Mkuu Mathias Raymond Nyakapala, kwanza asante kwa taarifa hii, pili, kwa ruhusa yako, naomba niitumie sehemu ya bandiko hili kama mbegu kupandishia bandiko langu fulani.
Japo siungi mkono kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe na Mbunge Esta Matiko kufutiwa dhamana, kwa sababu lengo la mtu kushikiliwa mahabusu no ili asitoroke kujibu mashitaka yanayomkabili, the common sense logical inaelekeza mtu kuwa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, hiyo pekee tuu ni dhamana tosha, na Mbowe sio Mwenyekiti tuu wa Chadema bali pia ni Mbunge wa Bunge la JMT, hii pia ni dhamana tosha, sasa kwa kesi hii ambayo haina kichwa wala miguu, Mwenyekiti wa chama na Mbunge akimbie wapi, akimbie nini?!
Ipo haja ya kufanya mapitio ya sheria zetu kuhusu haki ya dhamana na sifa za mtu kujidhamini mwenyewe na masherti ya dhamana.
P