CHADEMA/UKAWA: Uwekezaji usiotabirika

Sehemu ya I

UKAWA

MAAFA YA KISIASA VIWANJA VYA JANGWANI

Tunaposema maafa ya kisiasa tunamaanisha tukio la jana la ufunguzi wa kampeni za UKAWA katika viwanja vya Jangwani.

Tukio lililowashtua wengi waliokuwa na matumaini makubwa kuliko fikra zao zilipoweza kufikia(overwhelmed and excited)


Kwa wengine tumeonya siku nyingi kuhusu UKAWA na hatua walizochukua.

Tulienda mabali na kuuliza katika uzi huu na mwingine maswali haya


1 UKAWA wamefanya analysis ya kutosha kabla ya kuchukuahatua walizochukua

2 Kwa hali ya kisiasa, kulikuwa na ulazima wa kuchukua hatuawalizochukua?

3 Hatua walizochukua zitaweza kulinda brand yao na politicalbase yao?

4 Wanaokea ugeni huo (receive) au wana accommodate(kuhifadhi ili ulingane namatakwa na haja ya walipofikia?)

5 Watawezaje ku merge timu mbili wakiwa safarini kwendakwenye mapamabano?

6 Wamejiandaeje kukubaliana na changamoto zingine zinazokujana ugeni walioupokea?

7 Wana political strategists wa kutosha na wanaojuawanafanya nini na kwa wakati gani na kwanini?

Hayo ni baadhi ya mambo tuliyoongelea kwa kina sana siku zanyuma.

Hakika kilichotokea jangwani si kigeni kwetu sisi wengine. Ilikuwa nijambo lililotarajiwa kabisa


Leo kinachofanyika ni post mortem baada ya maafa ya jwangwani.

Tunajua na tuliona nini kimepelekea matatizo yaliyotokea.

Tunachotaka kuwaambia akina Mbowe na Mbatia ni kuhusu siasa za majivuno zisizozingatia ushauri

Mbowe hasa ndiye anapaswa kubebeshwa mzigo uliopo na pengine unaokuja

Mbowe leo lazima aka echini na kufikiri kama kweli anakopelekaUKAWA ni njia sahihi.

Kama ndio kanywaga twende aliyosema lipo tatizo mbeleni

Maafa yaliyokea jwangwani yana sehemu kuu mbili

Timu ya UKAWA iliyopeteza Brand na kuwakabidhi wageni

Timu ya Lowassa iliyokuja bila kuwa na mkakati wa ku-mergena timu ya UKAWA

Haya ndiyo chanzo cha mivutano ndani ya UKAWA.

Jangwani si tukio moja, ni mwendelezo wa matukio ya namna hiyo na jana ilikuwa climax.

Kumekuwepo na kuficha ficha udhaifu wa UKAWA kwasababu zisizo na msingi.

Jana imedhihirisha lipo tatizo kubwa.



Inaendelea sehemu ya II
 
MAAFA YA KISIASA VIWANJA VYA JANGWANI

Sehemu ya II


UKAWA/CHADEMA ina watu wenye uwezo wa kujenga na kubomoa hoja.Hata timu EL wanao.

Kinachokosekana mkakati wa pamoja wa kutoa matokeo tarajiwa

Wakati wa kuchukua na kurudisha fomu, watu waliaminishwa siwakati wa kampeni na kifundi lingekuwa tatizo.

Wengine tuliliona kwamshangao. Kuzungumza na watu si kampeni na hilo halikuzuiliwa
!!!

Wakati wa kudhaminiwa, EL akiwa mikoani aliongea na watu kwa chini ya dakika 5. Tuliaminishwa si wakati wakampeni

Tukio la Jangwani likawekewa sababu za muda, zisizo na mashiko . Mwisho ilikafanyiwa damage control

Dakika 10 alizoongea, nazo zilisikitisha sana. Tukio lajana kisiasa lilikuwa ni kumu-introduce Lowassa kitaifa.

Ni tukiokubwa ‘major event'
Ndilo tukio lililobeba uzito wa uchaguzi kwa UKAWAkama ilivyokuwa CCM

KWANINI NI TUKIOKUBWA

Kwanza linatoa pichaya uongozi wa UKAWA kwa ujumla na fursa ya kuongea na Watanzaniana wala si wana UKAWA

Anachopaswa ni kuwafikiwa wanaokubaliana au wasio kubaliana naye na wa upande wa pili wanaoweza kubadilika.

Hivyo, hotuba ya jana ilikuwa ‘Rais mtarajiwa anaongea na taifa'

Pili, ni tukio la ku set tone ya uchaguzi. Kwamba, kwenda mbele UKAWA, katika ngazi zote sera ili kuwasaidia wagombea

Tatu, Ni kuonyesha tofauti kati yao na CCM. Kwambanini wanasimamia na watafanya nini. Kupitia ilani ya uchaguzi

Kwa muktadha huo, tukio hilo lina vitu vifuatavyovilivyopaswa kuangaliwa

1 Maudhui (theme ) kwamba, nini UKAWA wanafikiria kufanya wakipewa uongozi

2 Hamasa (excitement) , ufafanuzi (lay out) na hoja inayotokana na maudhui. Kuwajengea uwezo wa hoja

3 Connections,Mgombea na timu ya UKAWA inakuwa n amawasiliano na wananchi, kupitia mkusanyiko, Radio na TV

Ukubwa wa tukio hilo ni kuwafikia watu kwa mamilioni kwa kipinidi kifupi.

