CHADEMA: Serikali ilaani vurugu Ivory Coast | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Serikali ilaani vurugu Ivory Coast

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Dec 19, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  CHADEMA: Serikali ilaani vurugu Ivory Coast


  na Juma Kasesa


  [​IMG] CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka serikali kulaani hadharani matukio ya uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya demokrasia ya kimataifa unaofanywa na Rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo na wafuasi wake nchini humo.
  Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa ya chama hicho ilisema, Rais Jakaya Kikwete anatakiwa kutamka hadharani kumtambua Alassane Ouattara kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo na kulaani vitendo vinavyofanywa na Gbagbo na wafuasi wake.
  “Inashangaza kwamba wakati Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU) na serikali za nchi mbalimbali ndani na nje ya Afrika zimetoa matamko ya wazi serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya diplomasia ya kimya.
  “Hii ni tofauti kabisa na wakati Mwalimu Nyerere ambapo Tanzania ilikuwa mstari wa mbele na kutoa misimamo ya wazi ya kukemea vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
  Aidha, taarifa hiyo ilieleza CHADEMA inatambua kwamba Rais Kikwete alizungumzia kidogo matatizo ya Ivory Coast wakati akihutubia Mkutano wa Kimataifa wa Amani katika eneo la Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika hivi karibuni nchini Zambia.
  Katika mkutano huo Rais Kikwete alieleza kwamba suala la Ivory Coast linashughulikiwa na mikono salama na akaonyesha matumaini yake kwamba pande mbili zenye mgogoro zitafikia makubaliano.
  “Kauli hii ya Rais Kikwete inalea vitendo vya ukiukwaji wa misingi ya demokrasia vinavyofanywa na Laurent Gbagbo na wafuasi wake kwa kuwa inatoa fursa kwa mgombea ambaye taasisi zote huru zimetamka kuwa ameshindwa katika uchaguzi kuanza majadiliano na aliyeshinda badala ya kumpisha katika uongozi wa nchi,” ilieleza taarifa hiyo.
  Aidha, taarifa hiyo ilisema serikali ya Tanzania inatakiwa kueleza msimamo wake kwa uwazi, ili kuondoa mashaka kwamba ukimya wake unatokana na Rais Kikwete kukosa uhalali wa kimaadili wa kukemea vitendo vya ukiukwaji wa demokrasia na mchakato wa uchaguzi uliomuingiza madarakani kuhojiwa kutokana na tuhuma za matokeo ‘kuchakachuliwa’ katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
   
 2. P

  Pax JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Safi sana hii, anaogopa ile verse ya kitabu kitakatifu inayosema kabla ya kutoa kibanzi kwenye jicho la mwenzio kwanza uondoe boriti kwenye jicho lako. Raisi anayeongoza taifa kwa hila katika chaguzi hawezi kukemea mwenzie. Nini kilichotokea haoa Tanzania kwani kinacholeta tofauti na Ivory Cost kwani, wabunge wangapi wameibiwa kura mchana kweupe kwa nguvu? Ole wao wafanyao haya, mwisho wao utakuwa wa kusaga meno
   
 3. C

  Chesty JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2010
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,350
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  He doesnt have moral authority to do that.
   
 4. c

  chumakipate Member

  #4
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hiki ni bonge la kitanzi watajioondoaje,shingo imebana
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Sijui watakemea kilichotokea huko Ivorycoast ili waonekane wanafiki...
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  JK hawezi kutoa tamko la namna hiyo bila ya kujiuma midomo, kwani hadi sasa chama chake kinaendeleza unporaji, au tuseme unyang'anyi wa halmashauri mbali mbali hapa nchini. Labda akishamaliza shughuli hiyo ndiyo atatamka.
   
 7. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Kiranja mkuu hana amani moyoni. Anajua mwenzie akinyolewa,tia maji kichwani. Siku ya uhuru akatoroka na hotuba kwenye mfuko wa koti itakuwa vp atoe tamko zito kama ilo. Hana ujanja!
   
 8. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #8
  Dec 19, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Hata weza kutamka lolote maana anajua kuwa atapa kigugumizi hasa kuhusiana na uporaji wa halmashauri unaofanywa na chama chake rejea uchaguzi wa mayor wa Arusha na Mwanza.

  Hii inaonyehsa kukosa ujasiri wa kukemea maswala ambayo chama chake nacho kimefauta mkondo huohuo.
   
 9. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli ni ndoto kali sana. Ila kwa unafiki wa viongozi wetu their do not have such a thing called moral authority. They are typical immoral and out of their upuuzi utasikia wanalaani wakati na wao wamepitia mlango huo huo.
   
 10. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Laurent Gbagbo na Jakaya Kikwete ni sawa na idential twins!!wote ni wezi wa kura na wizi wao unafanana!!
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hivi CHADEMA mnaitambua serikali ya Jakaya Kikwete ? Nawashangaa sana kwa ombi hili zidi ya serikali ya Mheshimiwa Jakaya. Inaelekea kabisa hamjui mtendalo.
   
 12. N

  Njaare JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mh! Akitamta lolote kuhusu Ivory coast nitaamini kuwa nyani haoni kundule! Achilia mbali ya uchaguzi mkuu ulopita lakini hili la Arusha litamsuta.
   
 13. n

  niweze JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Si Tunaona Jinsi Gani Tanzania Inashindwa Kujihusisha na Maswala ya Afrika? JK Anaweza Kumwambia Dikteta Gbagbo Chochote? Alichokifanya Huyu Gbagbo Si Ndicho Kikwete Kafanya? Utakuwa Ujinga na Mimi Namshauri JK Akae Kimya Kama Anavyofanya It's Good Strategy. Hata Mugabe, Museven, Kibaki, Mubarak Tunawaona Wapo Kimya Wanajua Wanachokifanya Nchini Kwao. JK Amechukua Exactly Playbook ya Gbagbo na Mugabe Kuongoza Tanzania na Sita Shangaa JK Anawasiliana na Mugabe kwa Simu Kila Siku. Mpaka Leo Zimbabwe Hawana Katiba na Tanzania CCM Wanasema Hawataki Katiba, Imetoka Wapi?
   
 14. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  ...we kilaza mwiba kunywa maziwa fasta utapike hiyo sumu inayokuua ya propaganda za magazeti ya RA na Uhuru et al kwamba CDM hawamtambui Rais wa JMT!!!! Rais anatambulika kisheria lakini mchakato uliomuweka madarakani unatufanya tumuone illigitimate Presidaa. Kwanza JK akemee kitendo cha kumwaga damu ya Hon. G. Lema na kupora halmashauri ya arusha mjini.
   
Loading...