CHADEMA vunjeni UKAWA

CHADEMA vunjeni UKAWA

Ukuwa wawaachie majimbo ambayo chadema ina nguvu wasi nganganie pia uraisi chadema ndo watoe raisi kwa sababu wana nguvu labda makamo ndo atoke chama kingine

Kasome kwanza katiba ya JMT ya 1977, jinsi VP/running mate anavyopatikana ndio uje utoe maoni yako.

Vinginevyo unachekesha ku-suggest VP atako chama tofauti na Rais.
 
Segerea Mpendazoe alikosa kwasababu Wapinzani waligawana kura. i.e Jumla ya kura za Wapinzani zilikuwa zaidi ya CCM. Tarime CDM walikosa lakini kura za CDM + CUF zilikuwa zaidi ya CCM. The same scenerio kwa majimbo mengine. Je, nini kinachokufanya uamini kwamba 2015 hali kama hiyo haitatokea tena?

Lakini pia, lengo kuu la UKAWA ni kumuondoa mkoloni mweusi CCM madarakani, sio CDM kupata viti vingi vya ubunge. CDM ime sacrifice hayo kwa masilahi mapana ya Watanzania.
Sasa tutapata mkoloni mweupe?
 
Kwa majimbo kama segerea, ukonga, kigamboni, Serengeti, morogoro mjini na kilosa chadema ina nguvu Sana ukilinganisha na vyama vingine ndani ya ukawa...mi naona Ni bora hayo majimbo vyama vingine vikakubari kugawana hayo mengine yaliyobaki..
Nguvu ya chadema segerea ipo wapi? Mpendazoe mmemdanganya kuwa mtamsaidia katika kesi yake mpaka kafilisika anakimbilia kishapu kubahatisha labda mungu atamjaalia
 
Hivi unajua ulichoandika au ndio yale yale akili kama KENGEZA. Unachomaanisha kuwa Rais atoke UKAWA. halafu haujali hata kama CCM wakiwa na robotatu ya wabunge mjengoni? Na wasiwasi na upeo wako wa kufikiri

Wewe ni MBURUKENGE. I shall repeat again. THE MAIN OBJECTIVE/GOAL of UKAWA is to oust CCM from power, not CDM to get the lion shares of constituencies at the expenses of the other parties making UKAWA. Understood dude.
 
Wewe ni MBURUKENGE. I shall repeat again. THE MAIN OBJECTIVE/GOAL of UKAWA is to oust CCM from power, not CDM to get the lion shares of constituencies at the expenses of the other parties making UKAWA. Understood dude.

Makamanda vipi tena mbona mnarushiana maneno ya kejeli?
 
Mwaka huu raha sana... Tukumbuke na kulima Jamani tusijisahau sana kila kukicha Siasa Kumbukeni hao Viongozi Hayo Ndiyo mashamba Yao so shabikia Siasa Watoto wanapiga miayo
 
Sasa wewe shangazi mbona unahasira hivi umefukuzwa na mmeo?funguka mama yangu.


swissme

utaachwa na mume wako baada ya kukaa ukapika kutwa uko hapa,chunga sana usije ukapewa talaka ukafanya umalaya
 
Muungano wa ukawa una faida zaidi kwa kura ya urais ila kwa ubunge na udiwani chadema tumeingia mkenge
 
UKAWA haivunjiki nyie..Najua hakuna kitu kinawanyima usingizi kama huu Muungano...Matatizo yatarekebishwa lakini UKAWA haivunjiki,hakuna chama kinachojitoa aisee

Poleni CCM
 
Kwa majimbo kama segerea, ukonga, kigamboni, Serengeti, morogoro mjini na kilosa chadema ina nguvu Sana ukilinganisha na vyama vingine ndani ya ukawa...mi naona Ni bora hayo majimbo vyama vingine vikakubari kugawana hayo mengine yaliyobaki..