Inaendelea sehemu ya III
 
MAAFA YA KISIASA VIWANJA VYA JANGWANI


Sehemu ya III

FURSA WALIZOKUWA NAZO


Kama chama cha upinzani, fursa ya kukosoa na kueleza mbadalatofauti na CCM inayopaswa kueleza na kuitetea rekodi ikilazimika kueleza nini watafanya tofauti Mtu aiyebeba bendera ni waziri mkuu aliyeshirikivikao vya maamuzi.
Kila jambo lipo katika ‘finger tips'


Umma upo nyuma yao, kwamba kuichoka CCM kunajenga kiu yakuwasikilizwa na kila mwananchi

Walikuwa na muda wa kupanga, muda wa kuzindua kampeni , kujifunzamakosa kama si kufanya kwa ubora zaidi

KILICHOTOKEA

UKAWA wakaanza kujibizana na CCM. Wazungumzaji walikuwa na kazi ya kusafisha tuhuma au kujibu nani wa CCM kasema nini badala yakueleza sera zao

Kupandisha watu wasio na maana. Tambwe anajulikana ameshatumikiavyama vyote vikuu. Alikuwa mwiba wa Wapinzani akiwa CCM. Leo Mbowe na UKAWAwanampa nafasi ya kuongea.

Mbowe na UKAWA wameshindwa kujifunza kutoka kwaShibuda au Nkumba.


Katika muda muhimu kama ule, Tambwe alikuwa na kipi cha kusemaallichoshindwa akiwa CUF au CCM.?

Wazungumzaji wakawa ni wageni na kuua kabisa ‘political base'ya UKAWA

Kukakosekana ilie Firebrandwatu waliyoizoea kuiona kama Upinzani

Kulikuwa na kila dalili ya disorganization. Haielekei kamalilipangwa na watu wanaofahamu UKAWA kama ilivyozoeleka

KUZINDUA KAMPENI –UCHELEWESHAJWI WA KAMPENI

Kuchelewa kuzindua kampeni ni dalili ya uwepo wa mivutano ndani ya UKAWA na kutokuwa na mipango endelevu

Inaonekana hawakuwa nasera za pamoja. Tunauliza, Mbowe, miezi yote mlikuwa mnafanya nini?


Kama mtakumbuka huko nyuma tulieleza kuwa Lowassa atakuja na mizigo yake. UKAWA wamejiandaaje?

Inavyoonekana ndivyo hivyo na ndilo linaleta mipango hovyo kama ile ya Jangwani.


Inaendeea seemu ya IV
 
MAAFA YA KISIASA VIWANJA VYA JANGWANI

Seheu ya V

LOWASSA AZUNGUMZA


Akisubiriwa na mamilioni ya watu, EL alihutubia kwa dakika 10.
Katika muda huo, hakuzungumza kama kiongoziwa taifa bali mwanaharakati.

Mfano, ni nani alimwambia tatizo la Watanzania ni Babu Seya? Tatizola Watanzania ni Masheikh wa UAMSHO?


Kwa mtu aliyejiandaa dakika 10 ni nyingi sana za kutoa ujumbe.

Mwaka 1995 akizundua kampeni za CCM Nyerere alizungumza chini ya dakika10 mambo mawili

Alisema, watu wajiandikishe,wapige kura na mtu anayebebwa hajavunja sheria


Lowassa akiwa kiongozi wa UKAWA alipaswa kuongelea matatizoya taifa hili kwa muda mrefu, na upana wake.

Muda haukuwa tatizo, kulikuwa na muda uliochezewa kama ule wa akina Tambwe.

Lowassa alipaswa kuongea kwa muda mrefu kuliko mtu mwingine akiba maudhui ya sera na mitazamo.

Ndiye aliyebeba ilani ya chama, aliyepaswa kuwasiliana na umma na kujitambulisha kama Lowassa wa UKAWA.

Kilichotokea ni Lowassa kuwaelekeza watu katika tovuti, Watanzania wanaoishi kw dola1 na TV kwa jirani

Sababu za muda hazina mashiko. UKAWA wawe wakweli kwa umma kuwa kulikuwa na matatizo ya maandalizi.

Hadi wanakwenda hawakujua nini wafanye, nini waseme

Tunahakika kuna timu nzuri sana ya UKAWA , ambayo ingeweza kutoa kitu bora kuliko fyongo iliyofanyika.

Inaendelea sehemu ya IV
 
EL ni tambara bovu, anafanya kama ENRON walivyowahadaa wamarekani lakini siku ya siku ilifika. Za mwizi ni arobaini hili Jambazi sugu lililonunuliwa na Mbowe haliwezi kuwa rais.
 
MAAFA YA KISIASA VIWANJA VYA JANGWANI

HOTUBA YA PILI

Baada ya kutambua klichofanyika Jangwani ni fyongo, UKAWA wakaandaa hotuba ya pili iliyosomwa ITV.

Hii ilikuwa damage control, hata hivyo uharibifu ulikwishafanyika


Hotuba ya pili, ikama inavyoonekana katika mabandiko ya nyuma(text) nayo pia ina matatizo.

Suala si kuonyesha UKAWA watafanya nini, bali kwa njia zipi na kwasababu gani.

Kuorodhesha mikakati kila mtu anaweza, kuifanyia mchanganuo na ni suala la kiongozi na si kila mtu anaweza


Tatizo lipo pale pale, kwamba, UKAWA hawakuwa na maandalizi.

Je, ilitokana na mivutano ya ndani? Hilo ni swali gumu lakini jibu rahisi tu ni kuwa lipo tatizo


Hotuba ya kwanza ya dakika 10 iliyomhusisha Babu Seya na UAMSHO haikuwa namaana.

Hotuba ya pili, ilikosa ‘red meat' kwamba, ni orodha tu kama zile za CCM za miaka yote


Kama timu ya UKAWA ndiyo iliandaa hayo mawili, lipo tatizo tena kubwa sana.

Haiiingiii akilini imu nzima inayoweza ku organize na kuhamasisha ikishindwa hatua muhimu sana na za mwisho


Haieleweki kama washauri wa UKAWA wakishirikiana na wa Lowassa waliamua kwa nia gani.

Tunachoweza kusema ni kuwa huu umekuwa mwendelezo wa tatizo


Mfano, siku Lowassa alipokutana na akina mama wa Dar, je haikutosha kuwa hadhira muhimu kueleza kwa kina mambo yanayowahusu na jinsi gani atashughulikia yeye na UKAWA?

