CHADEMA tumuunge mkono W Malecela

Huyu nae si ndo wale wa Mtera ukoo mmoja na kibajaj? Watu wa Mtera bhana teh teh teh... natania tu jaman.
 
Huwezi kuamini sielewi kirefu cha M4C

Pole sana, hebu chunguza kwa makini hii logo hapa chini:

M4C.jpg
 
Mimi kama member wa huku jamvini na muunga mkono lakini si kwa uwana ccm wake.Namtakia kila la heri katika mapambano ya kugombea hiyo nafasi
 
Tangu lini mwanga na giza vikachangamana? Kwanza ajivue magamba, ajitakase, halafu tukamscan km yuko msafi halafu ndio tumuunge mkono kama tumejiridhisha ni msafi.

Ila kwa sasa mtoto wa nyoka ni nyoka tu. Hatudanganyiki ng'ooo
 
Pongezi kwa Kazi nzuri ya Arumeru, Kirumba, Lizaboni na Kiwira. William Malecela anajitaji kura za CDM awaze kuwa Mbunge wa EA. William ni mwanaCCM Aliye huko kimakosa anaweza simamia taifa kulikouCCM, ni msikivu na pamoja na mapungufu yote alonayo Mimi naona ni bora kuliko hao Tisa wengine nidhamu ya CCM. Sintoshangaa William siku moja akija CDM Chama makini aungane na wengine kuleta mabadiliko ya kweli. Ninaamini hata hoja za CDM baharia atazisimamia

Best wishes Malecela JNR

Rt Rev Masa

Sidhani kama anahitaji kura za CHADEMA kuwa Mbunge wa EA. Anachohitaji ni kutofungamana na kundi lolote (i.e. CCM Asili, CCM Mafisadi, CCM Wanaharakati) ndani ya chama ili aweze kupata uungwaji wa mkono toka makundi yote.
 
Mkuu Rev Masanilo una uhakika na huyu kijana, mbona yuko kwenye kambi hasi????? Utawezaje kumbatiza kwa moto wa CDM, uweze kumbadili???? Huyu jamaa na Nape kuna tofauti, akipata TCD atakumbuka kweli aliko toka?????
 
asijepata kichaa alichopata kibajaji akaanza kutukana ikawa aibu kwa CDM bure lol!!!!!! kudadadeki
 
PKP

U have a point! Wakichaguana wao kwa wao ndo hapo wataweka asiyefaa! Kumbuka huyu anawakilisha nchi kwenye bunge la EA

Mimi nafikiri tuweke utaifa mbele kwanza,kwa kua hawa watakaochaguliwa ni wabunge watakaoiwakilisha nchi kwenye EAC,ni lazima wote kama taifa tuwaangalie wao watakaofaa kwa hoja za msingi na wenye upeo ndio wakatuwakilishe huko,tungeomba yawekwe na majina ya hao wengine 8 mbali ya william ili nao tuwajue na tuwachambue!

Tusije tukapelekewa wabunge kama Lusinde kwy EAC,atakaedharauliwa na kuumia ni sisi kama taifa kwa kuwachagua wabunge vilaza kutuwakilisha,c.c.m tunawajua walivyo wa ajabu,wanaweza kumpitisha hata J.Komba (kama yumo) akatuwakilishe,huyo W.Malecella kama yeye ana uwezo wa kukabiliana na changamoto hizo kuliko wenzake,basi apigiwe chapuo!

Hizi hoja za kutaka kumuadhibu au kumtenga kwa kua tu baba yake aliwahi ku P.M zitakua hazina mashiko sana kama yeye William ana uwezo na vigezo kuliko hao wagombea wengine!maslahi ya taifa kwanza,pili rai yangu kwa W.Malecella ni kua kama anapigiwa chapuo na wana C.d.m kua yuko C.c.m kimakosa,kwa nini asitoke huko na kuja kufundwa C.d.m kwa ajili ya Mtera 2015?maana yule Lusinde ni dead mp
 
Mimi nategemea sana vijana mkiweza kuungana na kuondoa tofauti zenu kiitikadi ktk swala hili badala yake mkampata kijana mwenzenu kuwawakilisha ktk Jumuiya hii muhimu sana. William anaweza kabisa kuwa na mapungufu yake lakini tazameni the all picture kwa makini zaidi kwa sababu unatakiwa kumlinganisha William na wapinzani wake na sio kumtaka William awe kitu mbacho wewe ulitegemea kiwe..

Wakuu zangu uwe mwanachama wa Yanga au Simba utaitazama list na mchezaji wa timu yako kulingana na ushindani na sio kumtaka kila mchezaji awe kama Messi au Xavi ili aweze kuichezea timu yako, hutampata.
 
