CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,537
2,000
Naomba tuulizane, je tunavyoikomalia Ukawa na kuichambua chambua kama mchicha au mchele tunawaelewa wananchi wengi wapiga kura?

Maana kama ni kuichambua CCM, tumeichambua miaka nenda rudi na kila mwaka bila kujali scandal gani, umasikini wa kiwango cha medali ya dhahabu olimpiki, bado Watanzania waliendelea kukipigia kura CCM na CCM wameendelea kutudharau sisi "wachambuzi"!

What if Lowassa na wenzake nao wameibaini formula ya ushindi ya CCM? maana wakati tunahoji kuambiwa tukasome hotuba na ilani kwenye website ya Chadema, CCM wametoa PDF na ilani ya kurasa karibu 230 na hatuhoji ni nani huyo mwananchi mpiga kura wa kijijini au hata mjini atakayekaa chini kupitia kurasa 230 zenye majedwali na misamiati migumu ambayo haielewi?

Hatujiulizi ni vipi wananchi hawajuuliza ili kupata ufafanuzi wa hizo Milioni 50 kwa kila kijiji kama Mama Samia alivyosema, lakini leo tunamhoji Lowassa kusomesha elimu bure?

Nikiliangalia hilo la Shilingi Milioni 50 na lilivyopokelewa kwa shangwe (kwanza hiyo ni ahadi ya rushwa kupata kura), je shilingi hizi milioni 50 ni za kazi gani katika kijiji? ni wananchi kugawiwa fedha? ni za kununulia mabati ya shule? ni ya kununua magodoro ya zahanati? ni ya kuchimba mifereji? ni ya kununua ng'ombe wa mbegu? Hizi fedha ni za nini? je fedha zinazotolewa kila mwaka kwa shughuli za maendeleo na matumizi Wilayani haziendi huku vijijini?

Nikiongelea hili la Milioni 50 na rafiki yangu Mzee Mwanakijiji, akanikumbusha Mabilioni ya JK alipoingia madarakani na zile fedha za community fund, je uwiano wa kijiji chenye watu 100 na kijiji chenye watu 1,500 utapimwa vipi ikiwa kila kijiji kitapokea Milioni 50?

Nauleta huu mfano wa Milioni hamsini na ulivyopokelewa na wananchi kwa matumaini na vifijo kusema: Jamii ya Watanzania si wengi wanachambua mambo kwa kina na hata kuona mapungufu ya wazi.

Je Masha aliposema ameonewa na polisi na kuwekwa ndani kwa kuhoji, si ndivyo 50% ya walioko magerezani na jela wameswekwa kibabebabe? Hata la Babu Seiya na Mashehe si wananchi walilipuka kwa nguvu kabisa na limekuwa gumzo?

Sasa najiuliza ni nini sisi "wachambuzi" hatukioni miaka yote na CCM wanaendelea kujiamini hata kudiriki kuita wanaoihoji na kuipinga kuwa ni Wapumbavu na Malofa?

Nikikumbuka 1995 jinsi Mtikila na magabacholi au Mrema na mkwara wa kupambana na Rushwa akiingia ikulu na kisha wakaambulia kura za kubahatishabahatisha, je ni kitu gani wapiga kura wa Tanzania wanakiangalia kutoka kwa mgombea?

Jana na leo, Mwakyembe na Sitta wameudanganya umma tena kwa swala la Richmond huku wengine tunajua wao wawili walikuwa na uwezo mkubwa kuilazimisha Serikali kama Bunge kufuta mkataba huo mara moja na kuokoa mabilioni tuliyoyalipa kama Capacity Charge kwa Richmond, baadaye Dowans na sasa Symbion. Ikiwa waliweza mlazimisha Waziri Mkuu kujiuzulu, walishindwa nini kuilazimisha Serikali kufuta huo mkataba na wote walijua gharama tuliyoipata na IPTL na ubovu wa mkataba wa Richmond?

Hivyo lazima kuna kitu ambacho hatukielewi kwa kuwa tunapima na kuchambua kila anachokula bata na tunakuwa wepesi kutahamaki na kuonyesha mshangao huku Watanzania wanaimba korogakoroga zungusha zungusha Pipoz Pawa!

Maneno yako yanafikirisha sana na ni ukweli ambao ni mchungu.

