CHADEMA si kimbilio la wasomi!


Kujidanganya nafsi kubaya sana BAK...wanaficha maradhi wanasumbiri kuumbuliwa na vifo tu...siku zinakuja.
 

Mkuu Zawadi, hivi hao unaowaita wasomi ni asilimia ngapi ya watanzania wote kwa ujumla wao?

Pili,hao unaowaita wasomi ni asilimia ngapi ya watanzania wenye sifa za kupiga kura?

Najua takwimu zinaweza kuwa za mbali kiasi naomba utupe japo makadirio itasaidia!

Nitashukuru ukijibu! sababu itatusaidia kuona kiasi cha ukombozi tutakaoutegemea kutoka kwenu wasomi wa nchi hii!
Asante sana!
 

Wewe hujui kwamba vijana wengi wasomi wapo vijiweni wamekosa kazi? Hivi unadhani vijana wote wanaomaliza vyuo vikuu wanaenda wapi? Ungefanya research kwanza kujua vijana wakimaliza vyuo vikuu wanaenda wapi kabla hujaja na conclusion kama hii. Pili kwani vijana wa vijiweni si watanzania? Acheni unafiki ninyi watu.
 
Nina digrii nilitoswa UVCCM Mtwara eti kwa sababu ni msomi!! CCM ni chama cha watu wasio na Elimu'""""""""
 
Mmmmmmm sina imani kuwa CDM wataleta shibe. Ninachoona mimi, hawa CHADEMA wataongeza njaa + vita. Mwenyewe jaza kipi ni afadhali.
Bora vita na njaa ya haki kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa mwanadamu! Period!
 
Dah! yaani kama wasomi wa ccm ndio wewe mmojawapo basi ccm hakuna wasomi, kwa jinsi tu ulivyoandika haya maneno yako unaonesha ni jinsi gani elimu yako haijakukomboa hata kidogo, kwanza haupo makini, pili hujui hata kuandika kwa maana unakoesa kosea , sijui hukupitia darasa la kwanza maana. Siku nyingine jipange usikurupuke kijana.
 
Hoja finyu kama hii dawa yake ni kuitosa jumla,vinginevyo na sisi tutaonekana wapuuzi kama yeye
 

Hii kweli ni kali
1. Hao vijana wa darasa la saba/vijiweni sio watanzania?
2.Aliyewafikisha hapo ni nani kama sio chama tawala cha enzi za mkoloni??
3.Vijana wa vijiweni hawana haki ya kuwakilishwa?
4.Ushajua idadi ya vijana waliopo vijiweni compared na walio na ajira maalumu.???
5.CCM mna safari ndefu sana....mlishawahi kusema kura za wafanyakazi hamzihitaji...na sasa za vijana wa vijiweni
 

poa tu, wala sioni shida hapo iko wapi, hawajasoma ila ni waelewa. hao waliosoma wametufikisha wapi? hao madaktari wa falsafa? issue ipo hapo, na mbona hao unaosema wasomi wanang'ang'ana kutafuta vyeti vya awali hadi vya juu na kufoji n.k saa hizi? au unafikiri kuna siri? hizo safu zote tunazijua, hata viwango na uelewa wao, ikiwa kuna perfomance hamna tatizo, lakini ipo? safari hii tutawapa hao wasio na elimu ( according to you), tumechoka na sifa zisizo na tija.
 

wewe huenda hukwenda kabisa shule kwa upeo mdogo ulouonyesha hapa .utafiti wako ulofanya hauna data.hivi kuna majimbo yepi tz yenye wasomi wengi?kawe,ubungo,mwanza,arusha mjini,mbeya mjini,moshi mjini wanaongoza chama gani?pumba weye
 

nilikuwa sijui kumbe hata maandiko yanasupport CHADEMA
hehehe CHADEMA haikja kwa wenyeshibe(CCM) bali kwa wenye njaa (watanzania) hii ni habari njema kweli Mungu yu mwema
 
Zawadi na HAMY D,mnalipwa kiasi gani? Je wanao leta vurugu ni kweli CHADEMA au CHAMA CHENU KITUKUFU?

Hao uliowasema wakaa vijiweni,wavuta unga au madawa ya Kulevya ambao ni failures wa form four na form six ilikuwa ndoto kufika.

Yaani kwa kifupi tumeishia darasa la saba,ndio tuliomwangusha Mbunge wa CCM Mbeya mjini,pamoja na kung'ang'ania sana na hayo uliyoyaongea ndio maneno aliyotoa Mbunge huyo kwa tiketi ya CCM.

Hata wachimba makaburi kumbuka ndio sisi tusiokwenda shule na ndio tunaoumia na kuporomoka kwa hii shilingi yetu,na nyie wachache kujilimbikia mali nje ya nchi kwa kisingizio cha wivu wa kike.

Tuachane na Chadema ndugu zangu nyinyi fikirieni mbali zaidi shilingi mbili hizi unazopewa leo zitakuwa kaburi lako kesho.Poleni sana.

Kumbukeni hata siye ambao shule hatujaenda tunaakili japo ya kutambua mema na mabaya,msitudharau,ndio tutakao wachimbia makaburi yenu siku mkiondoka dunia hii na mkiacha mali zote mlizotudhulumu siye wa vijiweni.
 
Waacheni wafu wawazike wafu wenzao hivi humu JF tu mnapata picha gani nyie CCM mbona hamsomi alama za nyakati kama tulio JF ni wa kijiweni subiri muone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…