CHADEMA waandamana wakiilalamikia TAKUKURU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA waandamana wakiilalamikia TAKUKURU

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kaa la Moto, Oct 5, 2010.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  04 October 2010
  Mussa Juma, Arusha


  WAGOMBEA wote wa viti vya ubunge na udiwani kupitia tiketi ya Chadema katika Jimbo la Arusha, jana waliandamana kwenda ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), mkoani Arusha, wakiilalamikia taasisi hiyo kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya rushwa, walivyodaiwa kuwa vimekuwa vikifanywa na wagombea wa CCM.

  Tukio hilo la aina yake, lilisababisha kazi katika ofisi za Takukuru, kusimama kwa zaidi ya saa mbili, kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana.Shughuli katika ofisi hizo zilirejea katika hali ya kawaida baada ya kuwasili kwa polisi na kuwatawanya wagombea hao na wapambe wao.


  Wakizungumza na ofisa mmoja wa Takukuru ofisni hapo, wagombea hao wakiwa na jazba, waliiomba taasisi hiyo sasa kutamka kuwa imeshindwa kudhibiti rushwa, ndani ya CCM.Mgombea wa ubunge, Godbless Lema, alisema mara kadhaa wametoa taarifa kuwa wagombea wa CCM, wako katika eneo fulani, wakigawana fedha lakini taasisi hiyo, haiendi kuwakamata.


  "Juzi tu mimi mwenyewe nimewapigia simu kuwa kuna nyumba moja huko Ngulelo, watu wanagawana rushwa. Katika hilo tulipenyeza mtu wetu, lakini kuanzia saa 12 jioni Takukuru hawakuone hadi saa mbili ndipo walikwenda na kukuta tayari wametawanyika," alisema Lema.


  Alisema Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa wa katika Kata ya Sombetini, aliwapa taarifa kuwa kuna watu wanagawiwa fedha na sukari usiku katika kampeni za nyumba kwa nyumba za CCM, lakini pia hakuna hatua zilizochukuliwa.


  "Hata mke wangu juzi kaja hapa tena na usafiri na kuwaambia awapeleke kuna sehemu rushwa inagawanywa lakini hawakwenda. Sasa kama mmeshindwa tuambieni sisi tutajua la kufanya,"alisema Lema.


  Wagombea wa udiwani, Estomii Malla wa Kata ya Kimandolu na John Bayo wa Kata ya Elerai, walidai kuwa na ushahidi wa kutosha kuhusu rushwa inavyotolewa lakini wanashangaa Takukuru, kushindwa kuchukua hatua.


  "Tumekuja hapa kusema wazi kama hamuwezi kupambana na rushwa tuambieni, tutaueleza umma na watajua cha kufanya…mbona wakati wa kura za maoni ndani ya CCM mliweza sasa mnashindwa,"alihoji Malla.


  Baada ya malumbano hayo, ofisa mmoja wa Takukuru aliomba kukutana na mgombea mmoja mmoja ndani ya ofisi yake, lakini wagombea hao walipinga na kutaka kila mgombea aandamane na wanahabari.


  "Sasa mimi nasema siwezi kuwasiliza wote kwanza kamanda wa mkoa hayupo na kama mnasisitiza waandishi siwezi kuwasikiliza kwani kila ofisi ina utaratibu wake,"alisema Afisa huyo.


  Hata hivyo baada ya malumbano ya muda, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha, Zuberi Mwambeji, aliingilia kati na kuwataka wagombea hao kuchagua mwakilishi mmoja na kutoa malalamiko pasipo waandishi wa habari.


  Baada ya hoja hiyo, wagombea hao, walimteua Lema kuonana na ofisa huyo ili kuwapangia siku ya kuonana na kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Arusha, Ayoub Akida.


  Akizungumza mara baada ya kukutana na ofisa huyo, Lema alisema wameshindwa kuafikiana kwani badala ya kuwapangia siku ya kukutana na Kamanda wa Takukuru, alimtaka kuandika malalamiko.
   
 2. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  hiyo ni shida,, hata leo nilikuwa naongea na viongozi wa Chadema hapa arusha, na hilo tatizo lipo sehemu nyingi,, na Kwa taarifa tu Huyu mama anatoa hela mbaya sasa ili Takukuru wakipigiwa simu wanamshtua mgombe naye anakimbia kwa kweli hawa takukuru wanakula na hawa wakubwa na rushwa ndiyo nyumbani kwao na hawatashinda hata..
   
 3. W

  We know next JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi binafsi kwa upande fulani namwamini Dr Hosea, hembu atoe tamko na achukue action ktk hilo, kabla imani yangu kwake haijafutika.
   
 4. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  According to an independent credible source, when it comes to deal with grand corruption, TAKUKURU is doing much better than even FBI
   
 5. h

  hagonga Senior Member

  #5
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaani wewe mkuu bado una imani Hosea!! Waulize wabunge!

  No more comment on this, waacheni wananchi wa Arusha waamue!
   
