Chadema tunajifunza nini kutokana na uchaguzi wa liberia na uhusinao wetu na conservative party??. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema tunajifunza nini kutokana na uchaguzi wa liberia na uhusinao wetu na conservative party??.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kulwa12, Nov 9, 2011.

 1. k

  kulwa12 Senior Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu naandika hili kwa uchungu mkubwa kutokana natabia inayokua sasa kwa kasi kati yetu sisi watu tunayoitakia mema chama cha Chadema,tabia ya baadhi yetu kutoa maneno ya kejeli na matusi hasa kwa watuwanaochangia humu katika JF na kwingine mawazo yanayopingana na sera au misimamoya viongozi wa chama.

  Naomba leo nichangie mambo mawili ambayo wengi sana nimeona tuna dhalau umuhimu wake lakini yana hatari kubwa sana kama ya kibaki kama yalivyo.

  Kwanza ni la chama chetu kuwa na ushusiano na chama cha Conservative cha Uingeereza na pili ni chama chetu kuwa na sera (ideology) za Ubebari (Capitalism) na soko huria (Freemarkets).

  Ni ukweli usiopingika kabisa kwamba CDM inauhusiano wa damu na wakaribu sana na Chama cha mabeberu cha Conservative cha uingereza,ambacho kinajulika na sera zake za upebari(Capitalisim) zenye kukumbatia matajili na watu wenye uwezowa kifedha na huu ndio misingi mkuu hasa vyama vya Ki-conservative duniani kote(Kujali tabaka la matajiri).

  Katika vyombo vingi vya kimagharibi hasa UingerezaCDM inajulikana kama Conservative Party of Tanzania na kama chama chenye sera za Ubepari(Capitalisim) na kinachoaminikatika soko huria (Free Markets).

  CDM kwa miaka mingi sana imekua ikipata misaada ya kifedha na kiutaalamu wa kisera kutoka chama cha Conservative cha uingereza.Ushaidi nimetoa wapi kusema haya?? Kuna ushahidi mwingi sana na hililiko wazi kabisa.

  Mwaka 2005 kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania,chama cha Conservativekilimtuma Tanzania mtaalamu na nguli wachama hicho aitwae Reberat Halfon akiungana pamoja na mtaalamu muelekezi maarufu duniani wa sera za Kibepari na siasa aitwae John Earl ili kuja Tanzania kukisaidia chama cha CDM katika uchaguzi wa 2005 hasa katika mambo yafatayo,kwanzakusaidia CDM kutambua ipeleke katika majimbo gani rasilimali za kusaidiakushinda majimbo hayo wanayoyalenga kushinda (hii ni sawa na kuja kusimamiamatumizi ya fedha ambazo nyingi zilitolewa na chama cha conservative),Pili kusaidiaCDM kuunda kauli mbiu ya uchaguzi na ujumbe au sera za kutumia kwenye kampenina mwisho kusaidia kuratibu mpangilio(Orgainise) na mawasiliano katika makao makuu ya CDM.

  Mtaalamu huyu baada ya kumalizika kwa uchaguzi aliandika makala katika mtanadao maarufu huko wingereza wa the Social Affair Unity, yenye kichwa cha bari "Chadema offersTanzania real change and genuine democracy", katika makala hii inatoa ushaidi zaidi juu ya hoja zangu kwamba CDM inasaidiwa na Conservative party na pili ni chama chenye sera za kibepari(Capitalism).

  Kwa kifupia mtaalamu huyuanasema mambo yafatayo kuhusu chadema katika makala yake,naomba kunukuu hukunikitoa ufafanuzi,"Thus in 1993, Chadema was born. This was a politicalmovement that believed in an open society with open markets, that the best way of ending poverty was through a strong economy based on capitalism",akimanisha (mwaka 1993 Chadema ilizaliwa.Hii ilikua ni harakatiza kisiasa zinazoamini katika jamii iliyo wazi yenye masoko huria,na njia boraya kumaliza umasikini ni kupitia uchumi imara unaoelemea mfumo wakibepari),maelezo hapo juu yanazihirisha wazi kwamba CDM inaamini katika ubepari (Capitalism) na sera za soko huria.

  Anaendelea kusema kuhusu ushirikiano kati ya Chadema na Conservative Party na jinsi ambavyo alitumwa Tanzania na Conservative Party na akikili wazi kwamba wataalamu wengi sana kutoka conservative party wamekua wakija Tanzania kutoa mafunzo kwa viongozi wa chadema,naombakunukuu,"In the UK, the Conservative Party International Office has been instrumental in giving Chadema advice and training support. I was sent to Chadema along side John Earl, a highly respected political consultant (once running field operations at CentralOffice), our job was to help Chadema target resources at target seats, position the movement in terms of their values and help define a political message as well as organise their Party HQ. All these activities were given strong support by Chadema staffers and the Party Central Committee. Many other Conservative Party trainers have gone to Tanzania to support Chadema in every way possible.).

