Pengine unajiliwaza kwa kudhani kuwa CHADEMA imekumbatia wanachama wa madaraja yote TZ. Ikiwa viongozi wa juu wa CDM wamekubali kuwa Chama hiki hakifahamiki Vijijini, ni vipi unadiriki kuwakumbatia wakulima wakati huko hamfahamiki. Au ulimaana wakulima wadogpowadogo wa mijini. Any way swala hilo nawaachia wenzangu watafakari.
Wabunge wa CHADEMA hawana moja. Kumbuka mlipoamua kuondoka Bungeni, Zitto Kabwe alikuwa na lake jingine. Wabunge wengi wa CDM wanaburuzwa na majuaji 5 tu. Hawa wataloamua hakuna kupinga, ukipinga unafukuzwa na kuitwa msaliti. Kuwa na mawazo tofauti ndani ya CHADEMA ina maana kuwa wewe ni CCM. UDIKITETA ULIOJE!!
Nakuelewa kuwa mzee mwenye raha, si unakumbuka sababu kubwa iliyomfanya Mh Sitta akatae ombi lenu la kuhamia chama chenu na kupewa offa ya kugombea Urais. Mh Sitta alisema, Uongozi ndani ya CDM unatolewa kikanda. Na kanda utokayo Mheshimiwa ndio kanda yenye neema CDM..
"Hakuna kulala, mpaka kieleweke" Sentensi hii ina maana, maandamano, Fitina, Uhasama, Danganya, Susia bunge kama mlivyotikisha kiberiti bungeni baada ya uchaguzi na tukio la Arusha. Kifupi maana yake ni vita.