 6. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nimemuona lema , leo TBC, akilalamika kuwa wakiwapigia TAKUKURU, uwaekea nyimbo kwenye REDIO, ya NIPIGIE, hii ni aibu kwa TAKUKURU na mkurungezi wao HOSEA.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hali hii inatisha na kusikitisha!
  Inamaanisha huyu mama Batilda keshawaweka mfukoni ofisi nzima ya Takukunguru Arusha!
  Aibu sana kwa Hosea na wenziye!

  Give me my shortgun!

   
 8. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #8
  Oct 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Can you site one appropriate example? I am sorry but just your name sounds like a corrupt...
   
 9. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #9
  Oct 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mi nadhani tusiwategemee TAKUKURU sasa. Kwa nini Lema asingechukua vijana wake akaenda kuvamia eneo latukio hadi kikaeleweka?
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Acha ujinga fisadi mkubwa wewe...kwanza hatuna taasisi kama hiyo
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wakuu ni kweli Mama Batilda amekuwa akimwaga rushwa bila kuguswa na mkono wa dola tangu kampeni za ndani CCM ajabu ni kwamba mpinzani wake mkubwa mhe F Mrema hakupewa fursa ya kutoa rushwa na alipojaribu aliishia kudakwa na TAKUKURU sijui kesi yake imetupwa au ilikuwa mbinu ya kummaliza kisiasa.Lazima turudishe kumbukumbu vizuri kamanda wa TAKUKURU alijaribu anga za Mama kule Baraa aliishia kudhalilishwa na kulazimishwa kutoa tamko la kukanusha kuwakamata na kuwahoji wapambe wa mama waliokuwa wakigawana rushwa,au mnataka na yeye atimuliwe kama mkurugenzi wa manispaa.

  Watanzania lazima tusimame kwenye nafasi yetu kuipiga vita rushwa madhara ya rushwa ni makubwa kuliko tunavyoweza kufikiri.wagombea ubunge na udiwani wa vyama vya upinzani nao wamekuwa wakitoa rushwa tofauti yao na wagombea wa CCM ni kiwango cha rushwa wanachotoa kwa wapiga kura.

  Bwana G Lema alitoa rushwa ya tsh 3,000/= kwa wapiga debe, wasukuma mikokoteni na wacheza karata tatu[kamari] kwaajili ya uzinduzi wa tawi jipya kata ya Levolosi.Amekuwa akitoa fedha kati ya 2000/= mpaka 5000/= kwa madereva wa daladala wanabandika picha zaka na kupeperusha bendera za CHADEMA.Bwana Lema amegundua hawezi kuendelea na hili zoezi mpaka tarehe 31/10/2010,hana fedha za kutosha baaadhi ya madereva wa daladala wameanza kubandua picha na bendera kwa kukosa mgao wa kila siku.

  Mama Batilda ana fedha ndefu ya kuonga na ana uwezo wa kuwafikia wapiga kura wengi kwa urahisi kutokana na muundo wa CCM kazi ya kutoa rushwa imekuwa rahisi tofauti na wagombea wengine.
   
 12. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Naogopa kusema vibaya.
  You must be joking !

  Mkivaa hiyo minguo ya kijana na vichwa vinaganda kabisaa.
  Takukuru wanaweza kumkamata Rostam au Batilda?
   
 13. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Ndugu zako wa Rajkot na Mumbai wanakuita urudi kwenu ukasaidie baada ya mafuriko!:mad:
   
 14. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  What a joke!!! According to you everything is good in TZ. So why are we poor after all of these years of independence???
   
 15. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  RAJ PATEL JR bana!!! Haya bana wewe pia una uhuru wako wa kuongea!!!:A S 112:
   
 16. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kaka umesema ukweli kuwa hivi sasa karibu wagombea wote wanatoa rushwa si wa ccm au wapinzani,tatizo ninaloliona hapa ni udogma kwa wana jf wengi yaani wao wakiambiwa tu Ccm imeharibu basi hukimbilia kuishambulia bila ya kuuliza maswali wala kuhoji!Wakiletewa habari na wapinzani hususani toka Chadema basi wao huripuka kama moto wa kifuu na kutoa hukumu bila ya kufikiria.Haya sasa huyu jamaa anaushahidi wa wazi kuwa mgombea wa Chadema katoa rushwa ndogondogo kutokana na uwezo wake kwa madereva wa vipanya na sasa kaishiwa anaanza kutapatapa.Mwaka huu tutaona mengi tutayasikia mengi na yatawakjta mengi nyie msiotumia ubongo kufikiri
   
 17. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Fisadi nyangumi your head must empty, did you eat kachori?
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  PCCB wanatutia AIBU dawa yao iko jikoni
   
 19. a

  as me Member

  #19
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  acha kutuchanganya wewe mambo ya FBI yanatuhusu nini sisi??, hata km takukuru ingekuwa ya kwanza kimataifa km haiwezi kututhibitishia sisi hilo ni upuuzi mtupu, km wanapewa vithibitisho vyote vya harufu ya rushwa then hawachukui hatua c tuwaeleweje?, afu unakuja na story za FBI hapa we vipi
   
 20. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  :hand:
   
Loading...