  Ndugu zangu naomba sana sana tuungane kuwahoji viongozi wetu juu ya mambo haya makubwa mawili kwani nawambia wazi kwa jinsi Watanzania walivyo ichoka CCMhakika tutashinda uchaguzi ujao,ila hatutadumu madarakani kama Chadema kinaingiamadarakani na sera hizi za ubepari na kwa msaada wa chama cha kibepari chaconservative,sera hizi zitawafanya wananchi wazidi takua na hali mbaya zaidizadi kuliko nyuma na hawataona tofauti yoyote kati ya CDM na CCM.

  Tukumbuke sasa duniani mapambano yaliopo ni kati ya wananch na mfumo wa ubepari(Capitalism),angalia marekani nzima sasa wananchi wanaandamana na wameanzisha vuguvugu wanaloliita occupy wall street Movement,kupinga mfumo wa huu wakibepari na sera za soko huria zilizosababisha wananchi 99% wawe masiki wakutupa marekani na 1% ya idadi ya wananchi matajiri wa kutupa.Sasa tujiulize kama hizindio sera za Chadema je tutafikia lengo la kukomboa masikini wa nchi hii??.

  Naomba nitoe mfano wa mwisho halisi kabisa amabao utatuonesha nini kinatokea chama kinachoingia madarakani kwa nguvu ya umma na huku kwa ndani kimekumbatia seraza ubepari na pia kimeingia madarakani kwa msaada wa chama cha Conservative,

  Miaka mitano tu iliopita nchini Liberia, Chama cha UNITY PARTY (UP) kikiongozwa namgomea wake mama Sirlef-Johnson kilipataushindi wa kishindo nchini Liberia nakupewa idhini ya kuchukua dola,tukumbuke uchaguzi huu ulisimamiwa na nchi zamagharibi (UN) na mgombea wa UP aliungwa mkono na na chama cha Conservative nanchi zingine za magharibi ili kushinda uchaguzi huu na tukumbuke huyu mamaaliishi muda mrefu nje ya nchi na akifanya kazi UN.

  Kwa manufaa ya wote chamahiki UP ni chama rafiki sana cha chadema na kinamisingi,imani na mtazamo sawakabisa na Chadema,Chama hiki cha UP pia kinakumbatia sera za Ubepari (Capitalism) na soko huru kama sera zakerasimi na msingi wa chama kama ilivo Chadema.Pia tukumbuke Chama cha UP ni mwanachama pamoja na chama cha chademakwenye ummoja wa vyama vikuu vinne vya Africa unaoitwa Democratic Union of Africa (DUO),ni muungano wa vyama vinavyoamini katika sera za Ubepari(Capitalism) na Soko huria (Free markets),ummoja huu unapata masada mkubwa wakifedha,kisera na kitaalamu kutoka chama cha Conservative cha uingereza,ikiwemo kufadhilia miradi mbalimbali ya vyama hivi.

  Tarehe 18,march,2011,kulikua namkutano wa ummoja huu uliofanyika nchini Liberia na uliandaliwa na chama cha Conservativena cha cha UP cha Liberia,katika mkutano huu Chadema kiliwakilisha na mheshimiwaMbowe .Mkutano huu ulihutubiwa na Hon. Andrew Rosindell,ambaye alikiwakilishachama cha Conservative party,bwanaRosindell ni mbunge wa bunge la uingereza kupitia chama cha Conservative na piani mjumbe wa kamati y amambo ya nje ya bunge la Uingereza.Katika hotuba yakealisema nanukuu " expressed the commitment of the Conservative Party to support member parties and further continue the sponsorship of DUA programmes".

  Chama cha UP kutawala Liberia kwa muda wa miaka mitano tu,na sasa kimechokwa na wananchi,Makao makuuy achama hiki yamechomwa moto na wananchi miezi michache iliopiata na katikauchaguzi mkuu wa mwaka huu mgombea wake wa urais Sirleff-Johnson(ambaye ndieRaisi alieko madarakani)amepata asilimia 43 tu ya kura zidi ya asilimia 32 zaWinston Tubman ,ambaye alikua mgombea wachama cha upinzani cha Congress forDemocratic Change(CDC),Kutokana na chama tawala (UP) kushindwa kupata ushindiwa moja kwamoja na imebidi uchaguzi uludiwe mara ya pili leo tarehe 9 mwezi huu.

  Uchaguzi huu wa marudio umegubikwa na mashakamengi ikiwemo mwenyeketi wa tume ya uchaguzi kujiuzuru na lawama nyingi zauonevu kutoka na chama tawala kutumia nguvu ikiwewo police kuua waandamanji wanejuzi katika maandamano ya amanai yalioitishwa na vyama vya upinzania.Kutokanana uonevu huu vyama vyote saba vya upinzani vimejitoa katika uchaguzi nakumwacha mgombea wa chama cha UP kama mgombea pekee.