Kwa kweli hali hii inasikitisha sana katika hatua hii ukawa iliyofikia vyama vingine vianze kuleta unganganizi kwa majimbo ambayo hawana mitaji au uwekezaji wowote huko.Utaona hata kwenye nafasi kubwa kama ya uraisi. Katika makubaliano ya vyama vilivyounda ukawa walikubaliana jimbo lolote lenye m-bunge wa chama mshirika nafasi itaachiwa chama husika.Kwa yale yenye wabunge wa ccm wataangalia matokeo ya uchaguzi 2010. Chama kilichopata kura zaidi ya kingine kwenye muungano kitaachiwa jimbo maana wamewekeza na ndio mtaji wao. Ikitokea hakuna chama kilichoshiriki basi watachukua maoni kutoka jimbo hilo chama kinachokubalika zaidi ndio kisimamishe mgombea. Ni wazi wala halihitaji kulitolea ushahidi kuwa chadema bara inakubalika na imewekeza zaidi kuliko vyama washirika tofauti na visiwani ambapo cuf wana nguvu pengine zaidi ya chama tawala. Ni kweli pia mikoa kama Pwani,sehemu ya Dsm,Mtwara,Lindi,Songea,Tanga na sehem ya mkoa wa Tabora cuf wanakubalika zaidi hivyo ni busara kuwaachia majimbo mengi ya mikoa hiyo. Sikatai Nccr nao ni vinara mkoani Kigoma nao waachiwe ila angalizo kwa wabunge wa Nccr wa mkoa huo wasijedanganyika kujiunga na chama kilicho nje ya ukawa kwani watapoteza kwani hawatachaguliwa. Pia nakiri katika jimbo la Vunjo pamoja na kwamba chadema ina nguvu sana pale lakini m/kiti wa taifa nccr James Mbatia nae ana nguvu sana pale na anaaminiwa. Kwanza alishakuwa m-bunge pale. Kwangu namhesabu kama m-bunge anaesubiri kuapishwa tu. Hivyo hivyo kwa nafasi ya uraisi chadema 2010 ndio waliokuwa nyuma ya ccm hivyo busara inaonyesha wapewe nafasi hiyo. Umoja huu makusudio yake ni kuingoa ccm madarakani na sio chama gani kimepata majimbo mengi. Au kwa kuwa nyie mmepata majimbo mengi basi nafasi ya uraisi iende chama kingine. Tukianza kutafuta usawa wa namna hiyo hakika tutapoteza majimbo mengi na uraisi pia. Hivyo hivyo kufikiri kuuvunja umoja katika hatua hii. Naomba busara kubwa walizo nazo viongozi wa juu itumike sana. Hapo mungu atadhihirika mbele yenu na hakika mtafanikiwa. Msiyasikilize haya masaliti yanayojiingiza kutaka kuwavuruga. Haya ni mandege John tu mandoroooobooo tu.
 
Wewe ni MBURUKENGE. I shall repeat again. THE MAIN OBJECTIVE/GOAL of UKAWA is to oust CCM from power, not CDM to get the lion shares of constituencies at the expenses of the other parties making UKAWA. Understood dude.

Wewe ndio MBURUKENGE Hivi ukiwa na Rais kutoka CHADEMA au UKAWA Halafu watunga sheria na wapitisha bajeti wakawa ni CCM Kuna serikali hapo? hivi unajua wabunge wanapower ya kumng'oa Rais Madarakani? Akili yako inaonekana ndogo na siasa umejifunzia ukubwani. Huwezi kujizatiti eti ushinde urais then percent kubwa ya wabunge watoke chama kingine. yaani wewe ni Bogus kama lile KENGEZA Lenu la UFIPA
 
Kama kweli tunataka mabadiliko UKAWA ivunjwe tu kwa sababu zifuatazo:-

1. Kuna baadhi ya majimbo CHADEMA walikuwa na nafasi 2010 lakini leo wamewapa CUF na NCCR Mageuzi.

i) Segerea - Mpendazoe alikosa kiduchu tu
ii) Tarime - CHADEMA ina nguvu
iii) Serengeti - CHADEMA ina nguvu... na maeneo mengine mengi.

2. Urais NCCR Mageuzi na CUF wanataka.Swali la kujiuliza mwaka 2010 dr. Slaa alifanya vizuri sana.

Mimi binafisi sioni umuhimu wa kugombania nafasi ya Urais kama NCCR Mageuzi na CUF wanataka Urais. Ni heri UKAWA ukavunjwa ili CHADEMA waendelee na hakuna kulala.

Na watapata wabunge wengi tu watakosa Kusini na baadhi ya mikoa kama Tanga na Zanzibar.
Mkuu unaweza kuwa na point,lakini kwa sasa naomba tuangalie maslahi mapana ya taifa
letu,ni vema tuelewe kuwa tunaposema UKAWA tumaanishe muungano wa vyama
vinavyounda umoja huu,hapa namaanisha kama mimi ni mfuasi wa chama A
ambacho ni mshiriki wa UKAWA ikawa kwa bahati mbaya kwenye jimbo langu
chama A hakijasimamisha mgombea lakini chama B/C... ambao ni UKAWA wamesimamisha
mimi niunge mkono mgombea wa chama B/C... hapa lengo kubwa ni kuona
nchi yetu inaingia kwenye demokrasia ya kweli.Tukiendeleza mapenzi ya vyama vyetu
kiubaguzi hatutafika mbali,zaidi tutatawaliwa kimabavu na kijani mpaka tukome.
 
Nimefurahi sana hakuna aliyetaja CCM katika comments zenu zamani Hata mvua isiponyesha basi CCM
 
Huu umoja ukivunja kura yangu bora iende CCM tu.. Hapa ndio nitaona Upinzani uko kimaslai na si kuwakomboa watanzania
 
Mleta mada ana wazo zuri, lakini naona ni la kujenga chama kimoja, ambacho ni Chadema. Sidhani kama kwa sasa nguvu za chama kimojamoja zinaweza zikaiondoa CCM madarakani. Popote mtu anapopewa nafasi ya kugombea nafasi, kwamba katoka NCCR, CUF au CHADEMA lengo ni kuweka Mbadala wa CCM na sio kuongeza viti kwa chama kilichopata nafasi ya kuweka mgombea. Hapa tunaangalia maslahi mapana.
 
Back
Top Bottom