CHADEMA, umati wa Jangwani si nguvu ya chama! Ni kuchoka kwa vijana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA, umati wa Jangwani si nguvu ya chama! Ni kuchoka kwa vijana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, May 27, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Nimepita jangwani na nikatulia kwenye Luninga yangu nikifuatilia hotuba kem kema nzuri zenye mvuto za viongozi wa CDM. Pamoja na kufurahishwa na mengi yaliyozungumwa, kuna mambo kadhaa ambayo ningependa njiyaseme:

  1. Ule umati kwa kiasi kikubwa ni wa vijana ambao wengi wanashauku kubwa ya mabadiliko, tena ya haraka maana ndoto zao hazilingani na hali halisi ya mambo. hawahawa ndio wanaoweza kuigeuka CDM iwapo haitatimiza matarajio yao. Wakipata mwingine mwenye kuwa na mvutop na hamasa, hawasiti kuelekea kwake!

  2. Nimekerwa na matumizi mabaya ya muda, ni vema waandaaji wakawa wanajua watu ambao hata kama sio wasemaji wakuu, wanapaswa kuandaliwa muda wa kutosha kutokana na hoja zao kuwa moto kama akina Mh Tundu Lisu. Kumlazimisha Mh Tundulisu kutumia dk 5 ukijua fika hoja zake zina mchango mzito tu na msukumo kwa yale mnayokusudia ni udhalilishaji kwani atakapotumia muda mwingi zaidi, mnaionekana poor kwenye time management. Ama sivyo muwe mna uhakika hahitaji muda mwingi kiasi hicho maana hawezi katisha hoja.

  3. Hamkuweza kuleta hamasa hasa katika kuvua gamba na kuvaa gwanda, hilo zoezi lingekuwa la kwanza mapema na Wasemaji wakuuu ndio wakamalizia kutoa hotuba.

  4. Nimefurahishwa sana na uhamasishaji wa kufungua matawi, ila, pamoja na kuwa hilo ni jambo muhimu kuliko yote, bado hamkulipa uzito wa kutosha na ufafanuzi unaoeleweka, kama mtizamaji ni rahisi kufikiri Matawi hayana utaratibu yanafunguliwa tu popote na kwa idadi ya watu wowote. Sawa si vema kuleta urasimu ila ni jambo ambalo mngelihamasisha vya kutosha na kutoa ufafanuzi wa jinsi matawi yanavyoweza kukipa nguvu chama, nadhani hilo hamlioni. Uhai wa Chama chochote ni matawi imara yanayochangia kwenye ngazi za juu, na si umati unao=hang out of structure. Mnahitaji huo mfumo kama mnakusudia kuendesha serikali pamoja na mambo mengine.

  Kila la kheri mnaleta changamoto nzuri kwa chama chetu cha CCM.
   
 2. P

  People JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mtazamo mbovu! Vijana na wananchi kwa ujumla kweli wamechoka na li chama lenu lenye mfumo mbovu.Kwa upande mwingine nguvu ya chama,ushawishi wa chama,mvuto wa chama,mfumo mzuri wa chama,sera nzuri za chama(CDM) ndizo zilizopelekea na bado zitapelekea vijana na hata wazee wengi kuhudhuria mikutano ya m4c.
   
 3. M

  MpendaCHADEMA Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chadema mwagia maji magamba yalainike!
   
 4. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Waambie CUF au NCCM Mageuzi waitishe mkutano Jangwani, angalia mahudhurio then uje useme ni kuchoka kwa vijana au Chadema ina Nguvu.
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Poor reasoning
   
 6. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  shule za kata@work
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kama ulikuwa mbele ya runinga na hukuelewa basi tukuombee tu. Hoja ya muda umechemsha. Mrema alisema atampunguzia dk 5 wala si kumpa dk5! Kadhalika kwa mazingira yale ni ngumu kama utakavyo. Hoja ya wahudhuriaji ni dhaifu sana. Nilikuwa frontline kabisa. Watu wanakwenda pale kwa mapenzi na si nyie mnaosuburia kwenye runinga. Umeme ungekatika ungepata muda wa kusema hayo? Suala la kufungua matawi mkiti alitoa maelezo na namba za simu kwa ajili ya maelekezo zaidi. Akazirudia tena na tena. We Profesa wa wapi?

  Si kila kitu ni cha kukosolewa kiholela tu maana yote uliyokosoa, mkuu majibu yake yalikuwa ndani yako kama ungeamua kuwa makini.
   
 8. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Ok. ok. ok....professor. Je nani kawachosha hao vijana?
  Ni nani hajawatimizia ndoto zao?
  Una ushahidi gani na kuchoka kwao?

  Mods: Inabidi sasa mfikirie kuwawekea nyinyiem jukwaa lao. Hawako ktk viwango stahiki kushiriki ligi hii!
   
 9. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Magamba hatuyataki full stop
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Researchers have found that low self-esteem and materialism are not just a correlation, but also a causal relationship where low self esteem increases materialism, and materialism can also create low self-esteem.

  Most of us want more income so we can consume more. Yet as societies become richer, they do not become happier.
  Statistically people have more things than they did 50 years ago.

  Soma zaidi: https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/269483-matatizo-ya-wana-chadema.html#post3941843
   
 11. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Professor pole niliskia ulilazwa india umesharudi?
  Au sio prof maji marefu? Maana post yako imekaa kimajimarefu majimarefu
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mkutano wa jana ulionyesha kwamba Chadema ni ya rika zote na jinsia zote japo vijana walikuwa wengi zaidi kama ilivyo hali halisi vijana na watoto ni zaidi ya asilimia sitini kwa hiyo katika hali ya kawaida watakuwa wengi

  Nilichojifunza kwenye eneo nililokuwa nimesimama nikisikiliza michango ya chini chini kutoka kwa wananchi ni kwamba sasa basi wote tuseme CCm bye bye wengi walikuwa wanasisitiza umuhimu wa kubadilisha watawala kwa sababu wanasema CCM wameishiwa uwezo ,wengi walikuwa wanasema hata aje nani ndani ya CCM kwa mfumo walionao hawawezi kuitoa nchi kwenye lindi la umaskini

  Nakubaliana na wewe swala la kuwaeleza wananchi jinsi bora ya kuanzisha matawi. na namna bora ya wananchi kuchangia juhudi za kukieneza chama
  Hamasa zilizokuwepo uwanjani watu wamenifurahisha kila aliyekuwepo pale alionyesha anajua amefuata nini
   
 13. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mwenye akili ya wastani tu anaweza kujua kati yako na profesa nani ana mtazamo mbovu. profesa amejitahidi kutoa 'positive criticism'. Mimi ni mwanachama wa CDM, nina umri zaidi ya miaka 50 na nilikuwepo Jangwani. Kwa haraka haraka wenye umri kama wangu walikuwa kama asilimia 5 tu. On one hand this is a good thing - CDM kinakubalika na kizazi kipya; but on the other hand it is a challenge - Will CDM meet their expectations. Most are in colleges and soon will be in streets hunting for jobs. Hivyo kama matarajio yao hayatatimizwa wanaweza kuigeka CDM. Mimi sioni ubovu wowote katika kauli hiyo. Maana sote wanaCDM tunaijua. Ni tahadhari ambayo tunapaswa kuifanyia kazi kutoka sasa kabla hatujaingia ikulu 2015.

  Shida ya muda ni kwamba walitaka watu wote walioko jukwaani waonekane kwenye luninga. Wangeweza kuwa wameanza saa 9 kwa salamu mbalimbali na kisha saa 10 wakaendelea na mambo mengine kama kuvua magamba, harakati za kufungua matawi, na baadaye hotuba. Hoja nyingine zote za mtoa post zinajitosheleza.

  Anayekubali kukosolewa ana maisha marefu. Kifo cha ccm ni kwa sababu ya kukataa hoja zinazoikosoa. Tusiruhusu upofu huo uingie CDM.
   
 14. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mungi, taratibu Mkuu ... Humu JF wewe ni mmojawapo ya watu ninaowaheshimu sana.

  Mimi naona mtoa mada ametoa mchango mzuri kama tutauangalia positively. Hapo hata hakusema juu ya wanawake kutokuwepo wengi. Mimi ni mwanaCDM na nilikuwepo Jangwani. Wanawake kadhaa wabunge waliopewa nafasi kusalimu waligusia suala la wanawake kujivua gamba. Hii ilitokana na uchache wao katika mahudhurio.
   
 15. M

  MR.SILVER JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmezoea semina za siku zima mtua anaongea masaa ...pangilia unachosema in 5min pitch ni muda wa kutosha sana ili kila mmoja aongee ukizingatia kila mmoja ana influence tofauti kwa watu.

  Si mnaona waoenda kuongeana wazee a dar es salaam masaa mengi point zakutafuta
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ule ulikuwa ni uigizaji na kila mmoja alipewa muda mchache aoneshe kipaji chake cha maigizo. Kwi kwi kwi teh teh teh.

  CSS - Chadema Star Search!

  Kipi zaidi ya maigizo kilichokuwepo pale, ipi ni hoja ya maana iliyo-ongelewa, sijaiona!
   
 17. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Profesa ni ukweli kuwa wanaoisupport wengi CDM ni vijana ambao una hofu kesho wanaweza kuigeuka CDM endapo matarajio yao hayatimizwa.

  Ni kweli lakini tiba ya hili ni ndogo, ni kuwapa ukweli wafuasi wako wa wapi ulioikuta nchi na kuweka wazi mipango yako ya kuwatoa hapo na kweli kufanikisha.

  Kama utafanikisha hakuna mtu ambaye atashindwa kuona juhudi zako na kukubali. Nadhani chuki kubwa ya CCM ni kukumbatia uovu na serikali yake kutowajibika.

  Serikali inayowajibika inaleta matumaini kwa wananchi.
   
 18. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Strategically it seems Professor was in good manner,but CDM must stick in a point to build the concrete of the party and ignore some pointless, then taking the good good point for the seek of party and Tanzanian.

  Watu ni kweli wamekata tamaa kwani hata Sir Issack Newton aliwahi kusema 'For every action and reactions are equal and opposite"sasa basi ni wakati wa CDM kutobweteka na kuvimba kichwa,watu wamekata tamaa na maisha hakuna mwanga mpya unaoonekana mbele yao zaid ya CDM,its there time to face challenges to distinguish between CDM and CCM.

  Na hakuna wakati CDM inatakiwa kufanya kazi kubwa kama sasa kwa kuonyesha kwa vitendo nguvu ya umma inaweza hata kufanya shughuli za kimaendeleo kwa kuwashirikisha katika shughuli mbalimbali za kujenga uchumi kivitendo kama kilivyokuwa TANU wakati wa mwanzo wa uhuru.Nuguvu hii isiishie kwenye Tahrir square only,itumike kuwa mobilize watu kujenga uchumi kwa nguvu zao na umoja wao ili ile dhana ya tumeanza na Mungu na tutamaliza na Mungu iwe na mashiko,kwani hata Mungu alisema asiye fanya kazi na asile.
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwani lazima uandike Kiingereza kama kinakupiga chenga?

  Mlianza na mungu yupi?
   
 20. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Great thinking!
   
Loading...