CHADEMA waita wanachama nchi nzima tarehe 6 Desemba, 2018

CHADEMA waita wanachama nchi nzima tarehe 6 Desemba, 2018

Kwa hiyo Mashinji anataka kusema Mbowe alikuwa mahututi ndio maana hakufika mahakamani? Ile picha ya Ubeligiji ndio alikuwa Mahututi?
Kwani akiwa mahututi ubelgiji akipata nafuu arudi hapohapo bila kusubiria au picha ilikua inatoa sauti
 
#BREAKING_NEWS

Chadema yaita Wanachama wake wote Nchi nzima kufika Kisutu Dar Es Salaam Desemba 6, 2018.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimewataka wanachama wake wote Nchi nzima kufika Mahakamani wakati kesi inayowakabili Viongozi wake watano itakapounguruma ili wajionee uendeshwaji wa kesi na kuamua kwa pamoja nini cha kufanya.

Wito huo wa CHADEMA umekuja Saa chache baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu kuamua kufuta dhamana ya Viongozi wawili wa Chama hicho, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Ester Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Akizungumza na wanahabari, Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni Jijini Dar ES Salaam, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Vicent Mashinji amesema, "Wanachama wa CHADEMA nchi nzima, suala hili ni zito, ni nyeti na linahusu mustakabali wa nchi yetu, usisubiri kusimuliwa njoo uone mwenyewe kinachoendelea Mahakamani kwa sababu kumekuwa na upotoshaji mkubwa".

"Tunaomba tuje tusikilize wenyewe Mahakamani na baada ya hapo tuamue ni hatua gani tutachukua sisi kama Watetea haki wa Watu wote katika Taifa hili," ameongeza.

Aidha katika hatua nyingine, Chama hicho kimeazimia kukata Rufaa katika Mahakama Kuu kwa kile ilichokidai kuwa; ni kupinga juu ya hatua ya kufuta Dhamana ya Viongozi wake iliyofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

"Tumeamua kukata Rufaa kwenda Mahakama Kuu na tumeshawasilisha Barua yetu, bado tunasubiria watupe namna. Na katika Barua yetu tumeeleza haya mashaka yetu yote juu ya mwenendo wa hii kesi".

Chanzo; East Africa Television (EATV)
Mkuu Mathias Raymond Nyakapala, kwanza asante kwa taarifa hii, pili, kwa ruhusa yako, naomba niitumie sehemu ya bandiko hili kama mbegu kupandishia bandiko langu fulani.

Japo siungi mkono kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe na Mbunge Esta Matiko kufutiwa dhamana, kwa sababu lengo la mtu kushikiliwa mahabusu no ili asitoroke kujibu mashitaka yanayomkabili, the common sense logical inaelekeza mtu kuwa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, hiyo pekee tuu ni dhamana tosha, na Mbowe sio Mwenyekiti tuu wa Chadema bali pia ni Mbunge wa Bunge la JMT, hii pia ni dhamana tosha, sasa kwa kesi hii ambayo haina kichwa wala miguu, Mwenyekiti wa chama na Mbunge akimbie wapi, akimbie nini?!

Ipo haja ya kufanya mapitio ya sheria zetu kuhusu haki ya dhamana na sifa za mtu kujidhamini mwenyewe na masherti ya dhamana.

P
 
Nondo ameshinda kwa maelekezo ya nani? Muache uzwazwa!!! Kakiuka masharti ya dhamana ni kawaida kukumbushwa hilo.
Only in Tz , especially awamu ya 5. Unataka amani, huwezi kuwasumbua wapinzani wako kwa kesi za kishenzi namna hii. Mwanzo wa hii kesi unaujua , na sababu zake unazijua . Yuko wapi mkurugenzi wa kinondoni kama unataka kutenda haki ?! Akili za waTz za hovyo sana.
 