  Ikubukwe Kwa hofu yakushindwa chama hiki cha UP kilifanya juhudi nyingi kubadili sheria yauchaguzi na hasa sheria inayotaka mgombea wa uraisi ashinde kwa absolute majority,ikiwana maana lazima ashinde kwa kura zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa,chamahiki kilitaka sheria ibadiliswe ili mgombea ashinde kwa simple majority,ikiwa na maana mgombea hata akishinda kwa kura moja kama ilivyo hapa Tanzania natangazwa mshindi.

  Chama cha UP killiitisha kura maoni nchi nzima ili wananchi wapige kurakubadili sheria hii ya uchaguzi,wananchi wakapiga kura ya hapana zidi yao,nawakashindwa!!hawakuishia hapo mwenyekiti wa chama hiki cha UP ndugu Varney Sherman alikakata rufaa ili mahakama kuuingilie kuibadili sheria hii japo wananchi walitaka sheria hii ibaki ilivyo,napowakashindwa tena.

  Sasa wana Chadema tunajifunza nini?? chama hiki rafiki cha UP cha Liberia kimechukiwa na wananch ndani ya miaka mitano tu,kutokana na serahizizi ,Je Chadema ikiingia madarakani na sera na msingi hii ya ubepari ninikitatokea??
  watanzania watakaa kimya tu??

  Jamani amukeni,jifunzeni,fatilieni tusichukulia haya mambo ni rahisi sana kama tunakitakia mema cha chetu chaChadema,kama hakitabadili misingi na sera za ubepari na uhusiano wake na chama cha kibepari cha Conservative,nasema wazi Chadema haitadumu madarakanikamwe hata ikishinda 2015! MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  So what?
   
 3. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,536
  Trophy Points: 280
  Duh!! Jamaa weka basi hata paragraphs katika andiko lako; pangalia kazi yako ivutie na iwe rahisi kusomeka na kuifuatilia.
   
 4. k

  kulwa12 Senior Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Usilahisishe mambo magumu,tabia hiyo ndio imetufikisha hapa tulipo.
   
 5. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huo uchungu ndo umepelekea kuflow maneno tuuuuuuu bila hata mpangilio. Hebu pangailia maneno yako ili usomeke, kumbuka mpangilio mzuri wa maneno huvutia msomaji. Hukusoma uandishi wa insha darasa la tano kabla ya Mungai?
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  quantitative than qualitative

  i declare tis post as a mere crap
   
 7. k

  kulwa12 Senior Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ahsante mdau nimefanya hilo.
   
 8. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #8
  Nov 9, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,502
  Likes Received: 2,040
  Trophy Points: 280
  Hongera mkuu,umeongea mambo ya msing,acha wakutukane lakini sisi tulio na akili tunajifkiria zaid..BIG UP,YOUR A GREAT THINKER..
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mtu ambaye hajui kwamba chadema ni "Hoax" si mzalendo..tafuteni chama kingine kile ni kwa ajili wazungu na mabepari ..
   
 10. k

  kulwa12 Senior Member

  #10
  Nov 10, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .Mkuu nashukuru sana kwa mawazo yako,inasikitisha sana vijana wanaojiita wanaharakati na wenye uchungu wa nchii hii,inapokuakja wakati mjadili mambo ya ukweli wanatyoa matusi na kejeli badala ya kujibu hoja.Mi nilitegemea wajibu hoja sio kutoa majibu lahisi ya kejeli,ipo siku watu watakumbuka haya nilioandika.
   
 11. k

  kulwa12 Senior Member

  #11
  Nov 10, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nashukuru sana mdau nakuambia siku itafika watu wataona maana ya maneno nilioandika leo,inasikitisha sana tunaojiita wasomi na wanaharakati wa kuwakomboa wanachi masiki,tunajenga utamaduni wa kujibu hoja kwa matusi na maneno ya kejeli badala ya kujibu hoja kwa hoja,hivi kweli watu wenye akili zao watatupa kura?? Wengi ni thinkers sio washabiki tu bila kujau wanashabikia nini..
   
 12. k

  kulwa12 Senior Member

  #12
  Nov 10, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  i highly appreciate,for proving my words,insult and intimidation is best weapon for weak minds,don't insult respond to facts..
   
 13. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Mtoro wa shule ajifunze? magwanda wanamjuwa nani aliyetoroka shule.
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  story ndefu kumbe ungewezakufikisha kwa para mbili tu
   
 15. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hilo mbona linajulikana?..... Tatizo ni kuwa hata CCM kipo kwenye free trade. Ila angalau baadhi ya wana CCM wanaweza kuwaondoa kwenye uongozi wale wote wanaodai kutuletea azimio la Zanzibar, ambalo mpaka leo nimeshindwa kupata nyaraka zake (fake declaration).
  Just pick the less of two evils and move on!!
   
Loading...