Chadema, viongozi wenu pia wametokea CCM

Chadema, viongozi wenu pia wametokea CCM

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
20,142
Reaction score
24,432
Makamanda baada ya orodha ya wateule ma DC kutoka kila mmoja ameanza kejeli ooh UVCCM wametoswa wamechukuliwa waliounga juhudi. Tatizo liko wapi, kwanza ni Watanzania sio Wakenya.

Pili, mbona nyie mlimpa ukatibu mkuu Dk Slaa toka CCM, mkampa Lowassa nafasi ya ujumbe wa kamati kuu ili hali wapo waliosota na kuijenga Chadema bado haikutosha na akapeperusha bendera ya kugombea urais. Sumaye akawa mwenyekiti wa kanda, Nyalandu na wengineo.

Vipi hakuna watu waliokua na uwezo mpaka mkasubiri watu toka CCM kuja kuwaongoza.

Watu wakiachwa ooh wamekwenda kuunga juhudi lakini hawateuliwi wakiteuliwa ooh UVCCM na CCM wakongwe wameachwa.

Makamanda mkitaka kuongea malizeni kutafuna kwanza kilichopo mdomoni!

Naona maswali hakuna kazi iendelee!
 
Kwenda hawataki, kurudi hawataki, kukaa hawataki. Hawataki, hawataki. Ukiwauliza wanataka nini, wanasema Katiba Mpya.
 
Mnaumia kinyama!! Ndio ishakuwa hivyo hakuna namna bwashee. Subirini utawala mwingine tena. Hivi Wakudadavuwa Bia yetu wako wapi siku hizi? Unaweza kukuta wananyea ndoo huko kama 7ya
 
Back
Top Bottom