Mkuu kwanza kabisa nikupongeze kwa tafiti yako, maana naamini umetumia muda mwingi, rasilimali na nguvu katika kufanikisha tafiti hii, hapa napenda wachangiaji wasianze kuulizia methodology ulioitumia maana vitu vingine vipo wazi tu.
Kwanza napenda kuunga mkono hoja yako kuwa chadema sio kimbilio la wasomi bali ni kimbilio la failures. Hii nimekuwa nikiishuhudia mara kwa mara kwa kuangalia wanachama wengi wa chadema katika eneo ninaloishi, nikagundua wengi ni MATEJA, WEZI, VIJANA WA VIJIWENI. Nikaenda mbali zaidi nikagundua wengine wanaoiunga mkono chadema ni hawa wakimbizi ambao wanaishi hapa nchini kinyume na sheria. Makundi haya ya watu mara nyingi hawatambuliki katika daftari la kudumu la wapiga kura, kwa maana hawana kadi rasmi ya mpiga kura ambapo kimsingi hawawezi kutekeleza haki ya kupiga kura.
Sikuishia hapo, nikaanza kuangalia vyuo vikuu kama vile UDSM, Ardhi University, MUHAS (Muhimbili), Mzumbe na SUA n.k pia na kwenye taasisi za elimu ya juu kama vile IFM, IAA, TIA na CBE n.k nikagundua CCM ina wanachama wengi sana tena wale viongozi wa serikali za wanafunzi ni wakereketwa wa chama chetu hiki imara na madhubuti.
Hapa nikafanya hitimisho ya kwamba, sababu kubwa ya CCM kuibuka kidedea kila mwaka tangu mfumo huu wa vyama vingi kuanzishwa ni pale ilivyoamua kuweka vigezo na masharti katika upatikanaji wa wanachama wao.
Vigezo hivyo na masharti vinataka watu wazalendo na taifa lao, watu waadilifu, watu wenye kujishughulisha na wenye utayari wa kujitoa kufanya kazi za kijamii (hatutaki kabisa wavivu, wazembe na mazezeta). Ukiangalia hapo utaona wasomi na wananchi wanaojituma kama wafanyakazi na wakulima ndio wanakidhi hivyo vigezo na masharti, makundi haya yana kadi ya mpiga kura na ndio wapiga kura wengi, kimsingi kundi hili ndilo linatupa CCM ushindi wa kishindo dhidi ya wapinzani uchwara ambao tunaona wengi ni waroho wa madaraka.
Ndugu yangu mwananchi mwenzangu wa Tanzania, kaa hapo ulipo utafakari kwa nafasi uliyonayo katika jamii, je unastahili kuwa mahala gani kiitikadi? Maamuzi ni yako lakini ukumbuke yanaathiri taifa letu, fanya maamuzi sahihi kwa ustawi mzuri wa nchi yetu.