Ikiwa, timu ya UKAWA na Mbowe ndio ilimshauri Lowassa kwenda mwendo alio nao, timu hiyo inapaswa kuvunjwa haraka Haifai na wala haitakiwi kuwepo kabisa

Ikiwa ni Lowassa ameshauriwa na watu wake wa Karibu alio kuja nao, EL anapaswa kuwaondoa washauri hao mara moja.

Hawafai na wamemweka mahali pagumu sana. Huu ndio wakati wa kufanya maamuzi magumu.


Huyo aliyemkandhi au timu iliyomkabidhi hotuba ya babu Seya nay a ITV anapaswa au wanapaswa kuondoka katika timu ya washauri, kinyume chake maafa zaidi yapo njiani

Lakini pia inakuja kwa watu wawili muhimu katika UKAWA

Mbowe, hivi aliwezaje kuita mkutano mkubwa kama ule akiwa hajui mgombea ataongea nini.

Aliwezaje kuruhusu hotuba ya ITV isiyokuwa na ‘substance' kusomwa


Tunasema substance kwasababu uchaguzi huu ni juu ya hali za maisha za watu.

Unagusa uchumi sana. Hatujaona namba au mchanganuo unaoonyesha kauli ya uchumi ina maana yoyote


Mtu wa Pili ni Lowassa. Akiwa mzoefu wa siasa, aliwezaje kupokea hotuba ya babu Seya bila chembe ya fikra.

Aliwezaje kusoma hotuba ITV ikiwa haina substance. EL anapaswa kumuondoa aliyemshauri haraka.

Mshauri wake anaonekane kuwa ima mtu asiyejua siasa au mtu asiyeelewa nini matarajio ya anachokifanya


Na kama ni timu ya washauri, Lowassa aivunje haraka. Haimfai imemdhalilisha na akiendelea nayo, maafa ya jangwani hayataepukika


Hivi kweli Mbowe na Lowassa wameshindwa kupata vijana wanaoelewa siasa za ndani, nje, mahusiano ya jamii na uchumi wakawaweka pamoja kutengeneza kitu chenye ladha!!!

Inaendelea sehemu ya mwisho
 
MAAFA YA KISIASA VIWANJA VYA JANGWANI

MATATIZO YA UKAWA


Tuliwahi kuhoji, UKAWA wamejiunga na Timu Lowassa au ni kinyume chake?
Tukauliza, mizigo yake itahudumiwa vipi.
Kinachoonekana ni ujio kuteka UKAWA.

Tatizo lipo kwa Mbowe na UKAWA walioshindwa kuwa accommodate wageni.
Kumbuka ku accommodate ni tofauti na receive

Mbowe anasema kanyaga twende katika maafa kama yale ya Jangwani akiaminisha ana timu makini.
Timu iliyofanya research na kuja na majibu ya kisayansi.



HITIMISHO
Kuna tatizo kubwa la organization ndani ya UKAWA la kuendelea kukumbatia siasa za CCM.
Ile brand ya siasa za upinzani imetoweka


Kuna tatizo la Mbowe na UKAWA kukabailiana na ‘migrants'

kwamba, UKAWA imekubali wahamiaji wabadili culture na si kuwa sehemu ya culture.


Hakukuwa na mkakati wala mipango, ni mambo yanayotokea tu. Mbowe hakuwa na plan ''off guard'' amebakia

Kuna mvutano wa timu mbili ndani ya moja. Ni tatizo lilnalohitaji ufumbuzi wa haraka.
Kwa mwendo ulioonyeshwa na UKAWA , CCM watapata afueni huko ICU wataanza kwenda maliwato bila nurse.


Kama hali ni ile ya jangwani, kampeni inaweza kuwa imeisha kabla haijaanza

Mbowe kama kiongozi ni wakati ajaitazame na kutahmini kama bado anasababu za kuendelea kuongoza.

Makamanda wengine wali ishia njiani au kupunzishwa, naye pia ana fursa hiyo akiwa tayari aungane na wenzake


Kinachoendelea UKAWA si taasisi ya kisiasa ni taasisi ya personality. Wananchi si wajinga kiasi hicho

Lowassa mbeba bendera anapaswa kutatHmini kama washauri wake wanamsaidia.

Kwa hotuba ya Babu Seya na ile ya ITV hawana msaada, na maisha ya personality si ya kisiasa


Hizi ni zama za siasa za kileo, siasa zinazoongozwa na vijana wanaojua nini kifanyike na kwasababu gani.

Lowassa aiangalie timu ya washauri wake wa karibu sana maana ni maafa yanayosubiri muda


Kwa wapenzi na manazi wa UKAWA, lazima mkubalI kilichotokea ni fyongo.

Kurudi na kujipanga haraka ndilo jibu lenu na si kutafuta sababu zisizo na mashiko.


Kampeni ya Jangwani ni maafa makubwa kwa UKAWA ni COLLOSAL DAMAGE

MAAFA YA KISIASA VIWANJA VYA JANGWANI




Tusemezane
 
Huku kujisahau baada ya kuona makosa ya wenzao (Mkapa na Upumbavu wa Ulofa), kunanishangaza sana.

Uchu wao wa kuingia Ikulu umeingia mchanga mkubwa ambao una manyoya ya paka!

Nimewahi kuandika si kitambo sana ulazima wa kuwepo kwa strategist ambao si Mbowe, Lissu, Mbatia au Maalim..

Doesnt the two camp have enough money at least kuwaajiri political scientist na economist wanaoelewa hali halisi kuandaa ujumbe?

Hii biashara ya koroga, zungusha Pipoz ni ya kutafuta mtu mwingine kuifanya (they should find their own Nape) na Lowassa aanze kuonekana si kwa Ukawa au Watanzania bali hata wawekezaji na diplomats kuwa kweli yuko tayari kuwa Rais!

Hasira za Mkizi zitamponza Lowassa na Ukawa. Ameshaongelea la Richmond na akasema mwenye ushahidi aende mahakamani. That was the end of it, hapakuwa na haja ya Sumaye kuendella kuongelea hata kuyasema ya watu kuwa wagonjwa wakishavuka 50!

ni upotofu kushani kuwa ujazo wa watu kwenye mikutano ndio kupatikana kura!

