TAKUKURU Ikimaliza Kuichunguza CHADEMA Watumie Ripoti ya Wizi wa Mali za CCM ya Bashiru Kuichunguza CCM pia

FACTSFIRST

Senior Member
Dec 6, 2019
191
290
Katika kuendeleza mashambulizi dhidi ya CHADEMA na Mbowe, serikali ya CCM imeiagiza TAKUKURU kuchunguza tuhuma za ubadhilifu wa fedha ndani ya CHADEMA. Mbali na ripoti ya CAG kueleza wazi kuwa kulikuwa na kasoro kadhaa katika taarifa za fedha za vyama vyote, vikiwemo CCM na CUF, TAKUKURU wameamua kuiandama CHADEMA kwa malengo maalum, sambamba na jitihada nyingine chafu za kutaka kuidhoofisha CHADEMA.

Nawashauri TAKUKURU kuendeleza juhudi zao zankuchunguza ubadhilifu wa fedha ndani ya vyama kwa kuanza na ripoti ya Bashiru ya Mwaka 2016 iliyoibua wizi wa kutisha wa mali za CCM na kisha kunyamaziwa bila hatua zozote kuchukuliwa wala wana CCM au Taifa kwa ujumla kutangaziwa hatma ya wezi hao walioko ndani ya Chama na katika serikali hadi sasa.

TAKUKURU wasipofanya hivyo waache kupoteza fedha umma kwa kuichunguza CHADEMA au MBOWE kwa msukumo wa kuchanganyikiwa kisiasa.

Sote tunajua kuwa CCM hawatakaa walale usingizi wakati CHADEMA ipo hai na Mbowe bado anapumua kama Mwenyekiti wa Chama. Sote tunajua pia kwamba Magufuli hatakaa ajiamini kuingia kwenye uchaguzi wowote mkuu kwa kushindana na mgombea yeyote toka CHADEMA. Sote tunajua pia kwamba serikali na vyombo vya dola hawawezi kuwa na raha kuiona CCM ikikaribia kukutana na CHADEMA imara kwa mara ya tatu mfululizo. Lakini pengine hofu kuu kuliko zote ni kwa CCM kumwona Mbowe akiipeleka CHADEMA katika round ya 3 ya uchaguzi mkuu akiwa kamanda wao asiye na bei, asiye panic wala kuendesha mambo kitoto.

Mbowe anaogopwa na CCM na serikali kuliko coronavirus au vikwazo vikubwa vya uchumi vinavyoinyemelea nchi.

TAKUKURU wamekurupushwa kujiunga kwenye mkakati wa hofu. Wanadhani watanzania wameisahau CCM na madudu yao ndani ya chama na katika serikali. Wanadhani watanzania wataaminishwa kirahisi tu kwamba leo ndani ya CHADEMA kuna ubadhilifu wa fedha wa kutisha kuliko upigaji wa enzi na enzi ndani ya CCM na serikali yake. Wamelishwa hofu ya Magufuli na sasa wanataka kusumbua watu hapa.

TAKUKURU wasipoanza na wizi mkubwa ndani ya CCM basi wasiisumbue CHADEMA na Mbowe. Watafute kitu kingine cha kuoneshea wasivyo na maana kwenye Taifa hili.
 
Hiyo TAKUKURU nayo imekuwa sawasawa na Jumuiya ya CCM.......

Yenyewe inafanya mambo kumpendezesha Jiwe
 
Ni vyema Takukuru wakasimamia majukumu yao kwa haki. Tuone michakato ikiendelea pande zote. JPM aliwahi lalamika na kuamua kuunda tume chini ya Bashiru ; Pia yapo malalamiko Watanzania mali za umma zilizohodhiwa na ccm mfano viwanja michezo.
 
Chama chako kimekwepa kodi wakati wa kununua gari. Jibu hoja hiyo acha maneno mengi hayasaidii.
 
Kwanini makamanda mmepanic kiasi hiki? Kabla ya takukuru kuitisha uchunguzi mlikuwa manajubasibu mitandaoni kwamba mna hati safi ya CAG. Sasa tatizo liko wapi kupinga uchunguzi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni mara ngapi CAG amebainisha matumizi mabaya ya serekali pamoja na vyama vingine vya siasa mbona sijaona takukuru wakichukua hatua stahiki tunajaribu kutengeneza taifa la ajabu sana karne hizi kweli mbona ni kama tutaendelea kuchelewa kupata maendeleo.

Kama tusipoamua kubadilika kwenye mifumo yetu kuendeshwa kisiasa kuna nchi zenye udikiteta ila wanafanya vizuri kuliko sisi. Mfano Uganda bunge linafanya vizuri kuisimamia Serekali mpaka unashanga ndomana mpaka leo tunakosa sukari wakati uganda wana viwanda vitano vikubwa na vidogo kumi na tano sisi ni Porojo tu.
 
Back
Top Bottom