Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,904
Jamhuri ya muungano wa Tanzania Serikali huru ya Tanganyika (hii iko wapi?)
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda kuna umuhimu mkubwa kuanza kuuhoji muungano huu. Kuna kitu kilikosewa ama kilisahauliwa kwa makusudi na kamwe hakijawahi kuhojiwa popote!
Kwanza lazima tukubaliane hakuna uhuru wa Tanzania bali kuna uhuru wa Tanganyika.. Maana tuliungana tayari Tanganyika ikiwa huru
Baada ya muungano/muunganiko wa mataifa haya mawili nchi huru ya Tanganyika na nchi huru ya Zanzibar kukazaliwa taifa liitwalo TANZANIA.. Kwa maana ya kwamba serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar zilikufa rasmi na kuundwa serikali moja ya Tanzania iko wapi hii?
Hili kosa kubwa na la wazi ndio linatusumbua mpaka leo hii
Baada ya muungano wa haya mataifa mawili, taifa la Zanzibar likabaki na utambulisho wake kama taifa, lakini taifa la Tanganyika likaukana utambulisho wake asilia
Kwa taifa la Zanzibar kubaki na utambulisho wake kama taifa kukawapa nguvu ya kuunda serikali yao inayojulikana kama Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Kwa kuukana utambulisho wake asilia kama taifa, serikali ya Tanganyika ikakosa nguvu ya kuunda serikali yake ambayo ingeitwa serikali huru ya Tanganyika
Kilichotokea ninini sasa badala ya kuwa na serikali huru ya Tanganyika kukawa na serikali ya jamhuri ya Tanzania ambayo kwayo ni sehemu ya muungano..
Serikali ndio chombo cha kiutawala kinachoendesha nchi
Zanzibar ana faida mbili tayari ndani ya muungano
1. Utambulisho wake upo
2. Ana serikali yake
Kwa hiyo linapokuja swala la kuamua mambo yake ya ndani kiutawala.. Zanzibar ina chombo chake huru cha kufanya hivyo. Na linapokuja swala la kuamua mambo ya muungano ipo serikali ya Jamhuri ya muungano
Hapo ndipo Tanganyika alipopigwa bao la kisigino kwenye huu muungano.. Ndio maana leo hii watu wa Zanzibar wanaweza kuvuka maji na kuja kuwa viongozi Tanganyika kwa kofia ya muungano lakini mtanganyika kamwe hawezi kuvuka maji na kwenda kuwa kiongozi kule!
Muungano ni mzuri, kuungana kuna faida nyingi, USA ni muungano wa majimbo, UAE ni muungano wamajimbo pia.. Tunaziona faida za kuungana.. Lakini ni lazima uwe ni muunganiko wenye mizania sawa..
Suala la dpw litutoe sasa kwenye hii ganzi tuliyopigwa itutoke tuwe na mwanzo mpya sasa hasa kwenye huu muungano. Tungekuwa na utambulisho wetu wa Tanganyika ina maana tungekuwa na serikali yetu huru na hili suala la bandari lisingeamuliwa na serikali ya Muungano na kutufikisha hapa tulipofikia
Tuurejee mkataba wa muungano upya! Utambulisho wa Tanganyika uwepo ili tupate nguvu ya kuwa na serikali huru ya Tanganyika... Tukiliacha tena hili...TUTAHUKUMIWA NA WAKATI
Sent using Jamii Forums mobile app