CHADEMA Special Thread

Makamu Mwenyekiti Bara, Mhe. @HecheJohn , akizungumza katika Mkutano Mkuu Maalum Mkoa wa Simiyu leo.

Pia, Wazee wamemzawadia Mbuzi.

CHANGIA

M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ

NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo John Mnyika amesema kuwa chama hicho na Mwenyekiti wake Tundu Lissu mpaka hivi sasa hakijafanya mazungumzo yoyote na serikali huku akiipinga kauli iliyotolewa na Rais Samia Julai 30, 2026.

Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari leo Agosti 3, 2026 ameeleza kauli ya Rais Samia alipokuwa akizungumza na vyama vya siasa kuwa yupo mwenzao mmoja ambaye anaendelea kutafakari masharti haikihusu CHADEMA.

Mnyika amesisitiza kuwa walipomtafuta Lissu kufahamu kama amezungumza na serikali alikataa akisema mara baada ya kuzungumza na Rais Mstaafu wa Malawi Lazarus Chakwera hajazungumza na mtu yoyote hivyo amewataka viongozi wa CHADEMA kuendelea kubaki kwenye msimamo wao.

Ikumbukwe Julai 30, 2026 Rais Samia alikutana na viongozi wa vyama 18 vya siasa vyenye usajili wa kudumu na CHADEMA pekee ndiyo haikushiriki na moja ya kauli aliyotoa alisema "Kuna mwenzetu mmoja bado anaendelea kutafakari bado tunaendelea kupokea misukumo yake conditions zake matakwa yake ndiyo mambo yanavyoendeshwa kwenye nchi."
 
#BahariaNEWS Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amesema hayo Agosti 3, 2026 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, Makao Makuu ya chama, Mikocheni.

Julai 30, 2026, Rais Samia alisema, “Tuko vizuri kisiasa, lakini mwenzetu mmoja anaendelea kutafakari. Tunaendelea kupokea matakwa yake,” alipokutana na viongozi wa vyama 18 vya siasa vyenye usajili wa kudumu, huku CHADEMA pekee ikiwa haikushiriki.
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. John Heche, ameungana na wanachama na viongozi wa CHADEMA katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga kufuatilia mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami, pamoja na wenzake.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…