CHADEMA waamua kuchimba visima 11 Igunga na Kafumu haonekani tena Igunga!

Hizi ndo fikra za kizamani, jimbo moja mtu mwenye Dr tena afisa mkubwa ndani ya serikali unataka kutuambia akifanya mkutano na kuongolea namna atakavyosaidiana na wananchi kusolve hizo inshu za jimbo atakuwa amewahi sana?

This is 21st century tumechelewa unataka tuendelee kutembea wakati inshu kama za maji zilitakiwa ziwe historia, watu bado tunahangaika na vitu ambavyo vinagusa maisha kila siku lakini viongozi hawaoni namna ya kumaliza tatizo zaidi ya kujitafutia mtaji wa kura.

Kila kitu kinahitaji mipango madhubuti ili kufikia malengo.

Naamini kuwa Kafumu anajipanga, kwakuwa matatizo ni mengi lazma apange mikakati madhubuti.
 
Siyo lazima kusubiri hadi asubiri kuapishwa wakati watu wanateseka na uhaba wa chakula, maji, elimu nk! He has to show at least his concern, maji kila mtu anajua ndo uhai wa mwanadamu unataka wasubiri hadi wabaki mifupa ndo uanze kusema Kafumu rudi jimboni kwako. !lol
ndiooo!
 
Tuacha ushabiki, Kiongozi gani anaweza kuleta maendeleo ndani ya wiki mbili. Ni mapema sana kumsemea Kafumu.


Mkuu zambia sata ndani ya siku9 amefanya maajabu uchumi umeimalika kwacha imepanda dola inashuka mishahala imepanda huyo nikiongozi wa nchi igunga ni kajimbo tuachane na hilo jee chadema wanamiaka mingapi? hadii kuyaona matatizo ya wanaigunga miaka50 ya uhuru ndani ya igunga ni ccm au cdm kwani utowe visingizio ni wiki2 cdm ndowana wiki2
 
Kuapishwa kwenyewe bado halafu aanze tuu nyie viazi kweli kafumu ni mbunge mteule bado hajawa mbunge kamili subirini akiapishhwa muone mziki wa CCM
tuone mziki wa CCM upi, huyo Vasco wao ana miaka sita saa hizi madarakani hatujaona mziki wake wa ahadi alizozitoa 2005, CCM wamezoea kutoa ahadi za kupata kura na kuendelea kutumia ujinga wa watanzania kuwaaamini.

Chadema naomba muwafundishe CCM, timizeni ahadi hata kama hamkushinda uchaguzi hata kama uwezo wenu ni mdogo. Mungu atawabariki na laana ya CCM itaendelea kwa kuendelea kuwadanganya watanzania.
 
Kila kitu kinahitaji mipango madhubuti ili kufikia malengo.

Naamini kuwa Kafumu anajipanga, kwakuwa matatizo ni mengi lazma apange mikakati madhubuti.
Tunajua ataendelea kujipanga mpaka 2015 na wakati wa kampeni atatuambia tumpe tena kura atekeleze ahadi maana keshajipanga. Kafumu ni balaa jingine
 
wanaochimba visima ni chadema au ni Sabodo?


sabodo nikada wa ccm nimwanachama hai ni mfadhili wa ccm nikwa nini ameamuwa kuigeukia cdm nakuipa mgongo ccm misada anayotowa ccm inaichia mifukoni mwa watu haifiki kwa wana nchi kama umemsikia anasema nibola cdm ishinde 2015 anasema kafulaiswa na msimamo wa silahaa
 
