CHADEMA, umati wa Jangwani si nguvu ya chama! Ni kuchoka kwa vijana

Mwenye akili ya wastani tu anaweza kujua kati yako na profesa nani ana mtazamo mbovu. profesa amejitahidi kutoa 'positive criticism'. Mimi ni mwanachama wa CDM, nina umri zaidi ya miaka 50 na nilikuwepo Jangwani. Kwa haraka haraka wenye umri kama wangu walikuwa kama asilimia 5 tu. On one hand this is a good thing - CDM kinakubalika na kizazi kipya; but on the other hand it is a challenge - Will CDM meet their expectations. Most are in colleges and soon will be in streets hunting for jobs. Hivyo kama matarajio yao hayatatimizwa wanaweza kuigeka CDM. Mimi sioni ubovu wowote katika kauli hiyo. Maana sote wanaCDM tunaijua. Ni tahadhari ambayo tunapaswa kuifanyia kazi kutoka sasa kabla hatujaingia ikulu 2015.

Shida ya muda ni kwamba walitaka watu wote walioko jukwaani waonekane kwenye luninga. Wangeweza kuwa wameanza saa 9 kwa salamu mbalimbali na kisha saa 10 wakaendelea na mambo mengine kama kuvua magamba, harakati za kufungua matawi, na baadaye hotuba. Hoja nyingine zote za mtoa post zinajitosheleza.

Anayekubali kukosolewa ana maisha marefu. Kifo cha ccm ni kwa sababu ya kukataa hoja zinazoikosoa. Tusiruhusu upofu huo uingie CDM.

Sound like magamba on work!!
 
Ukitaka kupima nguvu za mlevi mwaga pombe yake, hasa anapokunywa! Tz kuna vyama zaidi ya 18, itisheni mkutana Jangwani, then mtapata jawabu kuwa, CDM ni ya wahuni, vijana au ya kikanda, au ni chama chenye matumaini kwa watz. Fanyeni utafiti kidogo tu, Ccm bila ya pilau na malori ya kusomba watu mahudhurio ya mikutano ni zero.
 
Nimepita jangwani na nikatulia kwenye Luninga yangu nikifuatilia hotuba kem kema nzuri zenye mvuto za viongozi wa CDM. Pamoja na kufurahishwa na mengi yaliyozungumwa, kuna mambo kadhaa ambayo ningependa njiyaseme:

1. Ule umati kwa kiasi kikubwa ni wa vijana ambao wengi wanashauku kubwa ya mabadiliko, tena ya haraka maana ndoto zao hazilingani na hali halisi ya mambo. hawahawa ndio wanaoweza kuigeuka CDM iwapo haitatimiza matarajio yao. Wakipata mwingine mwenye kuwa na mvutop na hamasa, hawasiti kuelekea kwake!


Kila la kheri mnaleta changamoto nzuri kwa chama chetu cha CCM.

Sioni chenye kutia mashaka hapo kwani CDM wanafahamu kuwa vijana wanahitaji mabadiliko, na ni haki yao kumuondoa asiyetimiza matakwa yao. Sasa sioni unaonya nini ktk hilo.

CDM haijaja kuleta changamoto, inaleta serikali mbadala.
 
Waambie CUF au NCCM Mageuzi waitishe mkutano Jangwani, angalia mahudhurio then uje useme ni kuchoka kwa vijana au Chadema ina Nguvu.

sio cuf na nccm wanaopashindwa jangwani hata hao ccm hawapawezi sana sana watapeleka mabus mkuranga,kibaha,bagamoyo,kisarawe na kwingineke ili kuleta watu jangwani kwani wewe hukumbuki,bila hivyo hawawezi
 
Mungi, taratibu Mkuu ... Humu JF wewe ni mmojawapo ya watu ninaowaheshimu sana.

Mimi naona mtoa mada ametoa mchango mzuri kama tutauangalia positively. Hapo hata hakusema juu ya wanawake kutokuwepo wengi. Mimi ni mwanaCDM na nilikuwepo Jangwani. Wanawake kadhaa wabunge waliopewa nafasi kusalimu waligusia suala la wanawake kujivua gamba. Hii ilitokana na uchache wao katika mahudhurio.

wanawake walimwogopa kova ndio maana walikuwa wachache
 
Sioni unachotaka kutuaminisha hapa kwenye suala la ufunguaji matawi..
Mbowe amesema wanachama 30 wanaweza kufungua tawi dogo....na kama matawi yakifika 10 wanaweza kufungua tawi kubwa....na akaenda mbali zaidi kwa kutoa namba za viongozi wa kuwasiliana nao katika shughuli za ufunguaji matawi....hapa hujaelewa nini au unaogopa matawi yatakavyochipuka?
 