Sisi tulio humu jamvini twaweza kuchambua kila linaloendelea kwenye ulingo wa siasa lakini bado hatuwakilishi asilimia kubwa ya wapiga kura ambao wako mtaani na vijijini. Ndio hawa hawa ambao waliipa kura kuirejesha CCM madarakani 2010 pamoja na kashfa lukuki zilizokuwapo, ndio hawa hawa waliwarejesha majimboni wabunge watuhumiwa wa kashfa za ufisadi mwaka 2010 na hata sasa wamewapitisha kwenye kura za maoni!

Kuna wakati huwa najiuliza kama ni kweli kwa siasa zetu za kiafrika hizi hususan hapa Tanzania chama kinaweza kushinda uchaguzi kwa sera pekee? Najiuliza kama wananchi wanaohudhuria mikutano ya kampeni wanaenda kusikiliza seraza vyama na wagombea ili kuzichambua au wanaenda kusikiliza porojo, vijembe na tambo za wagombea majukwaani? Nini kinachowavutia?

Ili kuweza kuelewa haya lazima tufike mahali tufanye tathmini juu ya mindset ya watanzania inapofikia masuala ya siasa na uchaguzi... sababu hiki ndicho CCM wanakitumia kujipatia ushindi miaka nenda rudi. Ndio maana tunasikia kauli hizi "Mchagueni Rev Kishoka sababu ana MVUTO na ANAKUBALIKA"... lakini swali ni kwamba mvuto na kukubalika vinahusiana vipi na sera?? Lakini mwisho wa siku ndicho wananchi wanakikubali!

Watanzania tumekuwa wasahaulifu mno na tunapokea mambo bila kuhoji ndio maana watu kama kina Mwakyembe wanaweza kusimama leo jukwaani kusema ati Lowassa anaweza kushtakiwa kuhusu Richmond na akapigiwa vigelegele! Wala hatumhoji kwa nini aliamua kuficha madudu mengine kwenye ile ripoti yake ili kuisitiri serikali ya chama chake isianguke! Na hii ndio mindset ya watanzania ninayoiongelea...

Mwanzoni UKAWA walipoamua kumsimamisha Lowasa nilishtuka na sikuelewa kwa nini. Lakini baada ya kuona mwitikio kwenye mikutano ya kampeni sasa naanza kuelewa. UKAWA safari hii wameamua kukalibiana na CCM "using their own game"
 
Alinda

Platinum Member
Jun 26, 2008
1,690
2,000
Alinda ndg yangu,
nimesikia tetesi mitandaoni,kesho Dr.Slaa anamwaga manyanga, sasa hii itakua pigo takatifu na demage kubwa sana kwa UKAWA na sijui watafanyaje iki kuniokoa, naombea tu atumie busara, maana kwa namna yoyote ile atarudisha nyuma mipango ya UKAWA kwa kiwango kikubwa mno na mambo nayaona yakienda mrama, only God knws wht willhappen after his damage, kiuhakika wajipange sas akina Mbowe.

Ni kweli kuwa leo mzee wetu anataka kuongea neno.

Kama ulitusoma huko nyuma utaona kuwa tulitoa tahadhari juu ya hali kama hii, ila kwa bahati mbaya hatukusikilizwa au tulisikilizwa na maoni yetu hayakuchukuliwa.

Na kibaya zaidi tuko katika wakati mgumu kama Ukawa/wapinzani hivyo kila kura ni lazima tuipiganie kwani ni muhimu kwetu Hivyo basi inapokea Dr. Slaa kukaa pembeni ni pigo na ni upweke mkubwa.

Lakini ndivyo hivyo Dr. Slaa ni mtu huru na anachofanya ni haki yake, hatuwezi kumlazimisha kuwa nasi iwepo yeye mwenye anaona kuwa kuwepo katika team hasiyo na imani nayo ni unafiki.

Chakufanya ni kumtakia safari njema na pia kumshukuru kwa kufikisha Chadema hapa ilipo maana bila yeye sidhani hata kama Lowassa angetimkia Chadema.

Na kwetu sisi wanamegeuzi ni wakati wa kushikamana kuliko wakati mwingine wowote ule maana "hiki kikombe ni lazima kukinywa" iwe kwa kushinda au kwa kushindwa.. Na siku zote umoja ni ushindi na kwa pamoja tutashinda!