Chama cha magamba wametumia zaidi ya bil 3 kwenye uchaguzi huo kwa muda wa mwezi 1 wa kampeni zao,wanaonekana kuwa na hela za kutumia hovyohovyo.Kwa nn sio kwenye mambo ya msingi kama ya kutatua kero za wananchi?
Kingeshinda chama kingine ingekuwa sahihi kuwapa muda lkn sio ccm!
Na nyie watu wa Igunga na tabora kwa ujumla YOU ARE BREAKING OUR HEART! kumbukeni enzi za mzigo mzito mbebeshe myamwezi zimeshaisha.
Mlikuwa mnalialia RA alipokuwa anajivua gamba.Amewaletea nn kwa miaka yote aliyokaa zaidi ya kuwaletea umasikini kwenu na nchi nzima?
Mnaudhi sanaaana nyie! Kwenye biblia imeandikwa yesu alikuja kuwakomboa watu katka utumwa wa dhambi lakn watu wakamuua hatimaye.Na nyie ndo walewale wa kuridhka na matatizo.NDUHU TABU GETE! NAHENE MIJAMPOLA!
 
Aliyetoa tamko la kuchimba visima ni Sabodo au Slaa wa CDM, au kama hujafuatilia thread vizuri ruksa to read it again, carefully.

mwambie kijana huyo,maana wengne kwa kubaka mada tuuu.
 
Kuapishwa kwenyewe bado halafu aanze tuu nyie viazi kweli kafumu ni mbunge mteule bado hajawa mbunge kamili subirini akiapishhwa muone mziki wa CCM

CCM hawana jipya kwani RA amekaa muda mrefu na mpaka sasa ni shida na aibu igunga? au alikuwa bado hajaapishwa? hakua mb wa ccm? Ninacho jua mimi mbunge wa wananchi igunga ni kashindye, hoyo kafumu ni mbunge wa ccm tena huko dar, muache aungane na kina david matayo ambao huonekana jimboni kipindi cha kampeni tu.
 
Tuacha ushabiki, Kiongozi gani anaweza kuleta maendeleo ndani ya wiki mbili. Ni mapema sana kumsemea Kafumu.

Dr Kafumu ni Mbunge wa Igunga;kachaguliwa na wana Igunga lkn sherehe za kujipongeza zinafanyikia Dar! Hata mtoto mdogo hapo atajua kuwa Igunga wameula wa chuya!
 
tuacha ushabiki, kiongozi gani anaweza kuleta maendeleo ndani ya wiki mbili. Ni mapema sana kumsemea kafumu.

kweli usolijua usiku giza totolo,kasome upya binadamu anakuwa na uwezo wa kutenda kaz kwa bidii wakat up?au ndo nyie kijana taifa la kesho!tuache kutetea uzembe tuwaonee huruma watesekao.
 
Tuacha ushabiki, Kiongozi gani anaweza kuleta maendeleo ndani ya wiki mbili. Ni mapema sana kumsemea Kafumu.

Wiki mbili mbona zinatosha sana kuweka mikakati kama walivyofanya CDM? Mwacheni Kafumu arudishe zile hela alizohonga kule Igunga, ndio wakati wake huu!
 
wanaochimba visima ni chadema au ni Sabodo?

Tatizo magamba si wabunifu, wakijitahidi ni kwa maslahi yao, sabodo hawezi kuwapa magamba fedha kwani anajua fika haziwezi kuwafikia wananchi bila kuchakachuliwa kwa uhakika.
 
nyie mbona mnafadhiliwa miradi mingi na world bank & IMF bado mnashindwa kuisimamia.

Nyie kina nani? Mi siwakili chama hapa..natoa maoni ya ujumla. Tukubali kushindwa na tuache watu wafanye kazi zao...kama sabodo kaamua kutoa msaada safi mtanzania mwenzetu anasaidia watanzania wenzake. Sa CDM hapa sijui imeingiaje
 
Kuapishwa kwenyewe bado halafu aanze tuu nyie viazi kweli kafumu ni mbunge mteule bado hajawa mbunge kamili subirini akiapishhwa muone mziki wa CCM

Wee ndio kiazi kweli, watu wana shida halafu unangoja eti aapishwe, kwa kujua shida za watu CDM wameamua pamoja na kushindwa kwao kwa mizengwe hawajasubiri ushindi wala kuapishwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom