CHADEMA tumuunge mkono W Malecela

Pongezi kwa Kazi nzuri ya Arumeru, Kirumba, Lizaboni na Kiwira. William Malecela anajitaji kura za CDM awaze kuwa Mbunge wa EA. William ni mwanaCCM Aliye huko kimakosa anaweza simamia taifa kulikouCCM, ni msikivu na pamoja na mapungufu yote alonayo Mimi naona ni bora kuliko hao Tisa wengine nidhamu ya CCM. Sintoshangaa William siku moja akija CDM Chama makini aungane na wengine kuleta mabadiliko ya kweli. Ninaamini hata hoja za CDM baharia atazisimamia

Best wishes Malecela JNR

Rt Rev Masa

Rubbish!
Yupo CCM kimakosa?
Huu ni uchuro.
Hata kama amekutuma kumpigia kampen humu,tumia akili!
Au ndio multiple Id at work!
 
Wakuu !

Nimeangalia kwa mapana William yuko kimakosa sana CCM! Pamoja na mapungufu yake wabunge waCDM wamuunge mkono kuliko mCCM mwingine. Mwisho wa siku CDM lazima wachangue MCCM mmoja wapo Kati ya wale 9!

Huwezi honga mchungaji there is no price tag kwangu!

M4C

Acha utani Mkuu. Unless unaongelea Wiliam mwingine, na sio huyu mmwaga chakula cha kuku (pumba) hapa JF.
 
wakati wa kuvunja utamaduni wa kifalme wa kurithishana madaraka umefika. mm nashauri ni bora CDM kama haitasimamisha mgombea, iwapigie watoto wa maskini sio watoto wa viongozi wa ccm wastaafu

peoples power tupeni raha yaangusheni magamba
 
Kwa track record ipi ya uongozi ambayo ameitumikia nchi hii hadi tumwamini na kumpa nafasi muhimu hii ya kutuwakilisha? Kwa kumbukumbu za haraka haraka jamaa amekuwa busy akifungua matawi na mashina ya sisiemu huko US. Kwa faida na nani?
Kama ambavyo sisiemu wenyewe walishauri jina la mwl. JKN lisitumike vibaya kwenye majukwaa ya siasa, vijana kama akina WJSM wasitumie vibaya majina ya wazee wao.
 
Jmushi1,
Tatizo sio William bali mfumo mzima wa kuchagua wabunge wetu wa EAC. Bora mara 100 wateuliwe na rais au Bunge moja kwa moja kuliko mfumo huu wa majina kupitishwa na CCM kisha tunaletewa watu ambao wamechaguliwa na chama hicho. Nilipitia mchakato mzima nikakuta wote wamevaa MAGWANDA ya kijani sasa utaweza vipi walaumu wao, nao siku hizi magwanda hivyo wanakuja taratibu kukubali ukweli.

Ni kweli,
Lakini hivi umri wa kijana ni upi, maana kama sijakosea kuna mahala nimeona mwaka 70/71 alikuwa jkt kama ni kweli siamini kama bado kijana.
 
Pongezi kwa Kazi nzuri ya Arumeru, Kirumba, Lizaboni na Kiwira. William Malecela anajitaji kura za CDM awaze kuwa Mbunge wa EA. William ni mwanaCCM Aliye huko kimakosa anaweza simamia taifa kulikouCCM, ni msikivu na pamoja na mapungufu yote alonayo Mimi naona ni bora kuliko hao Tisa wengine nidhamu ya CCM. Sintoshangaa William siku moja akija CDM Chama makini aungane na wengine kuleta mabadiliko ya kweli. Ninaamini hata hoja za CDM baharia atazisimamia

Best wishes Malecela JNR

Rt Rev Masa

Inasikitisha sana!!!
 
Hivi unajifanya hujui kama Jakaya Kikwete ni Kijana?...

Nafahamu hata Wasira naye ni kijana. Mie nafikiri watuwekee kwanza ni nini anachokiamini ktk EAC, hapo wengi wanaweza kumuunga mkono, lakini hili la ujana ama mwana jf ama namfahamu naona haisaidii sana.
 
Kwani anapambana na kina nani?mbona wengine imekuwa siri kuwataja au mnaogopa atafunikwa!
 
Mkuu Masanilo kwa hiyo unamwombea William kura za kina Kiwia na Machemli pia.
 
Mbona mradi wa Jf unampa mpunga mzuri tu,asihangaike,ila bro piga jaramba mtoe City toilet pale mtera
 
Ok, kumbe keshafanya hivyo, tusubiri matokeo.

Matokeo ya kura za maoni za wabunge wa CCM ni haya hapa:

Adam Kimbisa (196), Dk Edmund Mndolwa (159), Siraju Kaboyonga (153), Bernard Mulunya (143), William Malecela (136), Elibariki Kingu (132), Evance Rweikiza (125), Mrisho Gambo (121) na Charles Makongoro Nyerere (113).

Assuming kwamba huo ndo mtaji alio nao kwa sasa, anaweza kuongezea kidogo za wale ambao wagombea wao hawakupita kwenye mchujo na pia akaongezea za kutoka kwa wabunge wa vyama vya upinzani. Kwa sababu kitakachofanyika baada ya hatua hii ni Bunge zima la wabunge wa CCM, CUF, CHADEMA, TLP, UDP na NCCR-Mageuzi watapiga kura ya kuchagua watu watatu kati ya hayo majina tisa.

Kuna tatizo ndani ya kundi la wabunge wa CCM, ukiangalia huo mtiririko wa kura kuna pattern fulani ambayo ninaiogopa. Mrisho Gambo ni mbaya wa EL kule jimbo la Arusha Mjini kwa Dr. Burian, yale makundi yanaendeleza minyukano mpaka hapa. Rafiki yangu Bwana Makongoro Nyerere nae anajulikana wazi kwamba ni mpinzani namba moja wa EL na alitaka sana EL atemwe ili CCM irudi mstarini.

Sinta-comment kitu kwa William Malecela, lakini ili aweze kushinda anahitaji sana kura za kutosha kutoka CHADEMA na vyama vingine vya upinzani. Akizikosa hizo, pattern ya kura inaweza kumsomba na maji.
 
Ni kweli,
Lakini hivi umri wa kijana ni upi, maana kama sijakosea kuna mahala nimeona mwaka 70/71 alikuwa jkt kama ni kweli siamini kama bado kijana.

Hukuangalia vyema, rudi tena ukasome vizuri. Walioenda JKT 70/71 sasa hivi watakuwa wako around 55 yrs old and above.
 
Hapa ndipo utaona zile kelele za CCM kumuweka Makinda uspika kwa minajili ya kutaka usawa wa jinsia zilikuwa geresha tu, nia ilikuwa kumuondoa Sitta.

Watu 9 hamna mwanamke hata mmoja!
 
Back
Top Bottom