Chadema sio mtetezi wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema sio mtetezi wa Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GHIBUU, Mar 22, 2011.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,087
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  Unaposema tanzania it means unaijumuisha na zanzibar ambayo sasa hivi wengi ya watanganyika ndio wamegundua kuwa ni nchi yenye mipaka yake.

  Sasa hivi kuna mjadala wa katiba,katika mijadala inayokwenda Tanzania hapa zanzibar wao wanajadili muungano,kwa sababu katiba ya muungano imeingizwa ndani ya katiba ya tanganyika na kuwa kama vile magaragwe na kunde kuchanganya hujui ya muungano na yepi sio yamuungano.

  Before muungano wetu ulikuwa unaitwa jamuhuri ya watu wa tanganyika na zanzibar,ambapo wakati huo tanganyika ilikuwa na katiba yake,ila rais alokuwa wa muungano pia alikuwa rais wa tanganyika wakati rais wa zanzbar alikuwa makamo wa kwanza wa muungano.

  Kilicho fanyika Nyerere alifanya ujanja kuifuta Tanganyika ambayo nchi kamili iliyojipatia uhuru wake 1961,na kuita tanzania-Tan zania eti Tan imetoka katika tanganyika herufi za mwanzo tatu,na zania imetoka katika zanzibar sijui hapo nichambue vipi imetoka vipi katika zanzibar.

  Halafu kachukua katiba ya tanyanyika na kutia yale makubaliano ya muungano ( article of union) kuchanganya pamoja na kuongeza viraka na kuita katiba ya tanzania. Ni kichekesho.

  Nashangazwa sana kuona chadema wanapotamka neno tanzania wakisema kuwa wanatetea wakati unasema tanzania unaijumisha na zanzibar,na zanzibar sasa hivi wanajadili muungano,wanacho hitaji sasa hivi kujadiliwa muungano aidha kuleta serikali tatu kama ilivyokuwa hapo mwanzo tena ujadiliwe upya,au kuuvunja muungano.

  Kwa nini chadema wasitamke tanganyika wanaposema wanataka katiba mpya kwa sababu wanaposema tanzania inawajumuisha na zanzibar wakati hawatetei watanzania wote ? Ikiwa wao wanatetea watanzania wote basi pia wafike zanzibar kutetea maslahi yao wazanzibari ,na moja ya maslahi hayo wanayohitaji ni zanzibar kuwa nchi yenye mamlaka yake yote,kimataifa na kitaifa.

  Ikiwa kweli chadema munatetea watanzania pasi musitetee upande mmoja ambao ni tanzania bara,kwa jina jengine tanganyika.
   
 2. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,277
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kakwambia nani kama wanatetea upande mmoja?
  Halafu nyie mnaokurupuka na kuandika andika vitu visivyoeleweka sijui nani anawatuma? Kama kuna mtu anawatupa mwambieni ndio mnazidi kutupandisha chati,kwanza kubishana na nyie nisawa na kuisumbua akili yangu.
   
 3. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 281
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Umejitaidi ila "Craps"
  Kumbuka Tendwa mpaka asajili chama chako lazma uwe na wapigakura kote bara na visiwani kama sikosei bara kuna idadi yake na visiwani kuna idadi yake usipotimiza vyote chama chako akisajiliwi wanaojua embu tupe hizo takwimu kati ya bara na visiwani

  Mchangiaji kuwa makini usikurupuke.
   
 4. Gwota

  Gwota JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nani ni mtetezi wa tz?
   
 5. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,074
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama chama chenu kinapigania Maslahi ya nchi nzima Zanzibar ikiwemo, mbona mmepinga Waziwazi Wa Zanzibar kuungana kwa kuacha siasa za chuki kwa kuunda Serikali ya Umoja? jee, mnaunga mkono Zanzibar kubadilisha Katiba? Jee, chama chenu kinakubali Zanzibar ijiunge na OIC?, jee, Chama chenu kikotayari kutetea mafuta ya Zanzibar yaondolewe ktk Muungano? jee, mnakubali Zanzibar wawe na Mahakama ya Kadhi?

  Kama chama chako kinapinga yote hayo, utasemaje mnatetea Maslahi ya Wa TZ wote? hayo niliyokutajia ni sehemu ya Maslahi ya Watu wa Visiwani? unasemaje?
   
 6. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 2,901
  Likes Received: 1,552
  Trophy Points: 280
  Ni mtetezi wa babu yako,bibi yako, mama yako,ndugu zako etc. sasa hawa wote wanaangukia kundi gani?
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 9,814
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  Zanzibar, Zanzibar.................

  What is Zanzibar, by the way?
   
 8. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,664
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
 9. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Nashangaa mtu anatumia muda mwingi kuandika, lakini ukisoma unakuta crap! Hivi suala la katiba mpya ni la CHADEMA tu?
   
 10. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chadema ni wanafiki tu hawana jipya z zaidi ya kutetea tanganyika especially kanda ya ziwa na kaskaziini. Si watetezi wa Tanzania. Na sisi Znz hatuwatambui kama wao wasivyotutambua.
   
 11. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  makamba, tendwa, chiligati, lyatonga, sophia simba.
   
 12. bmx

  bmx Member

  #12
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm unayoishabikia haitaki oic, mahakama ya kadhi na mafuta yanatakiwa na muungano sembuse cdm hawatakubali vyote hivyo,,,mukitaka muendelee na cuf yenu,,
   
 13. N

  Nonda JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,169
  Likes Received: 1,823
  Trophy Points: 280
  Jerusalem.
  What is Zanzibar, by the way?

  You must be kidding,mkuu!
  The best way to know the answer..try this
  Take this name; Tanzania..then remove the -zan-
  Then what is left is the answer,
  Tan-zan-ia.......Tan....ia.
  Mkuu ..tunakosea njia...kama unajua historia ya Tanzania,vipi imezaliwa Tanzania basi huwezi kufanya utani huu unaofanya.
  Tanganyika iliungana na Zanzibar ndio leo tuna Tanzania. Jina la kisanii na utaifa wa kisanii. Vile vile nchi ya kisanii.

  Moves wanazofanya wazanzibari zinatusaidia tuirudishe Tanganyika ambayo tutasherehekea uhuru wake wa miaka 50.
  Are "you" not happy to get "our" Tanganyika back?
   
 14. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,584
  Likes Received: 783
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu anajiita Zubeda hapo juu, kila nikisoma comment yake naona element za Uzanzibar+Uislam, hivi hatuwezi kutenganisha vitu hivi? Yaani yeye hakuona maisha magumu ya watu wa Visiwani, hajaona elimu duni ya huko, hajaona sakata la umeme lililowaweka gizani miezi kadhaaa kipindi kile, wala hajaona tofauti ya maisha kati ya tajiri na maskini wa huko? Ila kaona kadhi, IOC na mafuta... Iko hivi, kama utalii wa Zanzibar haukumfaa masikini, hata hayo mafuta yatakuwa vivyo hivyo. Sucker....
   
Loading...