Ule ulikuwa ni uigizaji na kila mmoja alipewa muda mchache aoneshe kipaji chake cha maigizo. Kwi kwi kwi teh teh teh.

CSS - Chadema Star Search!

Kipi zaidi ya maigizo kilichokuwepo pale, ipi ni hoja ya maana iliyo-ongelewa, sijaiona!

Hoja ili ionekane ya maana inategemea pia uwezo wa mtu katika kufikiri na kuchanganua mambo. Kama uwezo wako wa kufikiri ni mdogo hutaelewa wala kuiona hoja ambayo wenzio wanaiona.
 
Sawa umewasilisha vema Prof!

Sasa unadhani ni sahihi kwa chama kwamba shughuli ya kapaumbele iwe kuwavua watu magamba? Kweli?
Pia nilikuwepo jangwani, na nilipenda zoezi lile kuwekwa mwisho sababu ilituma ujumbe kwa Nape kuwa hyo sio agenda ya chama kama anavyohaha kulalama kwenye vyombo vya habari.

Pia kwa mujibu wa tangazo la mkutano ilitangazwa kuwa agenda kuu ni Katiba na kujadili hali ya Maisha.
Unapozungumzia suala la mkutano kuwahi kuanza inatakiwa pia ukumbuke kwenye kupanga timing kuna masuala kama mda wa watu kupatikana, hvyo ni lazima uwekwe muda ambao watakuwa wametoka kwenye shughuli zao sababu ule ni mkutano watanzania watu wazima ambapo kuna wafanyakazi, wafanyabiashara na wanafunzi hvyo ni lazima uzingatie muda kuwanasa wote hao, pia kuna suala la hali ya hewa ya eneo husika, mfano kwa dsm hapa ilikadiriwa kutakuwa na jua kali sana ukifuatilia toka wiki ilipoanza (japo jana mvua hatujui ilitokea wapi)
Sasa mkuu na jua hili la bongo hapa halafu uitishe mkutano saa nane kweli??

Mi siamini kama vijana watanzania tunaka CDM iigeuze Tz kuwa Ulaya kwa miaka 5, ila ninachojua watz wanataka kushiriki kwenye ujenzi wa nchi yao huku wakielewa masuala yote ya msingi ya taifa lao.
Na hlo vijana wanaambiwa kwenye mikutano kuwa 2015 baada ya kuiweka CDM madarakani hautakuwa mda wa kusheherekea bali kazi ya kujenga taifa lao ndio inaanza!

Mi nadhani mkutano wa jana ulikuwa sawa maeneo mengi japo ni muhimu kukosoa kama unaona kuna pa kukosoa sababu tunakubaliana hamna mkamilifu miongoni mwetu.
 
Researchers have found that low self-esteem and materialism are not just a correlation, but also a causal relationship where low self esteem increases materialism, and materialism can also create low self-esteem.

Most of us want more income so we can consume more. Yet as societies become richer, they do not become happier.
Statistically people have more things than they did 50 years ago.

Soma zaidi: https://www.jamiiforums.com/habari-...483-matatizo-ya-wana-chadema.html#post3941843

What has your dying party CCM delivered to that end. I realy respect the opinion of Profesa it is well intended. I for one would have been satisfied with Tundu Lissu using the whole meeting to expound on the issues he highlidghted.

As for you Mr. Ribosome assure yourself that if you do not notice the change now, you will regret when the changes sweep you away to an unknown destination.
 
Umati uliojitokeza jana pale jangwani ulichangiwa na matangazo kupitia vyombo vya habari hilo halina ubishi na sidhani kama ule umati ulikuja kusikiliza sera mbadala
 
Ule haukuwa mkutano wa kutangaza sera mbadala, ulikuwa kwa ajili ya maoni kwa katiba mpya. Either way, ulitaka watu wajue kwa njia zipi?
 
Hahahahahahaha!

Makopo bana! Yaani mnafikiri weeee hampati jibu!

Mara sijui mill 500 zimenunua watu,

Mara promosheni,

Mara ......

Mimi nasema hapa kila siku Hakuna kuionea huruma magamba!

Endeleeni kutokwa mapovu tu na Nape wenu badala ya kuisimamia Serikali itimize majukumu yake!
 
Umati uliojitokeza jana pale jangwani ulichangiwa na matangazo kupitia vyombo vya habari hilo halina ubishi na sidhani kama ule umati ulikuja kusikiliza sera mbadala

duh kuanzisha thread tu kunahitaji mtu awe na akili zaidi ya hizi, sasa nashangaa wewe umewezaje, au kuna mtu kakuanzishia?
 
Back
Top Bottom