PreGE2025 CHADEMA waburuzana mahakamani, kesi kuanza leo

PreGE2025 CHADEMA waburuzana mahakamani, kesi kuanza leo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
9,522
Reaction score
14,794
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka Zanzibar, wamekiburuza mahakamani chama hicho pamoja na mambo mengine wakilalamikia upendeleo katika mgawanyo wa rasilimali za chama pamoja na stahiki nyinginezo.

Kesi hiyo ya madai namba ya mwaka 2025 imefunguliwa na Said Issa Mohamed, ambaye anajitambulisha kama mwanachama na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu, ambao wanajitambulisha kuwa ni wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho.

Majibu ya CHADEMA soma CHADEMA yaomba siku 21 kujibu hoja zilizowasilishwa Mahakamani na wanachadema wanne kusimamisha shughuli zote za kisiasa za chama

Wamefungua kesi hiyo Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, ikiwa mdaiwa wa kwanza na Katibu Mkuu wa Chadema ni mdaiwa wa pili.

Katika kesi hiyo, wanaiomba Mahakama hiyo itamke kuwa wadaiwa wamekiuka sheria zinazohusiana na vyama vya siasa na Katiba ya chama hicho.

Wamechukua hatua hiyo na kuomba Mahakama iamuru na kutamka hivyo wakidai kuwa kumekuwa na mgawanyo usio sawa wa mali za chama na rasilimali za kifedha kati ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara.

Pia, wanadai kuwa kuna ubaguzi wa kidini na kijinsia; pamoja na kutoa maoni na matamko yaliyo na nia ya kuvuruga muungano kati ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa msingi huo, walalamikaji hao wanaomba Mahakama hiyo itoe hukumu na amri dhidi ya wadaiwa kwamba wamekiuka kifungu cha 6A(1), (2), (5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 Marejeo ya mwaka 2019.

Pia wanaiomba Mahakama hiyo itamke kwamba ugawaji wa fedha, mali na rasilimali kwa ajili ya shughuli za kisiasa na kiutawala kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar unaofanywa na wadaiwa ni kinyume cha sheria na ni batili.

Vilevile wanaiomba Mahakama itamke na kuwaelekeza wadaiwa kuzingatia kifungu cha 6A(1), (2), (5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura ya 258 Marejeo ya mwaka 2019.

Amri nyingine wanazoomba ni kusitishwa kwa muda kwa shughuli zote za kisiasa hadi hapo kutakapokuwepo na utekelezaji wa maagizo ya Mahakama. Na wanaiomba Mahakama hiyo itoe amri ya zuio la kudumu dhidi ya matumizi ya mali, fedha na rasilimali za chama hadi wajibu maombi watakapotekeleza matakwa ya sheria husika.

Mbali na amri hizo, wanaiomba Mahakama iamuru, wadaiwa walipe gharama za kesi hiyo na itoe nafuu nyingine yoyote ambayo Mahakama itaona inafaa kuzitoa.

Kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa na Jaji Hamidu Mwanga, itaanza leo Alhamisi, Aprili 17, 2025.
Tayari Mahakama imeshatoa wito kwa Chadema kupitia Katibu Mkuu kufika mahakamani wakati kesi hiyo itakapotajwa.

Kwa mujibu wa hati ya wito ambayo Mwananchi imeiona, licha ya kukitaarifu chama hicho kuwa kesi hiyo imepangwa kutajwa leo, pia mahakama hiyo imekitaka kuwasilisha maelezo ya utetezi wake kwa maandishi.

"Pia tambua zaidi kuwa ikiwa utashindwa kuwasilisha maelezo yako ya utetezi wa maandishi kwa muda ulioainishwa, Mahakama itaendelea kesi na kutoa hukumu dhidi yako", inasomeka hati hiyo ya wito iliyosainiwa na kugongwa muhuri wa Naibu Msajili Mwandamizi.

Mwananchi

Pia soma ~
CHADEMA yaomba Siku 21 kujibu hoja za Wanachama wao waliowashtaki Mahakamani
 
Chadema waburuzana mahakamani, kesi kuanza leo
Wafunguaji wa kesi hio ni wanachama wa Zanzibar
Hoja ya msingi ktk kesi
1. Ubaguzi
2. Udini
3. Kivunja Muungano
Source: mtandao wa mwananchi
Kwani ni DHAMBI kwenda mahakamani? Nyie Yule Mzee alitaka kwenda mahakamani kupinga Samia kujipitisha kihuni mkamfukuza UANACHAMA
 
Chadema waburuzana mahakamani, kesi kuanza leo
Wafunguaji wa kesi hio ni wanachama wa Zanzibar
Hoja ya msingi ktk kesi
1. Ubaguzi
2. Udini
3. Kivunja Muungano
Source: mtandao wa mwananchi
Kama hiyo habari yako ni ya kweli basi utoto huu unaweza kufa.nywa na CCM tu. Ila wanazidi kumharibia mama yao.
 
Chadema ina wanachama wa zanzibar? Hizo kesi zimesha fail kabla ya kufika mahakamani
Inao mwenyekiti BAWACHA taifa anatoka Zanzibar, Naibu katibu mkuu yupo kutoka Zanzibar na hao wanaoshtaki ni wanachama wa Chadema toka Zanzibar na viongozi wa baraza la wadhamini toka Zanzibar

Hujui hata hayo? Mwana CHADEMA wa wapi
 
Inao mwenyekiti BAWACHA taifa anatoka Zanzibar, Naibu katibu mkuu yupo kutoka Zanzibar na hao wanaoshtaki ni wanachama wa Chadema toka Zanzibar na viongozi wa baraza la wadhamini toka Zanzibar

Hujui hata hayo? Mwana CHADEMA wa wapi
Actualy si mwanachadema, na sina chama. Is why nauliza

One last question nn misingi ya kesi zao? Wana evidence and fact?

Au ndio zile kesi hewa baadae warud nyuma wazifute?
 
Back
Top Bottom