Asante Dr. Slaa tutakukumbuka daima. Ila umetuacha wapweke
 
Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,537
2,000
Inafurahisha kuona sasa hivi sasa machoni pa CCM Dr Slaa anaonekana kama kiongozi msafi na muadilifu aliyestahili kupeperusha bendera ya UKAWA badala ya fisadi Lowassa! Ni Slaa huyu huyu ambaye alishambuliwa kwa kila aina ya vijembe, kejeli na matusi kibao... akaitwa Padre, Mzinzi na mwizi wa mke wa mtu, Kibabu, Kakimbia upadre baada ya kukwapua pesa za TEC n.k.

Leo CCM hawa hawa wanampamba kwa kila meneno matamu mzee wa watu kwamba ndie kiongozi anayefaa!
 
Alinda

Platinum Member
Jun 26, 2008
1,690
2,000
Maneno yako yanafikirisha sana na ni ukweli ambao ni mchungu.

Sisi tulio humu jamvini twaweza kuchambua kila linaloendelea kwenye ulingo wa siasa lakini bado hatuwakilishi asilimia kubwa ya wapiga kura ambao wako mtaani na vijijini. Ndio hawa hawa ambao waliipa kura kuirejesha CCM madarakani 2010 pamoja na kashfa lukuki zilizokuwapo, ndio hawa hawa waliwarejesha majimboni wabunge watuhumiwa wa kashfa za ufisadi mwaka 2010 na hata sasa wamewapitisha kwenye kura za maoni!

Kuna wakati huwa najiuliza kama ni kweli kwa siasa zetu za kiafrika hizi hususan hapa Tanzania chama kinaweza kushinda uchaguzi kwa sera pekee? Najiuliza kama wananchi wanaohudhuria mikutano ya kampeni wanaenda kusikiliza seraza vyama na wagombea ili kuzichambua au wanaenda kusikiliza porojo, vijembe na tambo za wagombea majukwaani? Nini kinachowavutia?

Ili kuweza kuelewa haya lazima tufike mahali tufanye tathmini juu ya mindset ya watanzania inapofikia masuala ya siasa na uchaguzi... sababu hiki ndicho CCM wanakitumia kujipatia ushindi miaka nenda rudi. Ndio maana tunasikia kauli hizi "Mchagueni Rev Kishoka sababu ana MVUTO na ANAKUBALIKA"... lakini swali ni kwamba mvuto na kukubalika vinahusiana vipi na sera?? Lakini mwisho wa siku ndicho wananchi wanakikubali!

Watanzania tumekuwa wasahaulifu mno na tunapokea mambo bila kuhoji ndio maana watu kama kina Mwakyembe wanaweza kusimama leo jukwaani kusema ati Lowassa anaweza kushtakiwa kuhusu Richmond na akapigiwa vigelegele! Wala hatumhoji kwa nini aliamua kuficha madudu mengine kwenye ile ripoti yake ili kuisitiri serikali ya chama chake isianguke! Na hii ndio mindset ya watanzania ninayoiongelea...

Mwanzoni UKAWA walipoamua kumsimamisha Lowasa nilishtuka na sikuelewa kwa nini. Lakini baada ya kuona mwitikio kwenye mikutano ya kampeni sasa naanza kuelewa. UKAWA safari hii wameamua kukalibiana na CCM "using their own game"

Watanzania tuna tatizo na nafikri tatizo linatokana na elimu yetu, mashuleni tunafundishwa kukariri tu, hatufundishwi kuhoji na pale Mwl anapoulizwa swali basi hujibu kwa kumkatisha mtoto tamaa.

Majumbani nako ni hivyo hatuwafundishi watoto wetu ujasiri, hatuwafundishi kuhoji, unaweza kuja nyumbani ukamwambia mtoto wako tafuta fimbo nikuchape na mtoto akafanya hivyo bila kuhoji "kwani kosa langu ni lipi? hatufundishi watoto wetu kuwa na "confidence" kitu ambacho ni muhimu sana katika maisha yetu.