Tumewaambia mara nyingi, na kama kawaida tunapigia mbuzi zeze!
 
Rev.Kishoka tunadhani wapo watu wazuri tu wanaoweza kuandaa ujumbe
Tatizo lipo kwa viongozi kuweka timu hizo pamoja Nimesikia hotuba ya Jangwani, haikuandaliwa na timu naweza kusema. Kuna hotuba ya ITV text, ile haikuandaliwa na timu naweza kusema

Tunasema hayo kwasababu, ukisoma tu utaona ni ima Lowassa kaandika mwenyewe, kijana wake au kaandikiwa au mtu si watu. Kama ile hotuba ni timu ya watu basi UKAWA ni janga.


Hivi unawezaje kuwa na timu inayoorodhesha habari badala ya mchanganuo.
Unapouzungumzia Afya, lazima utueleze tupo wapi. Vigezo vipo kama WHO, SADC, EAC, AU na ikishindikana basi linganisha na majirani wenye ukubwa tunaolingana na uchumi unaokaribiana


Akizungumzia elimu, hajaeleza elimu unataka iwe vipi nakwanini. Utatumia rasilimali gani kufikia malengo hayo
Akizungumzia utalii, angalia ni nini anataka kufanya tofautina utalii uliopo ili kuongeza tija

Mapato, nataka kufanya nini ili tuweze kunufaikana kodi, kupunguza omba omba, na matumizi yetu

Akizungumzia mahusiano ya kimataifa, suala si haki za binadamu. yapo yanayotuhusu sisi na majirani n.k.

Kuna mambo kama muungano, ni donda kubwa, analionaje na analizungumzia vipi. wananchi wanataka kuona mbadala.

Si babu Seya wala UMASHO. Si kuorodhesha matatizo bali kuelezaufumbuzi.


Hotuba ya ITV Ina mapungufu. EL ajiulize nani amempa kitu cha chini kiasi kile. Mbowe ajiulize, aliruhusu vipi kitu cha chini kiasi kile

Kama hotuba ya Babu S na ile ya ITV zingeandikwa timu tungeona mtiririko fulani. Ile imeandikwa na mtu mmoja, haijulikani ni UKAWA au ni timu Lowassa. Ni mtiririko wa mawazo ya mtu bila substance.

Mbowe wabanwe, nani huyu anayeandika hotuba za UKAWA za kiwango cha chini.

Nadhani Mbowe apewe muda akiwa tayari aungane na wenzake


.......
 
MAAFA YA KISIASA JWANGWANI-UKAWA

Badala ya kuanza kampeni, UKAWA wangerudi makao makuu watathmini colossal damage tarehe 29 Jangwani.

Wafanye post mortem ya kubaini nani yupo au wapo nyuma yauozo ule na kuwaondoa haraka kabla ya jioni ya leo hata kama ni wakubwa.Hawafai ni aibu si kwa UKAWA bali taifa

Kilichotokea Jangwani ni janga ni tatizo. Kinahitaji msaadawa haraka

Hapa tungewaalika akina Molemo na Tumaini Makene . Fikisheni ujumbe kuhusu uharibifu uliotokea

Mwambieni Mbowe, sisi Wananchi na si wanachama wa UKAWA wanasema ajitathmini

Mshaurini Lowassa afumue timu ya washauri , ni tatizo.

Mshauri wake aliyesoma na kumkabidhi ile hotuba bila kumshauri matatizo yaliyopo alimkabidhi kaala moto. Hamfai asilani

Hakuna haja ya kuanza kampeni wakati hamjamaliza rescue operation iliyotokana na desert storm ya 29.
 
Nimeona mikutano ya Lowassa ya jana ya Mafinga na Iringa....Bado wanaendelea kuwatumia Sumaye na Masha kama wazungumzaji watangulizi katika kampeni za Lowassa....Na Sumaye anajikita katika kile kinachoonekana kumsafisha Lowassa juu ya tuhuma za 'ufisadi'....Na Masha anasimama jukwaani kuzungumzia 'kukamatwa kwake na Polisi' na kunyimwa dhamana...

Hii ni wrong move...

Both Sumaye na Masha wangejikita katika kuzungumzia Ilani (kumsaidia Lowassa ambaye si muongeaji) badala ya kuishambulia serikali na kutoa utetezi wa ufisadi....Hilo la kutetea ufisadi wangemuachia Lowassa alizungumze mwenyewe kuondoa ile dhana kwamba hana guts za kupinga ufisadi....Pia Sumaye sio msafi kiasi cha kusimama jukwaani na kumsafisha Lowassa..Washindani wa Ukawa watatumia nafasi hii kuwashambulia wote Sumaye na Lowassa(rejea kauli za Habib Mchange, Zitto Kabwe, Samwel Sitta na UVCCM kwa nyakati tofauti jana na juzi)...

Kwa ujumla hoja ya kupinga ufisadi anayojinasibu nayo Sumaye sasa hivi ni mfu kwani kinara namba 9 wa ufisadi kwa mujibu wa viongozi wa CHADEMA pale Mwembechai mwaka 2011(Edward Lowassa) ndiye wanayemtegemea kushika dola...Sasa ni vigumu sana kwa CHADEMA kuanza kusimama jukwaani kumsafisha Lowassa kipindi hiki cha Kampeni badala ya wale viongozi waliosimama majukwaani wakiuaminisha umma wa watanzania kwamba Lowassa ni fisadi na ushahidi wanao(Rejea kauli za Dk. SLAA, MNYIKA, GODBLESS LEMA, SUGU na Mwenyekiti Mbowe)...Ushahidi wa video za kauli za viongozi hawa wa CHADEMA zinazosambazwa Youtube, Whatsapp na Instagram ni kielelezo tosha kwamba CHADEMA hawasimamii wanachokitangaza/wanachokihubiri...Ni vigumu sana kwa mtu kama Lema, Slaa, Mbowe, Mnyika ama Sugu kusimama jukwaani sasa hivi na kuanza kumnadi Lowassa kwamba ni mtu msafi na anafaa kuliongoza Taifa la watanzania...Video na audio clips zenye kauli zao dhidi ya Lowassa zinawaumbua..Mtu pekee ambaye wanaona atamsafisha Lowassa ni Sumaye...Ambaye kimsingi sio MSAFI...

