Maridhiano ya CHADEMA na CCM bila kuwaondoa wabunge fake 19 bungeni na kuwaachia wanachama na wafuasi wa CHADEMA Magereza hayana umuhimu

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,073
Maridhiano baina ya ccm na chadema ni wazo zuri sana kwa ustawi wa nchi.

Katika maridhiano hayo chama cha chadema ndicho kilicho umizwa sana na serikali ya ccm.Kwa kuwa ccm inataka maridhiano sharti la kwanza ni ccm kuomba msamaha kwa mabaya yote iliyowatendea wafuasi na wanachama wa chadema ambayo ni mengi sana.

Na ili mazungumzo ya maridhiano yawe na tija ni muhimu kwa chadema kuitaka ccm na serikali yake kutenda haya kwanza

1.Kuwaachia bila masharti wafuasi na wanachama wa chadema waliofungwa na wote walio magerezani kwani kesi zao zilikuwa za kubabikizwa na utawala wa magufuli wakati wa uchaguzi mkuu

2.Kuwaondoa bungeni akina halima na genge lake kwani ubunge wao hauna mkono wa chama cha chadema ulitengenezwa na serikali ya magufuli na watanzania wote ni mashahidi wa uovu huo.

Yakifanyika haye nina imani maridhiano yataafikiwa lakini utakuwa ni unafiki kufanya maridhiano huku ccm ikiendelea kukumbatia uovu ilioufanya kwa hayo mambo 2

Chadema amkeni
 
Tukiondoa hao wabunge 19 na Katiba Mpya, kwa sasa chadema ni dustbin.
 
Na nyie mnawaachia nn?
Au mnadhan maridhiano ni nyie Tu mfanyiwe mnachotaka?
Kwa uspesho gani ambao mnao?
 
Hata kama panahitajika uvumilivu kwenye maridhiano. lakini kuendelea kuwaacha wafungwa wa kisiasa wanatumikia adhabu za uongo, kwa makosa ya uongo, ni dhambi.
Unaweza kuwa shahidi wa kuonesha uongo wao?
 
Maridhiano ni mchakato. Kumbuka waliowapa ubunge ni system nzima na waliofungwa pia walifungwa kwa ku-involve a complicated systematic rogues.

Sio jambo la siku moja.

Kuna majambazi pia nao watataka msamaha kupitia maridhiano🤣🤣
 
Back
Top Bottom