Tuna wafundisha watoto wetu heshima za uoga si heshima na matokeo yake ndio unapata taifa kama la watanzani, taifa la wapiga makofi, taifa la wapiga vigeregere, taifa lisilohoji, taifa ambalo watu wake hawafahamu haki zao na ili taifa haliko tayari kuwapa elimu watu wao ili wafahamu haki zao kwa taifa ili viongozi ni miungu watu, viongozi hawakosei, na ndio maana kiongozi anaaweza kusimama na kusema "kama kula nyasi mtakula ila ndege ya rais lazima tununue" na huyu akashangiliwa tena kashangiliwa na viongozi ambao ni wabunge. au kaporomosha matusi kama Mkapa na kashangiliwa na watu wale wale anatukana.

Kama wewe ni mzazi au mzazi mtarajiwa bado hujachelewa mfundishe mwanao kuhoji, ujasiri, hasiwe muoga wa kutetea haki zake na nk ili huyu mtoto hasipate viongozi wa kunyanyasa kama tunavyonyanyasika sisi wazazi wake.

Hebu fikiria
Sitta anasema Lowassa ni fisadi wakati bunge la katiba limeisha majuzi alichokifanya sote tunafahamu, zile pesa za walalahoi zilizokuwa zilipe wabunge wa Ukawa hazijulikani zilipo, kuna swala la mabehewa mabovu(rejea Sumaye) yenye thamani ya bil.220 hakuna aliyechukuliwa hatua, kuna swala la jengo la spika alilojenga katika jimbon lenye thamani ya mil.500 wakati huo watoto wa shule katika jimbo lake hawana hata madawati, kuna wagonjwa wanaokosa madawa, kuna wazazi wanakwenda kujifunga na ndoo za maji au nyembe, kuna ukosefu wa maji safi jimboni kwake lakini kwake kitu kilichokuwa cha muhimu ni ofisi ya spika tena ni ofisi yake si ya serikali halafu huyu anasimama majukwaani na kutamba yeye ni msafi na watu wanapiga vigeregere kweli??? leo hii huyu mtu ni

Mafuguli tunayeambiwa ni mchapakazi na msafi kauza nyumba za serikali kwa ndugu zake, bil.265 zimepoteka katka wizara yake ya ujezi na hakuna maelezo, katika wizara ya ujezi serikali (yaani mimi na wewe) tunadaiwa tril.1.2 wakati huo bil.900 ni faidia kutokana na kuchelewesha kulipa makandarasi (hapo bil.265 zimepotea) huyu mtu ndio tunaambiwa ni msafi na watu wanashangilia. Hivi kweli hizi ni akili za kawaida au kuna kitu tulikosea kama taifa?
 
Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,537
2,000
Kama kuna kauli inanichosha ya wanasiasa ni hii ya kusema "nina nyaraka na nyingine sitazitoa hapa"

Unazihifadhi ili iweje? Kwa manufaa ya nani? Kwa nini asianike kila kitu hadharani wananchi waamue wenyewe? Hayo yanayofichwa yanafichwa kwa manufaa ya nani?
 
Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,422
2,000
Ngoja nitulize kichwa nitarudi kujadili.. Ila siasa kwa Tanzania ni ngumu jamani..CCM wapo tayari kutumia njia yeyote ile kuleta mgawanyiko.. Katika maongezi ya Dr. Slaa kuna mgawanyiko aliyougusia dah kweli tusiwaamini wanasiasa by Zitto Kabwe

Ukweli anaouzungumza mwanasiasa ni salamu tu mkuu....

Binafsi sikuwahi kutegemea kama Lowassa atakuja kuwa mwana CHADEMA kwa ghafla...Hasa nikirejea kauli za Lema..Slaa...Mnyika..Mbowe na Sugu kuhusu Lowassa
 
Azimio Jipya

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
3,364
1,195
Miezi michache iliyopita hakuna mtu angeweza kwa kutumia akili timamu kuja na analysis yenye kueleza kinachotokea kwenye siasa za Tanzania leo hii. Nani angeweza kuja na analysis ambayo ingemuweka Membe, Magufuli, Lowasa, Dr Slaa, Sumaye na Prof Lipumba Hapo walipo sasa.

Pia ni vigumu kabisa kwa kutumia ujuzi wowote unaopatikana kwenye akili zetu kutabiri baada ya wiki tatu nini kitakuwa kinajiri ndani ya siasa za Tanzania.