Ukimya wa Dk. SLAA mpaka sasa ni pigo lingine kwa UKAWA...Kuna wanachama wa CHADEMA ambao ni waaminifu kwa Dk. SLAA na mpaka sasa wanasubiri kauli yake na wanaonekana wazi kutomuunga mkono Lowassa...Na wengine walienda pale Jangwani wakitegemea kumuona Dk. SLAA kama ilivyoelezwa kwamba atakuwepo siku ya uzinduzi wa Kampeni...Hawa wanaweza wakawa pigo kubwa sana kwa CHADEMA/UKAWA na kuna uwezekano wakapiga kura za hasira kuonesha kutoridhishwa na uamuzi wa Lowassa kuwa Mgombea Urais...

Hakika huu ni uwekezaji usiotabirikam
 
Ukimya wa Dk. SLAA mpaka sasa ni pigo lingine kwa UKAWA...Kuna wanachama wa CHADEMA ambao ni waaminifu kwa Dk. SLAA na mpaka sasa wanasubiri kauli yake na wanaonekana wazi kutomuunga mkono Lowassa...Na wengine walienda pale Jangwani wakitegemea kumuona Dk. SLAA kama ilivyoelezwa kwamba atakuwepo siku ya uzinduzi wa Kampeni...Hawa wanaweza wakawa pigo kubwa sana kwa CHADEMA/UKAWA na kuna uwezekano wakapiga kura za hasira kuonesha kutoridhishwa na uamuzi wa Lowassa kuwa Mgombea Urais...

Hakika huu ni uwekezaji usiotabirika

Nafikiri siasa za Afrika kwa ujumla ni ngumu na zinataka watu wenye ngozi ngumu, Nikimwangilia Mh. Mkapa alivyodharilishwa na serikali ya Kikwete hadi kuzomewa, nikimwangalia Jaji Warioba aliyetukanwa na kula vibao na aliyefanya hivyo kupewa cheo, nikimwangilia Mh. Sitta walivyonyanyaswa wakati wa Richmond na wakati wa kugombea uspika, lakini leo hii hawa watu wote wanasimama jukwaa moja kama wanaccm na kumuombea Magufuli kura.

Huwezi kufanya siasa za Tanzania kama wewe si mnafiki, kama wewe huwezi kugeuza geuza maneno na nafikiri hapa ndipo Dr. Slaa anaposhindwa. Yule mzee akishasema kitu amesema. Tuliona wakati mwaka 2010 baada ya mizegwe ya kura kati yake na Mh. Kikwete, kama alikataa meza moja na Kikwete basi haizidi mara 2 tena kwa ulazima. Wazee kama Dr. Slaa ni wachache mno katika siasa yetu za kiafrika.

Ila pengo lake tunaliona kuliziba haitakuwa kazi rahisi lakini baada ya uchanguzi tunaweza kuona team mpya zikija na mambo mapya.

Kuhusu Sumaye na Masha kuzunguka na Lowassa nafikiri ni kwa vile hao wengine uliyowataja wako katika majimbo yao na hiki ndicho kimekuwa kilio cha MM kila uchanguzi kuwa wakati wa uchaguzi viongozi wote uenda katika majimbo yao na kumuacha mgombea urais akiwa mkiwa. (Ila kila mtu anafahamu kiinua mgongo cha mil.200 sasa nani mzalendo wa kuacha hicho kitita?)
 
Nafikiri siasa za Afrika kwa ujumla ni ngumu na zinataka watu wenye ngozi ngumu, Nikimwangilia Mh. Mkapa alivyodharilishwa na serikali ya Kikwete hadi kuzomewa, nikimwangalia Jaji Warioba aliyetukanwa na kula vibao na aliyefanya hivyo kupewa cheo, nikimwangilia Mh. Sitta walivyonyanyaswa wakati wa Richmond na wakati wa kugombea uspika, lakini leo hii hawa watu wote wanasimama jukwaa moja kama wanaccm na kumuombea Magufuli kura.

Huwezi kufanya siasa za Tanzania kama wewe si mnafiki, kama wewe huwezi kugeuza geuza maneno na nafikiri hapa ndipo Dr. Slaa anaposhindwa. Yule mzee akishasema kitu amesema. Tuliona wakati mwaka 2010 baada ya mizegwe ya kura kati yake na Mh. Kikwete, kama alikataa meza moja na Kikwete basi haizidi mara 2 tena kwa ulazima. Wazee kama Dr. Slaa ni wachache mno katika siasa yetu za kiafrika.

Ila pengo lake tunaliona kuliziba haitakuwa kazi rahisi lakini baada ya uchanguzi tunaweza kuona team mpya zikija na mambo mapya.

Kuhusu Sumaye na Masha kuzunguka na Lowassa nafikiri ni kwa vile hao wengine uliyowataja wako katika majimbo yao na hiki ndicho kimekuwa kilio cha MM kila uchanguzi kuwa wakati wa uchaguzi viongozi wote uenda katika majimbo yao na kumuacha mgombea urais akiwa mkiwa. (Ila kila mtu anafahamu kiinua mgongo cha mil.200 sasa nani mzalendo wa kuacha hicho kitita?)


Alinda,
Mgombea wenu atleast jana Mafinga na Iringa kaongea sense kdg kwa kuonyesha tatizo, kwa nn ni tatizo na namna ya kulishughulikia. Angefanya hivyo Jangwani bila kugusia upuuzi wa akina Babu seya kusingekua na maneno sana, japo kama mwanasiasa wa upinzani anatakiwa awe mahiri sana kwenye convicing power huku akipambana kwa hoja na kuonyesha why achaguliwe yeye.

