Elections 2010 CHADEMA waandamana wakiilalamikia TAKUKURU

Hali hii inatisha na kusikitisha!
Inamaanisha huyu mama Batilda keshawaweka mfukoni ofisi nzima ya Takukunguru Arusha!
Aibu sana kwa Hosea na wenziye!

Give me my shortgun!


Give me my shortgun!

Naogopa kukupoteza mapema na ukizingatia na huwa uanakaaa huko A town duuuh na nilivyo tupiwa profile la ndugu zake na huyo Batilda nkachoka. nasikia huwa anatembea na Body Guard jamani huyo ni mbungeee au ni ??

Nakuja kwa hao takukuru ashukuru sana Hosea wakati nilipo pita pita huko kwenye kampeni mikoani nilijionea mengi ila sikuwa na vitendea kazi ninge record scrip chache na kumtumia kwani kuna wagombea wengine kabisa walikuwa wanapewa information directly toka Takukuru kinachoendelea ni nini na atafanya nini na asilimia kubwa ni wale waliokuwa wana mihela mingi wakati wa kura za maoni.

Kwa hilo sishangai kuona upane wa huyo mama Batilda kubebwa na Takukuru kwani EL bado ananguvu sana hap A town na hilo alina ubishi na twasikia wana CCM wamejitenga sana hata kujishughurisha kumsaidia huyo mama kampeni hawataki kabisa kwani inavyosemekani ni sio chaguo lao, Jambo la kujiuliza wana JF kama kweli wewe ni chaguo la wananchi sidhani unaweza kila kukicha wewe scandal ziko nyuma yako nini kunani hapo unakubalika au ndio hukubaliki maaan kama ukipita na usipo wafanyia maendeleo hawa watu wa jimbo lako inakula kwako 2015 bila ubishi ndugu wagombea.

Mifano dhahili inaonekana huko IRINGA,NYAMAGANA HAPA KWETU,NZEGA kwa Bashe, na ndio maana wanakuambia mabadiriko yajapo hayazuiriki hata hao JWTZ wafanyaje huto zui bari ndio mtaanzisha umwagaji wa damu wekeni uchaguzi uwe wa huru na haki , takukuru kama mwambiwa then mwawatonya wagombea ambao mwatakiwa enda kuwakamata na mkifika hapo bila aibu unawapigia simu wale watu waliokuambia isssue ati mbona hao mnao wasema hawapo hiyo ni kazi na huku mlichelewa kwenda jamani khaaaa
 
we are we exactly going and wat a we doing??, takukuru ndio wa wanza kuomba ushirikiano na wananchi, wanapoonyeshwa ushirikiano huo hawautilii maanani 2waeleweje?.ila kama ipo ipo tu ipo siku kitaelewaka tu
 
Bwana G Lema alitoa rushwa ya tsh 3,000/= kwa wapiga debe, wasukuma mikokoteni na wacheza karata tatu[kamari] kwaajili ya uzinduzi wa tawi jipya kata ya Levolosi.Amekuwa akitoa fedha kati ya 2000/= mpaka 5000/= kwa madereva wa daladala wanabandika picha zaka na kupeperusha bendera za CHADEMA.Bwana Lema amegundua hawezi kuendelea na hili zoezi mpaka tarehe 31/10/2010,hana fedha za kutosha baaadhi ya madereva wa daladala wameanza kubandua picha na bendera kwa kukosa mgao wa kila siku.

Nyie Chadema hebu semeni kuhusu hilo hapo juu!
 
Wakuu ni kweli Mama Batilda amekuwa akimwaga rushwa bila kuguswa na mkono wa dola tangu kampeni za ndani CCM ajabu ni kwamba mpinzani wake mkubwa mhe F Mrema hakupewa fursa ya kutoa rushwa na alipojaribu aliishia kudakwa na TAKUKURU sijui kesi yake imetupwa au ilikuwa mbinu ya kummaliza kisiasa.Lazima turudishe kumbukumbu vizuri kamanda wa TAKUKURU alijaribu anga za Mama kule Baraa aliishia kudhalilishwa na kulazimishwa kutoa tamko la kukanusha kuwakamata na kuwahoji wapambe wa mama waliokuwa wakigawana rushwa,au mnataka na yeye atimuliwe kama mkurugenzi wa manispaa.

Watanzania lazima tusimame kwenye nafasi yetu kuipiga vita rushwa madhara ya rushwa ni makubwa kuliko tunavyoweza kufikiri.wagombea ubunge na udiwani wa vyama vya upinzani nao wamekuwa wakitoa rushwa tofauti yao na wagombea wa CCM ni kiwango cha rushwa wanachotoa kwa wapiga kura.

