sasa jambo la msingi kwa Chadema ni kuchukua hatua za kisheria dhidi ya MTU
/watu walioandaa ujinga huu ili kukomesha upuuzi huu. Chama kikiacha mambo haya yaendelee, iko siku jambo hilo litaeleta shida.
 
Kwa sasa jambo la msingi kwa Chadema ni kuchukua hatua za kisheria dhidi ya MTU
/watu walioandaa ujinga huu ili kukomesha upuuzi huu. Chama kikiacha mambo haya yaendelee, iko siku jambo hilo litaeleta shida.

mpaka barua zenye sahihi za viongozi wa chama zimeandaliwa?duuuuh kweli chadema wasafi
 
.Kisu ni zana ya kijeshiiii?????

Ama kweli hata mimi nina miliki zana za kijeshi pia
 
mpaka barua zenye sahihi za viongozi wa chama zimeandaliwa?duuuuh kweli chadema wasafi

Hakuna jambo baya Ktk maisha kama umaskini. Umaskini wa akili ni nyundo ya maisha kwa mhusika wa um as kin I huo
 
Jinga sana wewe....Li Bunge lizima hovyo...hata hujui maana ya ugaidi!! ukiulizwa kuwa..thibitisha kuwa hao ni wanachama wa chadema ...utathibitisha?

kwanza huna hadhi yoyote nyambafu...

hivi kwanini watu wachadema mkiona watu ambao hawakubaliani na nyie mnawashambulia kwa matusi?sikilizeni kama ilivyo cuf ccm NCCR vina wanachama na kuna watu hawavipendi kwahiyo hamuwezi kutulazimisha kuipenda chadema kwasababu ni kikundi cha uasi kila siku mbowe anatutishia ila ngojeni tu
 
vimetajwa vingi cha maana hapo ni kama hizo sare ni za jeshi gani, bendera,makoti, mawe,spring.kamba,sheguard,miwani,nuts havina la msingi sana kiujumla ni magnification kukuza jambo tu, wangalivaa kama crazy gk ama diamond si ingekua balaa, hao ni walinzi wa ofisi, manati sio issue zimejaa kariakoo ukitaka toa ela tu
 
Walianza na Chama cha Wachaga, Chama cha Kigaidi, Chama cha Kidini, wabaguzi nakazalika sasa wana jeshi na zana Kijeshi!!! Maajabu!

Kwa hali hiyo basi kila raia wa Tanganyika ni Askari na kila nyumba ina Vifaa vya Kijeshi.

Kumbe miaka ile nikiwa namiliki manati yangu na kokoto zake nilikuwa Askari na Mtu hatari sana? Nimejaribu kupitia taarifa huyo HAIONYESHI au HAISEMI au KUTAJA OFISI HUSIKA ni Ofisi zipi hizo? Vijana wenyewe hawafanani na waliopewa mafunzo.

Lakuunda nila kuunda tu!!!! Mzoea vya Kunyonga kamwe vya kuchinja Shughuli!!!! Ha haa!!!!
Tafuteni lingine kwa Wa Tanganyika na Wa Zanzibari wa Leo, Hiyo ni Ajua!!!!!
 
Hapa ni Sawa kabisa. Aa! Namaanisha wao Green Guard ni sawa na Mungu anataka.
 
Policcm ndio zao na bado watasingizia sana , badi kuleta mabomu na siraha na kusema chadema teh teh watafute swaga nyingine
 
Pia wamekamatwa na kiganja cha Albino!

No mkuu hujaelewa kulikuwepo watu watatu waliokamatwa na kiganja na wawili ndio police wanasema ni wafuasi Wa chdma ila wote wamekamatiwa Mbozi na makundi haya mawili hayanamahusiano
 
Masai wanaotumia sime nao wanataka kuharibu amani ya nchi?
 
Upuuzi huu mbona manati zinauzwa had I kwenye masoko uyasemaje silaha za kivita we mtoa maada vipi au umevulugwa
 
Kwa sasa jambo la msingi kwa Chadema ni kuchukua hatua za kisheria dhidi ya MTU
/watu walioandaa ujinga huu ili kukomesha upuuzi huu. Chama kikiacha mambo haya yaendelee, iko siku jambo hilo litaeleta shida.

Ni kweki kabisa ndugu, ofisi yenye watu wawili tu na haitwaji ni ipi na viongozi ya hiyo ofisi hawatajwi. Mbaya zaidi taarifa ya habari ya saa 2 itv wamwonyesha hizo silaha na katika hali ya kushangaza wakachanganya na habari mkono wa albino ili kuichafua cdm kipuuzi. Ungeona hiyo habari ungeshangaa aina gani utoaji wa habari yaani ni kama ni habari zilizotoka kwa tatizo la kiufundi, kwanza wameanza na hizo picha za cdm, kisha habari ya albino na kabla haijaisha wajarudishia picha za hai vijana wa cdm alafu hapohapo wakaweka picha ya mkono wa albino. Kwa mazingira haya polisi wanataraji cdm wawaamini? Cdm wachukue hatua mapema na msemaji wa chama atolee tamko mapema huu upotoshaji.
 
Hivyo visu ni vingi tu mitaani. Mimi nilinunua viwili pale Morogoro Msamvu kwaajili ya kumenyea miwa. Hizo buti gani!! Hizo buti ni tepetepe kuliko buti ninazovaa mimi kwa shughuli zangu za field. Hizo kofia waseme ni za jeshi gani? Maana kofia kama hizo siku hizi zipo kibao hata kwenye mitumba.

Polisi watapoteza heshima wakiendekeza ujinga wa namna hiyo. Hata manati wanazotumia watoto wa vijijini, siku hizi nazo ni silaha? Basi siku hizi kila kitu ni silaha. Nilidhani labda wamewakamata na Machine gun, AK47, SMG, RPG. Hapo kweli ningeshtuka. Yaani visu vya mboga siku hizi ni silaha?
 
Back
Top Bottom