Niliandika kwenye post yangu ya juu hapo soon after Jangwani incidence, wagombea inabidi watueeleze why tuwachague wao sio wengine, watafanya nn na kwa njia zipi watafanya, na tulishauri sana kwamba non Issues hazipaswi kabisa kujadiliwa kuanzia wapambe wake mpaka mgombea, kujitete kuhusu Richmond na takataka zingine hakupaswi kuzungumzwa, wanahitaji kufanya siasa za kushambulia sio kujilinda. La sivyo mgombea wao na UKAWA kwa ujumla vitapata anguko kubwa sana.

Nguruvi3 ameeleza sana kwenye mabandiko yake kwamba kuna udhaifu mkubwa sana kwenye timu ya UKAWA ambayo inabidi ijitathimini namna ya kupambana na kuweza kurejesha public trusts sio kuwapa ahueni wapinzani wao, kweli uchaguzi huu una mambo, mambo yanaenda kinyume nyume sana tofauti na matarajio.
 
Alinda,
Mgombea wenu atleast jana Mafinga na Iringa kaongea sense kdg kwa kuonyesha tatizo, kwa nn ni tatizo na namna ya kulishughulikia. Angefanya hivyo Jangwani bila kugusia upuuzi wa akina Babu seya kusingekua na maneno sana, japo kama mwanasiasa wa upinzani anatakiwa awe mahiri sana kwenye convicing power huku akipambana kwa hoja na kuonyesha why achaguliwe yeye.

Niliandika kwenye post yangu ya juu hapo soon after Jangwani incidence, wagombea inabidi watueeleze why tuwachague wao sio wengine, watafanya nn na kwa njia zipi watafanya, na tulishauri sana kwamba non Issues hazipaswi kabisa kujadiliwa kuanzia wapambe wake mpaka mgombea, kujitete kuhusu Richmond na takataka zingine hakupaswi kuzungumzwa, wanahitaji kufanya siasa za kushambulia sio kujilinda. La sivyo mgombea wao na UKAWA kwa ujumla vitapata anguko kubwa sana.

Nguruvi3 ameeleza sana kwenye mabandiko yake kwamba kuna udhaifu mkubwa sana kwenye timu ya UKAWA ambayo inabidi ijitathimini namna ya kupambana na kuweza kurejesha public trusts sio kuwapa ahueni wapinzani wao, kweli uchaguzi huu una mambo, mambo yanaenda kinyume nyume sana tofauti na matarajio.

Nakubaliana na kutokukubaliana na wewe..

Kwanza ni kweli kabisa kuwa wananchi waliowasomi wanataka kusikia Ilani yenu na utekelezaji wake. Na ni kweli kuwa tunatakiwa kuwa na siasa za namna hii yaani hoja kushindana na hoja, Ilani ya chama fulani kushindana na Ilani ya chama fulani, na nk.

Lakini swali la kujiuliza je wananchi walio wengi wana uelewa wa mambo ya Ilani za wagombea/Vyama?
Mfn. Juzi nilisoma habari kuhusu Makamba anavyoeleza jinsi Lowassa alivyokuwa mroho wa madaraka lakini kasahau kuwa CCM ndio waroho wa madaraka maana nusu karne wako madarakani na hawataki kutoka...

Nimesoma Mwakyembe anasema Lowassa ni fisadi kuhusu Richmond lakini kasahau kuwa yeye alitamka kuwa "Waziri mkuu ajipime na kuona kama anaweza kuendelea kuwa waziri mkuu baada ya madudu yote ya Richmond"

Nimeona video ya Sitta anamnaga Lowassa kuwa walitengeneza mkataba hewa wa Dowans na mpaka sasa serikali inalipata Dowans mamilion ya pesa.. Ila akasahau kuwa kama serikali inafahamu ni mktaba hewa kwanini waendelele kuwalipa?? na akaongelea mambo ya Msiba wa Mzee Kisumo na msafara wa Lowassa.

Hao ni baadhi ya viongozi wa team ya kampeni, kwa bahati mbaya kati yao hakuna aliyeongelea ni kwanini tuwape kura tena kama wameshindwa kwa nusu karne kujenga maabara, wanafunzi bado wanakaa chini, barabara mbovu, mahospitalini hakuna dawa, wazee wamesahaulika, wanafunzi vyuo vikuu kukosa mikopo na nk.

Ni kwanini hawa wakongwe na siasa hapa nchini wanasiasa za mipasho? Je hii ndio siri yao ya ushindi? Je ni kweli kuwa wapiga kura walio wengi wanapenda kusikia usafi au kashfa za wagombea?

Hebu fikiri kidogo mgombea urais anapanda kwenye jukwaa anaeleza Ilani zake na jinsi ya kufikia malengo yake na baada ya hapo anaondoka, anakuja mwingine anaelezea kashfa au na tuhumu kwa mpinzani wake, anaelezea ilani zake na kuondoka swali kwa kila mtu anayesoma hapa je ni nani atapata kura nyingi katika eneo hilo?

Mfn mwengine hebu jaribu kuanzisha thread inayohusu Ilani za uchaguzi za vyama mbali mbali na thread ya kashfa kwa viongozi wa kuu wa vyama vya upinzani (maana CCM kumezoeleka) ni thread ipi itapata views na wachangiaji wengi? Hawa ndio watanzani na wengi wao wanapenda kuwafahamu viongozi wao kama ni wasafi au kama nao wanakashfa.

Hivi kweli Lowassa akienda Dodoma alipokuwa Makamba je hasijibu tuhuma alizopewa tupiwa na Makamba? Je akienda Shinyanga na penyewe akae kimya? Mimi naona ni lazima hazijibu na kama kuna tuhuma za Magufuli naye arushe maana ndizo siasa tulizochangua.

Tangu mwaka 1995 hizi ndio siasa za chama cha mapinduzi kutengeneza kashfa hata ikibidi kulipa watu pesa ili kudhalilisha baadhi ya wagombea mf. Mrema na Angelina, Dr. Slaa na ex wa mama Josephine. au hata CUF ni chama cha waislamu. hii ni mfn wa viongozi ambao walikuwa wasafi hawana hata tone la ufisadi lakini tuhuma zilitafutwa na kusambazwa na kwa bahati mbaya kabisa CCM walishinda. Hivyo kuibua kashfa ni mbinu mmoja wapo ya kupata kura...(kwa Tanzania)
 
Dada yangu Alinda, post #374 ,
tutajadiliana zaidi juu ya uliyoyaongea, there is a point sana tu maana pia lazima uwasome watu wako wanataka kusikia nn, kuliko kumis the target na kukosa Kura, tutajadili zaidi nafasi gani UKAWA wapo na CCM wapo na nn wanapaswa kufanya katika kipindi hiki, nimekuelewa sqna point zako mama yangu, ngoja tungezee kuboresha.
 