Sidhani kama anahitaji kura za CHADEMA kuwa Mbunge wa EA. Anachohitaji ni kutofungamana na kundi lolote (i.e. CCM Asili, CCM Mafisadi, CCM Wanaharakati) ndani ya chama ili aweze kupata uungwaji wa mkono toka makundi yote.
Anaweza kuiwakilisha ccm halafu at the same time "asifungamane na upande wowote"? kichama?
 
asijepata kichaa alichopata kibajaji akaanza kutukana ikawa aibu kwa CDM bure lol!!!!!! kudadadeki

Kibajaji ni elimu na malezi ndivyo vinamgharimu hivyo!darasa la saba kwa ubunge mmm this is too much!
 
Ret. Rev. MasaMimi naomba kupingana na wewe bro! Wewe na wengineo wanaoisaupport CDM wanajua dhahama ambayo CCM imezalisha katika nchi hii. Nakuhahakikishia ndani ya CCM kuna watu wasafi na waadilifu na wenye uwezo wa kufanya makubwa, its clear that hawapewi nafasi kwa sababu nia na dhamira zao zinapingana na mazoea ndani ya chama na serikali.

CCM imeharibu mfumo wa nchi hii kiasi kwamba kuna watu ndani ya serikali wameacha kuruhusu ubongo wa kufikiri na kutenda kama wanavyotakiwa kisheria simply because wanasiasa ndo wamekuwa watendaji!!

William anaweza kuwa kati ya wale niliosema hapo juu kuwa ni wasafi na wenye dhamira safi, tatizo likawa atashindwa "ku-serve" kwa sababu hata akipeleka ushauri na maamuzi yenye faida kwa nchi anajua yatapingwa tu, iwe kwa uwazi au mtu akaamua kuchimbia na kukaa kimya!!

Mimi nilitegemea watu ndani ya CCM wame na dhamira ya wazi kupingana na siasa na mfumo ndani ya chama chao kwa kuonyesha kutokukubaliana na mambo yao na kukaa nje ya duara lao, kujisafisha kwa uwazi kutokupendezwa na yanajiri ndani ya chama. Kuna watu kama Vincent Nyerere, ambaye pamoja na kuwa mtoto toka katika familia ya mmoja wa waanzilishi wa CCM, amesimama hadharani kupingana na CCM na kujiunga na chama chenye muelekeo wa kukomboa wananchi.

Kanini asifuate huko? Kwanini asionyeshe usafi wake kwa mtindo huo? nataka kugombea kupitia cham chao maana anajua atakachopata!!! Namuona William kama mtu anayetamani kuhamia nyumbani baada ya kuchoshwa na maisha ya kitumwa, ametumia "advantage" ya historia katika familia yake, na kuja kugombea huko huko!!!

Kwa hiyo hana tofauti na wale wale!!!! yeye agombee tuu maana magamba watapigiana kura wao kwa wao tu...
 
Anaweza kuiwakilisha ccm halafu at the same time "asifungamane na upande wowote"? kichama?
Jmushi1,
Tatizo sio William bali mfumo mzima wa kuchagua wabunge wetu wa EAC. Bora mara 100 wateuliwe na rais au Bunge moja kwa moja kuliko mfumo huu wa majina kupitishwa na CCM kisha tunaletewa watu ambao wamechaguliwa na chama hicho. Nilipitia mchakato mzima nikakuta wote wamevaa MAGWANDA ya kijani sasa utaweza vipi walaumu wao, nao siku hizi magwanda hivyo wanakuja taratibu kukubali ukweli.
 
Ndani ya chama kimoja wagombea 10? kwanini wasiwe wawili au watatu?au ndio ............?
 
Pongezi kwa Kazi nzuri ya Arumeru, Kirumba, Lizaboni na Kiwira. William Malecela anajitaji kura za CDM awaze kuwa Mbunge wa EA. William ni mwanaCCM Aliye huko kimakosa anaweza simamia taifa kulikouCCM, ni msikivu na pamoja na mapungufu yote alonayo Mimi naona ni bora kuliko hao Tisa wengine nidhamu ya CCM. Sintoshangaa William siku moja akija CDM Chama makini aungane na wengine kuleta mabadiliko ya kweli. Ninaamini hata hoja za CDM baharia atazisimamia

Best wishes Malecela JNR

Rt Rev Masa

Ukitumwa jambo fulani lipime kwanza, aibu yako aibu yake? Kama yuko magamba kimakosa mwambie arekebishe makosa kwanza kabla ya kuja mbele za JF, simple common sense.

I thought Retired Kumbe Tired Rev.
 
Rtd Rev Masa! Kumbe kupotea kote ilikuwa ni kwa ajili ya kujiandaa na kustaafu!!!!!! Nadhani tuna haja ya kumuunga mkono William, sawa ni mwana ccm lakini michango yake inamwonyesha ni wa namna gani> Pamoja sana
 
Back
Top Bottom