Bwana G Lema alitoa rushwa ya tsh 3,000/= kwa wapiga debe, wasukuma mikokoteni na wacheza karata tatu[kamari] kwaajili ya uzinduzi wa tawi jipya kata ya Levolosi.Amekuwa akitoa fedha kati ya 2000/= mpaka 5000/= kwa madereva wa daladala wanabandika picha zaka na kupeperusha bendera za CHADEMA.Bwana Lema amegundua hawezi kuendelea na hili zoezi mpaka tarehe 31/10/2010,hana fedha za kutosha baaadhi ya madereva wa daladala wameanza kubandua picha na bendera kwa kukosa mgao wa kila siku.

Mama Batilda ana fedha ndefu ya kuonga na ana uwezo wa kuwafikia wapiga kura wengi kwa urahisi kutokana na muundo wa CCM kazi ya kutoa rushwa imekuwa rahisi tofauti na wagombea wengine.
Pole sana kaka kwa kutunga Uongo hapa Swala la Lema kutoa Rushwa kwa Lema i doubt..By the way do you still think MAXMILAN ATSHINDA?ENDELEA KUPIGA DEBE HUMU JAMVINI...LEMA ATASHINDA YOU HAVE WROTE A HOAX BRO.
 
Pole sana kaka kwa kutunga Uongo hapa Swala la Lema kutoa Rushwa kwa Lema i doubt..By the way do you still think MAXMILAN ATSHINDA?ENDELEA KUPIGA DEBE HUMU JAMVINI...LEMA ATASHINDA YOU HAVE WROTE A HOAX BRO.


Asante sana Dada / Kaka BRIA.

Maxmilan hawezi kushinda ubunge zipo sababu kibao moja kubwa hana fedha za rushwa[kama anazo hataki kutoa rushwa sijui wewe utampigia mgombea gani anayepinga rushwa kwa vitendo au utakimbilia mgombea wa chama chako] kama walivyo Lema na Batilda.Wagombea wa CUF,demokrasia makini na TLP hawana nafasi ya kushinda ubunge Arusha mjini kwasababu mpaka sasa wanafikiri kushinda ubunge Arusha au Tanzania ni mikutano na kubandika post kumbe unatakiwa kutoa rushwa,kumwaga fitina mbaya dhidi ya wapinzania wako.Nafasi ya kushinda inawezekana iwapo wapiga kura wataamua kuwatupa watoa rushwa na kuwaunga mkono wagombea wasiotoa rushwa.Arumeru magharibi na hata Arusha mjini inaweza kutokea.

Kuhusu Lema kutoa rushwa halina ubishi hata jana aliwenda kata ya Suye sehemu ilipohamishiwa krokoni [garage] akawanunulia mafundi viroba vya konyagi ili mkutano wa Lyimo ushindwe kufanyika lakini mambo yakawa tofauti na mipango yake.Inaelekea wewe ni aina ya wapenzi wasiokuwa tayari kusikia lolote baya dhidi ya mgombea wako / chama chako.Nenda kata ya Levolosi walipo mafundi na mama lishe waulize kiungwana Lema kawafanyia nini wakati wa ufunguzi wa tawi la CHADEMA.Juzi nilipanda daladala la kwenda Kisongo kufika eneo la uwanja wa ndege tukapa pancha tairi ya mbele,dereve na kondaka wakaanza kulaumiana kwa uzembe hawakuwa na spare tyre ya kubadili kondakata akakata kulaumiwa kwa maelezo hakuwa na fedha ya kukomboa tairi kwa fundi mziba pancha dereva akamjia juu mbona jana na leo umechukua mgao wa CHADEMA.Abiria bila chenga wala zengwe tukamuuliza dreva kulikoni mpewe mgao CHADEMA akacheka sana akajibu hapa mjini mzee vifodi vyote unavyoviona vina bendera na picha za wagombea wa vyama wanapewa fedha kwa kukubali kutangaza chama/mgombea.


Nilikuwa natazama TBC1 nikabaki nacheka jinsi Lema alivyo msanii mwenzake akitoa rushwa kosa yeye na wafuasi wake kama wewe akitoa rushwa ruksa.Tanzania ni yetu sote kama tumeamua kuchagua viongozi kwa njia ya rushwa ni vyema tukaalalisha kwa wote.Ubaya unakuja pale kikundi fulani kinapewa fursa ya kutoa rushwa huku vyombo husika vikibaki vinakodoa macho.

Tuichukie rushwa bila kujali inatolewa na nani na ni kiasi gani iwe ndogo ama kubwa madhara yake bado yatabaki makubwa kwa jamii.Tuache kudhani rushwa inatolewa na CCM pekee yake hata wapinzani wanatoa rushwa Lema kadhiirisha sijui majimbo mengine hali ikoje.

Wiki iliyopita nilikuwa Arumeru Magharibi kule mgombea wa CCM Ole medeye anamwaga rushwa kama mvua ya mawe hakuna wa kumkamata dalili za mwanzo zinaonyesha mgombea wa CHADEMA Ole Kisambu atashinda ingawa hatoa rushwa.mfano wa Arumeru unaweza kutoa somo zuri kwa Bwana Lema kwamba si mara zote rushwa ushinda haki.
 
Back
Top Bottom