Alinda na King Suleiman

Siasa za nchi zetu bado zina matatizo. Hata hivyo, kuna mambo yanayofanyika katika uchaguzi popote duniani kwa sababu maalum. Kwa wenzetu kuna watu wana strategists ambao Balantanda, na sisi wengine tumepiga kelele sana.

Kinachotokea kwa CCM ni mambo mawili, kwanza wanaleta distractions za kampeni kwasababu hawana cha kuonyesha miaka 50, na pili hali yao ni ngumu kiasi cha kuwalizumu kutupa karata ya aina yoyote iliyo mbele yao

CCM wanajua hawana cha kuonyesha, na ilani zao hazina jipya, ni photocopy

Kwa upande wa wapinzani, wanakosa watu wa mikakati na hilo ni tatizo.

Kama mlitusoma hapo nyuma, tumeelezea kwa kirefu sana kuhusu maafa ya Jwangwani.

Tunawaeleza wapinzani kuwa tatizo si kilichotokea bali watu waliossababisha maafa yale.

Ndio maana tukahoji kama wapo na wanaendelea na kazi basi maafa mengine tarajiwa yapo njiani

Kwa wapinzani, walitakiwa kuwa na strategist watakaowalazimisha CCM kurudi katika hoja

Kwa mfano, suala la umeme. CCM wanasema bei ni kubwa kwasababu ya Richmond.

Well wangeulizwa wanasemaje kuhusu Escrow ya jana? Nani ameshatakiwa? Nani analipa gharama za pesa za viroba?

Pili, wakisema fulani ni fisadi ni rahisi kuwauliza nani alikuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Usalama?

Ilikuwaje waliweza kuishi na fisadi huyo hadi juzi?

Wlichukua hatua gani na kama hawakuchukua ni kwanini?

Hiyo ni mifano michache sana. Kazi ya wagombea si kujibu tuhuma rahisi kama hizo.

Hizo ni distractions ambazo zinaajibiwa na 'attacking dog(s)'

Sasa ukiangalia timu ya UKAWA, hakuna mkakati kama huo. Kumtanguliza Sumaye na Lowassa at the same time ni kuua brand ya upinzani. Wameliona hilo? Jibu ni hapana kwasababu hawana wana mkakati

Mgombea anatakiwa ajikite katika sera, mwisho wa siku wanaotukana hawataukuwa na hoja, watarudi kwenye mada na ndipo pa kuwashika.

Mungu aliwapa neema upinzani kutokana na maneno ya Mkapa 'wapumbavu na Malofa' utaona wananchi wanaichukulia kauli hiyo kwa hisia na hasira kubwa sana.

Wapinzani wanachotakiwa ni kuiongelea kauli hiyo kama sehemu ya hisia na kuwaleta karibu wananchi.

Kisha sera zinamwagwa wananchi wakiwa tayari na wazo la upumbavu na ulofa waliorushiwa

Kinyume chake tumesikia Babu Seya na UMASHO.
Nani anawashauri hawao viongozi asiyeweza hata kuona mambo rahisi kama haya?

Hayo yanawezekana kama kuna mipango ya namna ya kuongea, nini cha kuongea , nani aongee na kwa muda gani

Yanapotokea kama yale ya Jwangwani kupandisha watu, vurugu tupu ile dhana nzima ya kushambulia inaondoka inabaki kujilinda. Hapo kuna tatizo

Tusemezane
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,
Kwenye bandiko lako #376 , mimi nakuelewa vema kabisa mkuu wangu, na ninachanganyikiwa kabisa maana ninachojua mm mgombea hakutakiwa kabisa kujibu mipasho na kuongea non issues, pia watangulizi wake hawakutakia kabisa kujihusisha nayo, na hapo CCM wangekosa majibu na kuacha porojo kugeukia kwenye sera. Sasa wao wanawapa maeno kila siku kwa iisue ambazo sio muhimu sana.

Kitu chapili cha ajabu sana,nimeshangaa sana UKAWA original hawapo front kwenye kampeni za mgombea na inakua kama wageni ndi wamekuja kuteka kampeni za UKAWA, ama kweli wame wareceive sio kuwaacomodate kama Nguruvi3 alivyosema, siasa za mwaka huu ni za ajabu sana na zinanichanganya, mm kila nikiona kuna fursa za zinajitokeza kwa wapinzani lakini wao wanafanya kinyume.

kiufupi mkuu Nguruvi3 mm binafsi nimekata sana tamaa sana, japo naamini labda kuna maajabu yatajitiokeza kurescue sutuation.
 
Swali ni kuwa kwa miezi hii karibu miwili iliyobakia wataendelea kutuma hotuba zake kwenye mitandao?

Au siku moja atasimama na kuelezea kwa kina? Au wapiga kura wanatakiwa kumkubali tu kwa imani hata kama hawajui yeye mwenyewe anasimamia nini hasa?

Kama yeye mwenyewe hakisemi kila anachosimamia katika mambo muhimu tutajuaje kile kinachosemwa atasimamia kweli anakiamini?


Are you implying that the guy can not speak? I wonder why he spends so much money to sell himself.
 
Nafikiri siasa za Afrika kwa ujumla ni ngumu na zinataka watu wenye ngozi ngumu, Nikimwangilia Mh. Mkapa alivyodharilishwa na serikali ya Kikwete hadi kuzomewa, nikimwangalia Jaji Warioba aliyetukanwa na kula vibao na aliyefanya hivyo kupewa cheo, nikimwangilia Mh. Sitta walivyonyanyaswa wakati wa Richmond na wakati wa kugombea uspika, lakini leo hii hawa watu wote wanasimama jukwaa moja kama wanaccm na kumuombea Magufuli kura.