Dr Slaa leo kakamilisha kile kisichotabirika kwa siasa za uchaguzi wa mwaka huu.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,959

Mwanasiasa mmoja wa Uingereza aliwahi kusema 'siku moja ya siasa ni muda mrefu sana'

Pamoja na unayosema, kuna jambo moja umesahau. Mbona mengi tuliyoongea hapa yanatokea sasa hivi?

Kwasisi wengine 'maandishi yanatimia'

Dr Slaa ametumia haki yake ya kujieleza. Hakuwa na njia nyingine bali kujieleza tu ili abaki na kile anachosema ni credibility. Ameeleza mengi na ana haki hiyo kama walivyo na haki wengine kwa upande mwingine

Tunazidi kupata undani wa nini kilitokea na kwanini.

Tunaweza kusema kwa ufupi, hii ni collateral and colossal damage ya kiwango kikubwa sana kwa UKAWA

Yapo mengi sana yasiyoonekana, inatosha kusema kwa ufupi hayo
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,144
2,000
Nguruvi3,

..hivi mbona mambo haya hayatokei CCM?

..yaani CCM wanaweza kufanya chochote, kwa yeyote, na hakuna mtu wa kuleta ubishi-ubishi.

..kuna mtu kama Salim Salim. kwa jinsi alivyochafuliwa ungetegemea angemwaga mboga na ugali kama alivyofanya Dr.Slaa. Au, Mzee Malecela alivyokata bila maelezo ya kuridhisha.

..Kwanini CCM wanaonekana kuwa wavumilivu na watiifu kwa chama chao, kuliko hawa walioko vyama vya upinzani?

cc Mkandara, betlehem, Mzee Mwanakijiji, Alinda, Mwalimu
 
Last edited by a moderator:

Alinda

Platinum Member
Jun 26, 2008
1,690
2,000
Ukweli anaouzungumza mwanasiasa ni salamu tu mkuu....

Binafsi sikuwahi kutegemea kama Lowassa atakuja kuwa mwana CHADEMA kwa ghafla...Hasa nikirejea kauli za Lema..Slaa...Mnyika..Mbowe na Sugu kuhusu Lowassa

Hizo ndizo siasa za Tanzania.. Hivi ulifkiri kuwa leo hii Dr. Slaa angekuwa hero wa CCM? kuna mtu mbaya aliyekuwa upinzani kama Dr. Slaa? yako wapi? leo Dr. Slaa anakuja na propogada za udini? hivi ndo huyu Dr. Slaa aliyekuwa anasimangwa kuwa ni padre? Siasa za Tanzania ni mgumu jamani.
 
Alinda

Platinum Member
Jun 26, 2008
1,690
2,000
Nguruvi3,

..hivi mbona mambo haya hayatokei CCM?

..yaani CCM wanaweza kufanya chochote, kwa yeyote, na hakuna mtu wa kuleta ubishi-ubishi.

..kuna mtu kama Salim Salim. kwa jinsi alivyochafuliwa ungetegemea angemwaga mboga na ugali kama alivyofanya Dr.Slaa. Au, Mzee Malecela alivyokata bila maelezo ya kuridhisha.

..Kwanini CCM wanaonekana kuwa wavumilivu na watiifu kwa chama chao, kuliko hawa walioko vyama vya upinzani?

cc Mkandara, betlehem, Mzee Mwanakijiji, Alinda, Mwalimu

CCM wanakaa kimya maana kule kuna ulaji.. akiropoka tu ndo mirija yake yote ya kunyonya wanyonge inakuwa imekatwa.. yuko wapi Jaji Warioba aliyesimangwa usiku na mchana si ulimuona yuko jangwani?

Si ulimsikia Dr. Nchimbi analalamika kuhusu majina ya mfukoni? au si ulisikia Prof. Mwandosya? wametulia kutunza vitumbua vyao wakiwa na imani kuwa watakumbukwa. Lakini tukija kwa wapinzani ni tofauti maana hawa hawana cha kupoteza..

Kama umemsikia vizuri Dr. Slaa amesema kuwa alikuwa mmoja wa watu waliomleta Lowassa Chadema .. alipigiwa simu na Gwajima na yeye akasema mpaka aongee na Mwenyekiti hivyo utaona Lowassa alitoka kwa Dr. Slaa si kwa Mbowe kama tulivyokuwa tunaaminishwa..
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,758
2,000
.....

