CHADEMA waita wanachama nchi nzima tarehe 6 Desemba, 2018

Mathias Raymond Nyakapala

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
2,181
Reaction score
1,494
#BREAKING_NEWS

Chadema yaita Wanachama wake wote Nchi nzima kufika Kisutu Dar Es Salaam Desemba 6, 2018.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimewataka wanachama wake wote Nchi nzima kufika Mahakamani wakati kesi inayowakabili Viongozi wake watano itakapounguruma ili wajionee uendeshwaji wa kesi na kuamua kwa pamoja nini cha kufanya.

Wito huo wa CHADEMA umekuja Saa chache baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu kuamua kufuta dhamana ya Viongozi wawili wa Chama hicho, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Ester Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Akizungumza na wanahabari, Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni Jijini Dar ES Salaam, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Vicent Mashinji amesema, "Wanachama wa CHADEMA nchi nzima, suala hili ni zito, ni nyeti na linahusu mustakabali wa nchi yetu, usisubiri kusimuliwa njoo uone mwenyewe kinachoendelea Mahakamani kwa sababu kumekuwa na upotoshaji mkubwa".

"Tunaomba tuje tusikilize wenyewe Mahakamani na baada ya hapo tuamue ni hatua gani tutachukua sisi kama Watetea haki wa Watu wote katika Taifa hili," ameongeza.

Aidha katika hatua nyingine, Chama hicho kimeazimia kukata Rufaa katika Mahakama Kuu kwa kile ilichokidai kuwa; ni kupinga juu ya hatua ya kufuta Dhamana ya Viongozi wake iliyofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

"Tumeamua kukata Rufaa kwenda Mahakama Kuu na tumeshawasilisha Barua yetu, bado tunasubiria watupe namna. Na katika Barua yetu tumeeleza haya mashaka yetu yote juu ya mwenendo wa hii kesi".

Chanzo; East Africa Television (EATV)
 
Naona hii habari kila mwamaufipa anaileta! Mbona ilishaletwa ikabuma??!!
 
Acheni ujinga Ufipa, suala ni Mbowe hakufuata sheria, nakwambia hiyo mnayosema ya kukutana Kisutu CHADEMA wote, je ni kwamba mna wanachama wachache hivo?

Au ni kwamba eneo la mahakama limepanuliwa ili muenee?

Au unadhani atakayethubutu kusema anaorganize watu kufika atajuta sana anaweza kuswekwa ndani kwa kosa la kuitisha mkusanyiko
 
Tujaribu kujitambua na kuzidai haki zetu.tatizo là watanzania ni waoga kuthubutu.
Haki gani ya kumtetea Mbowe aliyedanganya Mahakama kuwa yuko mahututi SA mara akaibukia Ubelgiji anapiga self na mgonjwa Lissu huku wakikenua meno kama mazuzu?!! Mahakama siyo ya kuchezea pia naamini watz hawawezi kuchezewa kiasi hicho eti waje Kisutu kwa gharama ya nani na wakikamatwa na kuwekwa lupango utawatetea wakati wapo waliondamana kwenye uchaguzi mdogo Kinondoni wanasota na kesi hata ruzuku hawapati ili ziwasaidie bali group la Mbowe ndiyo linapiga ruzuku pekee yao. Hata Kubenea anajua hivyo!
 
1.Mbowe alivunja sheria ipi Mkuu...mtu akishitakiwa Mahakaman akiwa na dharura anatakiwa mdhamini kwenda na kusema dharura ya Mshitakiwa.

2.Kuswekwa ndani wanaswekwa wenye hatia na wasio na hatia hata wewe hapo usijione upo salama,hujui kesho itakuwaje maana tunaona wanaCcm na wasio na Vyama nao ni wahanga kama Chadema tu.

3.Wanachadema wote Nchi nzima hawawezi kuja mahakaman ila sikio litakuwa huko na maombi juu
Acheni ujinha Ufipa, suala ni Mbowe hakufuata sheria, nakwambia hiyo mnayosema ya kukutana Kisutu CHADEMA wote, je ni kwamba mna wanachama wachache hivo?

Au ni kwamba eneo la mahakama limepanuliwa ili muenee?

Au unadhani atakayethubutu kusema anaorganize watu kufika atajuta sana anaweza kuswekwa ndani kwa kosa la kuitisha mkusanyiko
 
Baada ya mwenyekiti kuwekwa ndani hichi ndicho kilichotokea pigo kwa ccm
FB_IMG_1543091908219.jpeg
 
Yangu macho
Acheni ujinga Ufipa, suala ni Mbowe hakufuata sheria, nakwambia hiyo mnayosema ya kukutana Kisutu CHADEMA wote, je ni kwamba mna wanachama wachache hivo?

Au ni kwamba eneo la mahakama limepanuliwa ili muenee?

Au unadhani atakayethubutu kusema anaorganize watu kufika atajuta sana anaweza kuswekwa ndani kwa kosa la kuitisha mkusanyiko
 
Mpumbavu ni yule anayelialia kila siku anataka amani badala ya kulilia haki
HAKI KUPUUZIA MAHAKAMA.
KAma haki inapatikana Mahakani.kwanini udharau MAHAKAMA halafu uje kuita watu waje kujazana kwenye mkusanyiko wa kipuuzi....?
Hao watu wakikusanyana watabadili maamuzi ya mahakama?
 
Back
Top Bottom