Huwezi kufanya siasa za Tanzania kama wewe si mnafiki, kama wewe huwezi kugeuza geuza maneno na nafikiri hapa ndipo Dr. Slaa anaposhindwa. Yule mzee akishasema kitu amesema. Tuliona wakati mwaka 2010 baada ya mizegwe ya kura kati yake na Mh. Kikwete, kama alikataa meza moja na Kikwete basi haizidi mara 2 tena kwa ulazima. Wazee kama Dr. Slaa ni wachache mno katika siasa yetu za kiafrika.

Ila pengo lake tunaliona kuliziba haitakuwa kazi rahisi lakini baada ya uchanguzi tunaweza kuona team mpya zikija na mambo mapya.

Kuhusu Sumaye na Masha kuzunguka na Lowassa nafikiri ni kwa vile hao wengine uliyowataja wako katika majimbo yao na hiki ndicho kimekuwa kilio cha MM kila uchanguzi kuwa wakati wa uchaguzi viongozi wote uenda katika majimbo yao na kumuacha mgombea urais akiwa mkiwa. (Ila kila mtu anafahamu kiinua mgongo cha mil.200 sasa nani mzalendo wa kuacha hicho kitita?)

Alinda ndg yangu,
nimesikia tetesi mitandaoni,kesho Dr.Slaa anamwaga manyanga, sasa hii itakua pigo takatifu na demage kubwa sana kwa UKAWA na sijui watafanyaje iki kuniokoa, naombea tu atumie busara, maana kwa namna yoyote ile atarudisha nyuma mipango ya UKAWA kwa kiwango kikubwa mno na mambo nayaona yakienda mrama, only God knws wht willhappen after his damage, kiuhakika wajipange sas akina Mbowe.
 
Naomba tuulizane, je tunavyoikomalia Ukawa na kuichambua chambua kama mchicha au mchele tunawaelewa wananchi wengi wapiga kura?

Maana kama ni kuichambua CCM, tumeichambua miaka nenda rudi na kila mwaka bila kujali scandal gani, umasikini wa kiwango cha medali ya dhahabu olimpiki, bado Watanzania waliendelea kukipigia kura CCM na CCM wameendelea kutudharau sisi "wachambuzi"!

What if Lowassa na wenzake nao wameibaini formula ya ushindi ya CCM? maana wakati tunahoji kuambiwa tukasome hotuba na ilani kwenye website ya Chadema, CCM wametoa PDF na ilani ya kurasa karibu 230 na hatuhoji ni nani huyo mwananchi mpiga kura wa kijijini au hata mjini atakayekaa chini kupitia kurasa 230 zenye majedwali na misamiati migumu ambayo haielewi?

Hatujiulizi ni vipi wananchi hawajuuliza ili kupata ufafanuzi wa hizo Milioni 50 kwa kila kijiji kama Mama Samia alivyosema, lakini leo tunamhoji Lowassa kusomesha elimu bure?

Nikiliangalia hilo la Shilingi Milioni 50 na lilivyopokelewa kwa shangwe (kwanza hiyo ni ahadi ya rushwa kupata kura), je shilingi hizi milioni 50 ni za kazi gani katika kijiji? ni wananchi kugawiwa fedha? ni za kununulia mabati ya shule? ni ya kununua magodoro ya zahanati? ni ya kuchimba mifereji? ni ya kununua ng'ombe wa mbegu? Hizi fedha ni za nini? je fedha zinazotolewa kila mwaka kwa shughuli za maendeleo na matumizi Wilayani haziendi huku vijijini?

Nikiongelea hili la Milioni 50 na rafiki yangu Mzee Mwanakijiji, akanikumbusha Mabilioni ya JK alipoingia madarakani na zile fedha za community fund, je uwiano wa kijiji chenye watu 100 na kijiji chenye watu 1,500 utapimwa vipi ikiwa kila kijiji kitapokea Milioni 50?

Nauleta huu mfano wa Milioni hamsini na ulivyopokelewa na wananchi kwa matumaini na vifijo kusema: Jamii ya Watanzania si wengi wanachambua mambo kwa kina na hata kuona mapungufu ya wazi.

Je Masha aliposema ameonewa na polisi na kuwekwa ndani kwa kuhoji, si ndivyo 50% ya walioko magerezani na jela wameswekwa kibabebabe? Hata la Babu Seiya na Mashehe si wananchi walilipuka kwa nguvu kabisa na limekuwa gumzo?

Sasa najiuliza ni nini sisi "wachambuzi" hatukioni miaka yote na CCM wanaendelea kujiamini hata kudiriki kuita wanaoihoji na kuipinga kuwa ni Wapumbavu na Malofa?

Nikikumbuka 1995 jinsi Mtikila na magabacholi au Mrema na mkwara wa kupambana na Rushwa akiingia ikulu na kisha wakaambulia kura za kubahatishabahatisha, je ni kitu gani wapiga kura wa Tanzania wanakiangalia kutoka kwa mgombea?

Jana na leo, Mwakyembe na Sitta wameudanganya umma tena kwa swala la Richmond huku wengine tunajua wao wawili walikuwa na uwezo mkubwa kuilazimisha Serikali kama Bunge kufuta mkataba huo mara moja na kuokoa mabilioni tuliyoyalipa kama Capacity Charge kwa Richmond, baadaye Dowans na sasa Symbion. Ikiwa waliweza mlazimisha Waziri Mkuu kujiuzulu, walishindwa nini kuilazimisha Serikali kufuta huo mkataba na wote walijua gharama tuliyoipata na IPTL na ubovu wa mkataba wa Richmond?

Hivyo lazima kuna kitu ambacho hatukielewi kwa kuwa tunapima na kuchambua kila anachokula bata na tunakuwa wepesi kutahamaki na kuonyesha mshangao huku Watanzania wanaimba korogakoroga zungusha zungusha Pipoz Pawa!
 
Back
Top Bottom