Shida ya Dr. Slaa si ufasadi wa Lowassa shida yake ilikuwa ya wabunge 50 aliyosema hivyo kama angeleta wabunge 50 basi leo hii angekuwa anakula "tapishi lake" and after all hivi baada ya miaka 8 bado kunakufa na Richmond na kuacha Dowans na Escrow??
Mkuu za siku tele. Bila kupoteza muda, najikita kwenye hiyo redbold.

Nimemsikiliza Dr. Slaa, toka anaanza mpaka anamaliza kujibu maswali. Leo sikutaka kuhadithiwa wala kuwekekewa clips zilizokatwa katwa, ilinifanye tathimini sahihi.

Nadhani si kweli kusema Dr. Slaa hakuwa na shida na ufisadi wa Lowassa. Ninadhani hivyo kwa sababu wakati anaanza kutoa maelezo juu ya kumkaribisha Lowassa alitoa masharti ya kimsingi ambayo alitaka Lowassa ayatekeleze. Baadhi ya masharti hayo ni haya:

1. Lowassa atamke hadharani kuwa ameachana na CCM
2. Lowassa ajibu tuhuma hadharani tena kinagaubaga kwa kusema wazi nani alihusika na Richmond na kashfa nyingine zianzomuhusu yeye Lowassa (Badala ya kusema mwenye ushahidi apeleke mahakamani ama mfunge midomo. Pia suala mahakamani haliwezekani kwa raia wa kawaida , Dr Slaa kasema, kesi za jinai ni serikali ndiyo ufungua mashitaka)
3. Akisha maliza kujisafisha (Lowassa), atangaze anaamia chama gani(Chadema ama chama kingine!);
4. na kisha kama ameamua kuamia chadema, basi chama(Chadema) kiamue kumpokea ama la...!Baada ya kujiridhisha kama Lowassa ni Asset kisiasa(atakuja na viongozi na wabunge wa CCM ambao nao watafuata utaratibu wa 1-3 hapo juu) ama ni Liability kisiasa.

Hivyo nadhani Mkuu, Alinda, si sahihi kumuhisi Dr. Slaa hivyo(redbold).

Binafsi, nadhani kwa kiasi fulani Dr. Slaa alikuwa nafanya siasa sahihi zisizo za kilaghai (siasa za ukweli). Siasa zisizo za kilaghai ndizo zilizonivutia kufatilia maadishi mengi ya Nguruvi3, ya kwako(Alinda) na wengineo hapa jukwaani.

Nadhani kwa leo Dr. Slaa kazitendea haki siasa nilizoziamini na ninazozidi kuziamini yaani siasa za ukweli na wala si siasa za kitapeli.

Mapambano bado yanaendelea kutafuta na kisha kuupata ukombozi wa kweli kwa kufuata siasa za ukweli.

-TUJITEGEMEE.
 
Nimekupa mkuu..na nime"edi" hapo.. shukurani kwa maelezo yako...

Kama umemsikliza vizuri hivi ameongea nini kuhusu "udini" maana mie nilikuwa nafatilia update za watu wa hapa JF. Inawezekana kuna upotoshaji wa aina fulani..
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,758
2,000
..... hivi baada ya miaka 8 bado kunakufa na Richmond na kuacha Dowans na Escrow??

Katika hili naweza kudhani kuwa Dr. Slaa alikuja kueleza ukimya wake baada ya Lowassa kujiunga Chadema. Hiyo ndiyo hasa ilikuwa maudhui na aina ya dhima ya kuitisha mkutano wa leo na waandishi wa habari. Hakuwa pale kufanya kampeni wala kuchambua viongozi wote wa siasa wa nchi hii. Mkutano wake ulilenga kueleza kwa nini alikaa kimya. na walomfanya akae kimya ni viongozi wenzake ndani ya Chadema kwa kukubali mtu mwenye tuhumua za Richmond tena ambaye yeye binafsi alimtangaza hadharani kuwa ni fisadi hiyo 2008. Kwa akili ya kawaida kumkaribisha mtu huyu ilibidi apitie kwenye chujio la masharti kadhaa(hasa namba 3. kwenye post 395 ya uzi huu). Ni Lowassa ndiye aliyekuwa kiini cha yeye kukaa kimya. Kwa maana hiyo, mkutano wake wa leo lazima ungejikita kuelezea kilichotokea na sifa za wale waliosababisha akae kimya.

