Chadema wafanye maridhiano na wabunge na madiwani wao waliomwandikia barua Dr. Bashiru kuomba kuhamia CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,962
141,961
Binafsi naona kuna tatizo kubwa la kuhamahama kwa viongozi wa Chadema pasi na sababu za kueleweka na kuaminika.

Juzi kaondoka mzee Sumaye na kabla ya hapo Dr Bashiru akiwa Zanzibar City alisema ana barua nyingi tu za wabunge na madiwani wa Chadema wanaoomba kuhamia CCM.

Ni vema basi Chadema wakatafuta maridhiano ya ndani ya chama chao kwanza ambako tatizo liko dhahiri.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kabla ya kuwepo chadema, kulikuwa na ccm tu. Kwa mantiki hiyo, ni ccm ndiyo inayokimbiwa na maelfu, kama sio mamilioni ya wafuasi wake.
Katika nchi yoyote duniani yenye mfumo wa chama kimoja au vyama vingi, Kuna kundi linaitwa wasio na chama na hili lilikuwepo hata hapa Tanzania tulipokuwa chini ya chama kimoja.

Katika mchakato wa kukusanya maoni kama tuendelee na mfumo wa chama kimoja au vingi ,80%+ walisema tuendelee na chama kimoja na hao 20%- waliosema tuingie kwenye vyama vingi ndio wale wasio chama.

Kwa hiyo ,napingana na wewe kwamba kwa kuwa tulikuwa na chama kimoja kimoja basi CCM ndio inakimbiwa. CCM haikimbiwi kwa sababu sio kila mtu alikuwa mwanaCCM na upinzani/CHADEMA ni zao la wale waliokuwa hawana chama wakati wa mfumo wa chama kimoja na si zao baada ya CCM kusambaratika
 
Hakuna mbunge wa diwani aliyeandika barua mkuu kuhamia CCM sio lazima kuandika barua,na kwanini Bashiru kama kweli hawataji? Zile ni siasa tu
 
Bashiru hana barua za maombi lbd listing ya wabunge na madiwani wanaotakiwa kwa UDI na uvumba
 
Binafsi naona kuna tatizo kubwa la kuhamahama kwa viongozi wa Chadema pasi na sababu za kueleweka na kuaminika.

Juzi kaondoka mzee Sumaye na kabla ya hapo Dr Bashiru akiwa Zanzibar City alisema ana barua nyingi tu za wabunge na madiwani wa Chadema wanaoomba kuhamia CCM.

Ni vema basi Chadema wakatafuta maridhiano ya ndani ya chama chao kwanza ambako tatizo liko dhahiri.

Maendeleo hayana vyama!
HUU UTAKUWA UONGO. Dr. aNASITA nini kuwapokea. Kama waliweza figisua viti vyote vya serikali za mitaa, wameshindwa vipi kuwapokea hao wahamiaji, Na mbona bado hawajajitoa CDM
 
Katika nchi yoyote duniani yenye mfumo wa chama kimoja au vyama vingi, Kuna kundi linaitwa wasio na chama na hili lilikuwepo hata hapa Tanzania tulipokuwa chini ya chama kimoja.

Katika mchakato wa kukusanya maoni kama tuendelee na mfumo wa chama kimoja au vingi ,80%+ walisema tuendelee na chama kimoja na hao 20%- waliosema tuingie kwenye vyama vingi ndio wale wasio chama.

Kwa hiyo ,napingana na wewe kwamba kwa kuwa tulikuwa na chama kimoja kimoja basi CCM ndio inakimbiwa. CCM haikimbiwi kwa sababu sio kila mtu alikuwa mwanaCCM na upinzani/CHADEMA ni zao la wale waliokuwa hawana chama wakati wa mfumo wa chama kimoja na si zao baada ya CCM kusambaratika
Una haki na hizo hisia zako.
 
Binafsi naona kuna tatizo kubwa la kuhamahama kwa viongozi wa Chadema pasi na sababu za kueleweka na kuaminika.

Juzi kaondoka mzee Sumaye na kabla ya hapo Dr Bashiru akiwa Zanzibar City alisema ana barua nyingi tu za wabunge na madiwani wa Chadema wanaoomba kuhamia CCM.

Ni vema basi Chadema wakatafuta maridhiano ya ndani ya chama chao kwanza ambako tatizo liko dhahiri.

Maendeleo hayana vyama!
Asiyetaka kubaki Chadema aende tu huko CCM nayo ni demokrasia.
 
Dr Bashiru alikuwa anaheshimika sana kabla ya kujiunga na ccm
Kwa sasa anapiga siasa za kijinga sana
Amebakishiwa za kutolea povu tu.
1572191514899.jpeg
 
Back
Top Bottom