Kwani matiku na mbowe kufutiwa dhamana wameonewa? Je walifuata masharti ya dhamana au waliyavunja makusudi
 
Chadema wamechanganyikiwa
Niache shughuli zangu mbeya nije dar kusikiliza wapuuzi waliovunja sheria makusudi?
Hata kama ningeishi Tandale kwa mkunduge siwezi kuhribu nauli yangu
 
Only in Tz , especially awamu ya 5. Unataka amani, huwezi kuwasumbua wapinzani wako kwa kesi za kishenzi namna hii. Mwanzo wa hii kesi unaujua , na sababu zake unazijua . Yuko wapi mkurugenzi wa kinondoni kama unataka kutenda haki ?! Akili za waTz za hovyo sana.
Ni mtazamo wako
 
Nani aache shughuli zake aje kusikiliza kesi ya mtu aliyedharau mahakama na kwenda kula bata na Joyce Mkuya ulaya?

Naona hamkujifunza ya Mange Kimambi.
 
Kwani matiku na mbowe kufutiwa dhamana wameonewa? Je walifuata masharti ya dhamana au waliyavunja makusudi
Kama bunge limeitaarifu court, kwamba mbunge ni sehemu kamati na amewakilisha taifa, bado hakimu haridhiki mpaka atimize kiu yake, utasemaje dhana yangu ?!

Furahini wakoloni weusi
 
Katibu mkuu wa chadema alikuwa dr slaa tu, huyu mashinji ni porojo tu kama viongozi wengine wa chadema.
Wanachama wake kisutu kwa gharama za nani?
Wakikamatwa na kuswekwa ndani nani atawatetea?
Ni chama gani cha kipuuzi hicho kinachofanya maamuzi ya wanachama wote bila kufuata taratibu za vikao vya kikatiba vya chama?
Chadema imegeuka kuwa kama genge tu walevi wasiojua wanasimamia nini, na nini wafanye kwa wakati gani. Poor chama chetu kikuu cha upinzani.
 
Kama bunge limeitaarifu court, kwamba mbunge ni sehemu kamati na amewakilisha taifa, bado hakimu haridhiki mpaka atimize kiu yake, utasemaje dhana yangu ?!

Furahini wakoloni weusi
Sababu waliotoa ni kwamba ni mgonjwa yupo South Africa.. Mara tunamuona mitandaoni yupo kwa lisu Ubelgiji
 
Weeeee nije nifyekwe tu miguu twangu alafu nipambane na hali yangu[emoji16][emoji16][emoji16], never.
 
Acheni ujinga Ufipa, suala ni Mbowe hakufuata sheria, nakwambia hiyo mnayosema ya kukutana Kisutu CHADEMA wote, je ni kwamba mna wanachama wachache hivo?

Au ni kwamba eneo la mahakama limepanuliwa ili muenee?

Au unadhani atakayethubutu kusema anaorganize watu kufika atajuta sana anaweza kuswekwa ndani kwa kosa la kuitisha mkusanyiko
acha ungese we zwazwa.. wa lumumba
mbona mumeo akiswekwa lopango siku ya kuja mahakaman mnatafutanna wote ndg shangazi mjomba bibi babu mkweo na MASHOGA zako je huwa unaomba kibali[emoji196] [emoji196] [emoji83] [emoji160] [emoji90] [emoji217] [emoji216] [emoji61]
 
Haki gani ya kumtetea Mbowe aliyedanganya Mahakama kuwa yuko mahututi SA mara akaibukia Ubelgiji anapiga self na mgonjwa Lissu huku wakikenua meno kama mazuzu?!! Mahakama siyo ya kuchezea pia naamini watz hawawezi kuchezewa kiasi hicho eti waje Kisutu kwa gharama ya nani na wakikamatwa na kuwekwa lupango utawatetea wakati wapo waliondamana kwenye uchaguzi mdogo Kinondoni wanasota na kesi hata ruzuku hawapati ili ziwasaidie bali group la Mbowe ndiyo linapiga ruzuku pekee yao. Hata Kubenea anajua hivyo!
ruxuku ya fisiem anakula nani
 
Back
Top Bottom