CHADEMA waamua kuchimba visima 11 Igunga na Kafumu haonekani tena Igunga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA waamua kuchimba visima 11 Igunga na Kafumu haonekani tena Igunga!

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by MAGAMBA MATATU, Oct 14, 2011.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Dk Slaa anena
  Dk Slaa amesema chama hicho kinatarajia kuchimba visima vya maji 11 katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora ikiwa ni wiki takriban mbili tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika Oktoba 2.

  Dk Slaa alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kukabidhi mchanganuo wa namna walivyogawa mradi wa utekelezaji wa visima 200, vilivyotolewa na Sabodo kwa lengo la kuchimbwa katika majimbo tofuati wanakotoka wabunge wa Chadema.

  Alisema lengo la kutekeleza mradi huo wa maji katika Jimbo la Igunga limetokana na ziara aliyoifanya katika vijiji 98, vilivyopo katika jimbo hilo na kugundua wananchi wake wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji.

  “Katika mpango kazi wetu, tumepanga kuchimba visima 11 katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, hii imetokana na ziara yangu katika vijiji 98 ambapo niligundua kuwa wakazi hao wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji,”alifafanua Dk Slaa.

  Chadema kilishika nafasi ya pili katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, kwa aliyekuwa mgombea wake, Joseph Kashindye kupata kura 23,260 sawa na asilimia 44.3, nyuma ya mgombea wa CCM, Dalaly Kafumu aliyeshinda kwa kura 26,484 kati ya 52,487 halali zilizopigwa, sawa na asilimia 50.4.

  Habari zinasemekana kuwa baada ya Kafumu wa CCM kushinda ubunge tayari ameisha weka makazi ya kudumu Mbezi beach Dar es Salaam na kuwaacha wananchi wa Igunga wakifa na njaa na kuhangaika huku na kule kutafuta maji,,,hiki kitendo kimefanya CHADEMA waamue kuanza kuwatekelezea mradi wa visima 11 vya maji wananchi wa Igunga japo hawakushinda ndani ya hilo jimbo kwani kipindi cha kampeni Dr Slaa aliona ni kiasi gani wanachi wa Igunga wanavyoteseka na uhaba wa maji..
   
 2. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Tuacha ushabiki, Kiongozi gani anaweza kuleta maendeleo ndani ya wiki mbili. Ni mapema sana kumsemea Kafumu.
   
 3. B

  BMT JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  we unataka apewe miaka mingapi?mbona wakat anaomba kura alitoa ahadi nying,swali atazitekeleza lini??tuwen makni kuchangia,kwahyo we una ona raha wana igunga wanavyotabka?
   
 4. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hivi mbunge aliyekuwepo ameshikilia jimbo kwa muda gani vile? tukumbushane.....
   
 5. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kuapishwa kwenyewe bado halafu aanze tuu nyie viazi kweli kafumu ni mbunge mteule bado hajawa mbunge kamili subirini akiapishhwa muone mziki wa CCM
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  sioni raha wana Igunga wanavyopata tabu ila ndani ya wiki mbili hauwezi kuupima utendaji wake.
   
 7. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  tusimhukumu mtu kwa historia. Hata kama Rostam angekuwa ameshika jimbo kwa miaka mia haitoshi kumhukumu Kafumu.
   
 8. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  tatizo hawa jamaa hawataki kufikirisha akili.
   
 9. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 667
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 80
  Ni ngumu sana kwa sasa kwa Kafumu kurudi Igunga kulingana na matukio ya mauaji yanayoibuka huko kufuatia kampeni chafu za CCM. Na hata akitokea na kujaribu kuitisha mkutano wowote ule itakuwa ni aibu na fedheha kubwa kwake! Aendelee tu kula kuku Mbezi Beach! Alichokitaka keshakipata!
   
 10. C

  Chesty JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,335
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  CDM ndani ya wiki mbili tayari wana namba ya visima watakavyo chimba, hii inaonesha jinsi watu walivyo na mipango ya kuwajali wananchi masikini kama wa Igunga ambao umasikini wao unasababishwa na kuwepo kwa CCM Tanzania.

  Halafu unasema ndani ya wiki mbili, kama CCM kimeshindwa kuleta maendeleo yao for 50 years sitegemei hata miaka minne iliyobaki inatosha.
   
 11. undugukazi

  undugukazi JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Chadema wana majukumu gani nchini??? Na ni mradi wa kwanza kuufanya kama utafanyika kweli..kwani sabodo si ndio mfadiri. Acheni maneno kanga na muache siasa za kitoto. Ni mimi nisie na chama
   
 12. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  jina lako linaendana na mchango wako.
   
 13. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  wanaochimba visima ni chadema au ni Sabodo?
   
 14. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  asante.
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kafumu ana wiki mbili ila RA alikaa pale for 15 years ndani ya CCM
  Kafumu anakula shavu!
   
 16. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hizi ndo fikra za kizamani, jimbo moja mtu mwenye Dr tena afisa mkubwa ndani ya serikali unataka kutuambia akifanya mkutano na kuongolea namna atakavyosaidiana na wananchi kusolve hizo inshu za jimbo atakuwa amewahi sana?

  This is 21st century tumechelewa unataka tuendelee kutembea wakati inshu kama za maji zilitakiwa ziwe historia, watu bado tunahangaika na vitu ambavyo vinagusa maisha kila siku lakini viongozi hawaoni namna ya kumaliza tatizo zaidi ya kujitafutia mtaji wa kura.
   
 17. only83

  only83 JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Julius Mtatiro aliwai kusema wakati wa uchaguzi wa Igunga kuwa na hapa namnukuu.."Mkichagua ovyo ovyo haipaswi kuja kulalamika ovyo ovyo kwasababu ya uchaguzi wenu wa ovyo ovyo" mimi nadhani hiki ndicho walichokichagua wana-Igunga na wanapaswa wavune walichopanda...kwa upande wa pili,nakipongeza chama changu CDM kwa uamuzi huu wa hekima kwa kuamua kuonyesha kuwa chama cha siasa sio kupiga domo tu kama wengine wanavyofanya,bali ni kutumikia wanachi kwa kuondoa kero zao na matatizo yao......vinginevyo wana-Igunga wataona madhara ya kuchagua ovyo ovyo...........
   
 18. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Siyo lazima kusubiri hadi asubiri kuapishwa wakati watu wanateseka na uhaba wa chakula, maji, elimu nk! He has to show at least his concern, maji kila mtu anajua ndo uhai wa mwanadamu unataka wasubiri hadi wabaki mifupa ndo uanze kusema Kafumu rudi jimboni kwako. !lol
   
 19. C

  Chesty JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,335
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  Aliyetoa tamko la kuchimba visima ni Sabodo au Slaa wa CDM, au kama hujafuatilia thread vizuri ruksa to read it again, carefully.
   
 20. L

  Luiz JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nyie mbona mnafadhiliwa miradi mingi na world bank & IMF bado mnashindwa kuisimamia.
   
Loading...