Escrow....haikuwa kiini cha yeye kukaa kimya...!

Mimi ndivyo nilivyomuelewa.
 
Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,422
2,000
Hizo ndizo siasa za Tanzania.. Hivi ulifkiri kuwa leo hii Dr. Slaa angekuwa hero wa CCM? kuna mtu mbaya aliyekuwa upinzani kama Dr. Slaa? yako wapi? leo Dr. Slaa anakuja na propogada za udini? hivi ndo huyu Dr. Slaa aliyekuwa anasimangwa kuwa ni padre? Siasa za Tanzania ni mgumu jamani.

Swali la msingi ni Je, Lowassa ni Asset ama Liability kwa CHADEMA??
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,758
2,000
Nimekupa mkuu..na nime"edi" hapo.. shukurani kwa maelezo yako...

Kama umemsikliza vizuri hivi ameongea nini kuhusu "udini" maana mie nilikuwa nafatilia update za watu wa hapa JF. Inawezekana kuna upotoshaji wa aina fulani..

Kuhusu udini kausemea, lakini hasa kajikita zaidi kwenye maadili ya viongozi wa dini. Amesema alielezwa na 'mshenga' .... kuwa kunabaadhi ya maaskofu wa maadhehebu ya kikristo(katholiko likiwemo) wamehongwa na 'wanasiasa' kuanzia kati ya mil.50 na kuendelea. Akamalizia kwa kusema kama maelezo yale (ya mshenga) yalikuwa ya kweli amesikitika sana.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,959
2,000
Kuhusu udini kausemea, lakini hasa kajikita zaidi kwenye maadili ya viongozi wa dini. Amesema alielezwa na 'mshenga' .... kuwa kunabaadhi ya maaskofu wa maadhehebu ya kikristo(katholiko likiwemo) wamehongwa na 'wanasiasa' kuanzia kati ya mil.50 na kuendelea. Akamalizia kwa kusema kama maelezo yale (ya mshenga) yalikuwa ya kweli amesikitika sana.
Mkuu katika bandiko 2015-391 hapo juu nilisema naishia pale makusudi kabisa. Ukisoma vizuri nimeandika 'collateral and colossal damage' naomba nifafanunue

Collateral damage ni uharibu usiokusudiwa. Kwa mfano, ndege inaposhambulia askari , mabomu yakaangusha nyumba raia wakafa huo ndio mfano wake.

colossal damage ni uharibu mkubwa sana, wa kishindo.

Kilichotokea katika hotuba ya Dr Slaa ni vyote viwili. Lakini collateral damage ni kubwa sana kuliko watu wanavyoona

Katika nyakati hizi za uchaguzi kila kitu kinaangaliwa kutoka angel tofauti na si kila mtu atakuwa na muda au wasaa wa kutafuta ukweli. Habari zinakuwa sensitive kuliko inavyodhaniwa

Kwa mfano, tumesikia mtu akisema Lowassa hakwenda Ludewa kwasababu ya afya. Huo unaweza kuwa uongo. Katika nyakati hizi wapo watakaounganisha dot zisizohusiana na kupata ukweli kutoka katika uongo. Wapo watakaofanya spinning kupata maana waliyokusudia

Kwa hili la Dr Slaa na narudia tena, ana haki ya kujieleza kama wengine, alichosema kuhusu udini anaouzungumzia Alinda ni kibaya. Ni kibaya si kwasababu hakupaswa kusema, bali alipaswa kusema akiwa na uhakika.

Kwa maelezo yako mstari wa mwisho unasema ' kama aliyoelezwa ni ukweli, alikitika sana'

Maana yake hakuwa na uhakika, na busara ingemlazimu akae kimya. Kwa dhamana yake katika umma na 'credibility' anayosema kutoa kauli kama hiyo haikuwa sahihi.

Narudia haikuwa sahihi kwasababu hakupata ukweli, kama wapo wanaotafuta ukweli kupitia hisia zake, basi watakuwa wameupata
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom