Averos
JF-Expert Member
- Aug 6, 2010
- 994
- 703
mzee slaa anaorodha ya watu ambao alishapanga kuwaua akiwa rais sasa kiongozi wa namna hii atatufikisha wapi.
Yakhe kama hiyo orodha unayo niangalie kama nipo. Wako mpendwa . Mwigilulati Nchembito
mzee slaa anaorodha ya watu ambao alishapanga kuwaua akiwa rais sasa kiongozi wa namna hii atatufikisha wapi.
mzee slaa anaorodha ya watu ambao alishapanga kuwaua akiwa rais sasa kiongozi wa namna hii atatufikisha wapi.
hiyo ya kwako na wajomba zako mimi nlikuwa namaanisha huyu mzee wetu aliyeanguka bafuni kule mwanza wkt ana pump hadi akavunjika mkono, si ndio aliyevunja ndoa ya mushu...mbu..si. Huku akitelekeza watoto wake na mke wake.
Mtakalia Propaganda za kijinga wenzenu CHADEMA wanasonga mbele nyie mnajirudisha nyuma kwa mambo ya kijinga yasiyo na tija badala ya kutekeleza ILANI yenu, Hivi naomba nikuulize vile vipindi vya kwenye TV vya kuonyesha mafanikio ya Serikali ya awamu ya Nne vimeishia wapi?ni kitu cha hatari sana kuona mtu anashabikia kutaka chadema itawale,chadema wao wenyewe wameshindwa kujiongoza kila kukicha wanawindana kuuwana imefika hatua wanataka kumuuwa hata mama yake zito.
mkuu na wewe unajua ni ndoa ngapi mkuu wa kaya amezivunja hadi sasa????
Kwa hiyo huko kijijini kwenu wanaafikiana na magaidi kumbe...ni bukoba mjini au wapi hapo mana waasisi wa ugaidi chadema ni bukoba people
mzee slaa anaorodha ya watu ambao alishapanga kuwaua akiwa rais sasa kiongozi wa namna hii atatufikisha wapi.
Hiyo heading ya thred imenichefua na kuniharibia kabisa siku
Mungi ubarikiwe sanaccm kuwepo madarakani mpaka leo ni kwa bahati mbaya sana. Hili lichama lilitakiwa kuzikwa zamani sana.......... Washukuru.watamzania wana huruma ya ajabu sana
binafsi naamini sasa CDM juhudi wanazofanya ni kuongeza asilimia ya kura tu kutafuta ushindi wa kishindo, lakini uchaguzi ungfanyika leo, hata CCM waibe kura 1,000,000 bado CDM itashinda kwa 60%.Habari wanajamii,
Katika muda wa miaka 3 (2010-2013) nimekuwa nikifuatilia siasa za CHADEMA VS CCM kwa karibu. Ktk uchaguzi wa 2010, CHADEMA ilionekana kuungwa mkono zaidi mijini huku CCM ikiungwa mkono zaidi vijijini.
Baada ya uchaguzi wa 2010, nafikiri chadema wamegundua kuwa kuna haja ya kujikita zaidi vijijini hasa baada ya kuanzisha kanda za kiutawala ambazo hutoa nafasi zaidi kwa wananchi kuwajibika kukitangaza chama kwa rika zote.
Nimepata kutembelea vijiji kadhaa ambavyo vimekuwa chini ya CCM kwa muda mrefu, watu wanaonekana kuchoka na CCM. Kila unayemkuta anakwambia CCM hawataona tena kura zao kuanzia mjumbe wa x10. Wanaona kupigia kura au kugombea kupitia CCM ni kujidhalilisha. Hawana habari kabisa na ugaidi wa CHADEMA, wanakwambia tunawapa kura hivyohivyo walivyo! Acha nao waongoze!
Wengi wanashauri wafikiwe na viongozi wa chama kitaifa hasa Dr Silaa, Mbowe, Zitto, Lisu, Lema, Msigwa, n.k ili kubadilishana mawazo kabla ya kuchukua madaraka 2015 na wanamwamini sana Dr Silaa kama rais wa ajaye. Najua wapo watakaokuwa very aggressive kwangu lkn hii ndio hali halisi kwa sasa.
Siasa za chadema ni kubwa sana mtandaoni tena hapa jf. Huko kwenye field wanaokishabikia ni wahuni wahuni tu
Kwa hiyo huko kijijini kwenu wanaafikiana na magaidi kumbe...ni bukoba mjini au wapi hapo mana waasisi wa ugaidi chadema ni bukoba people
ugumu wa chadema kuchukua nchi huu hapa
ccm ina wanachama zaidi ya mil5 cdm ina wanachama zaidi ya laki5 na si zaidi ya mil1 wenye kadi sio wapiga mayowe ambao hawako kuacha kazi zao kwenda kupiga kura
mtaji mkubwa wa wapiga kura uliwah kujiuliza kuna walimu wangapi tz na hao walimu wanalea familia za watu wangapi majumbani kupitia pesa za ccm je uliwah kujiuliza kuna askari wangapi wa tz wanajesh magereza polisi tanapa migambo usalama wa taifa wangpa na ukubwa wa familia wanazotegemea fedha za ccm je uliwah kujiuliza kuna watumish wangapi wa mahakama madktari manesi wauguzi watumish wa ofisi za serikali na vyombo vyake kama bandari viwanja wa ndege nk je uliwah kujiuliza mtaani kwako kuna wajumbe wa ngapi wa nyumba kumi wa ccm na familia zao wanaweza kukipa kura cdm wakitose chama cha baba anaepata pesa ya ugali wa kura kutoka kwao madiwani wenyekiti wa kata mafisa kilimo nk na ukubwa wa familia zao
turudi kwenye mahesabu mil5 ya ccm kadiria zipatikane kura 3mil tu kadiria watumish wa serikali 2 mil waipigie ccm jumlisha na ndugu zao1 au 2 mil hizi ni kura za uhakika kwa ccm vp kwa cdm ya wanachama laki 5 itaweza kushindana nadhani kwenye ubunge ni rahisi lakini uraisi sababu ubunge unazungumzia maeneo machache ambayo mengine hayana watumish weng wa government hata kwa dr slaa kupata kura 2.5mil ni ushindi mkubwa sababu haijawah kutokea katika historia ya tz watz tuongeze idadi ya wabunge ili iwe rahisi kutoa maamuzi tofauti kwa serikali kwani ndio nyepesi ya kufanya mapinduzi ya amani ya kisiasa
mkuu umeandika ukweli na umetoa uchambuzi wa kitaalamu wa mafanikio ya CDM, mimi naona kuna jambo moja CDM hawajafanikiwa kulifanya HARAKATI ZA KIMAPINDUZI coz sina hakika kama CCM wataondoka madarakan kirahisi, ndio maana nakubaliana na CHE ' GUEVARA anaposema "cruel leaders are replaced only to have new leaders turn cruel" mwisho wa kunukuuPamoja na kwamba uzi wako umekaa kimahaba zaidi kwa CHADEMA,kuna ukweli ndani yake, ngoja nionyeshe kwa ufupi ni kwa namna gani
- CHADEMA walijivua gamba la kuendelea kuwa chama kinachoonekana kuwa na nguvu wakati wa uchaguzi mkuu. Walianzisha siasa za barabarani au siasa za uanaharakati- kwa kiingereza wanaita ni "activist politics". Hili liliwafanya kuwa barabarani muda wote katika operation zilizoitwa majina kama sangara, m4c na kuwafanya kujiimarisha vijijini. CCM walipiga kelele sana kwamba wao CDM wanafanya siasa za uanaharakati na kuwa hazifai kwa nchi. Walizipinga kwa sababu wanajuwa hatari yake! Kimsingi siasa za CHADEMA zilikuwa ni zawadi kutoka CCM. Yaani CCM ndio waliozalisha siasa hizi baada ya kuacha misingi yao,kumtelekeza mkulima na mfanyakazi ambaye awali ndio walikuwa wenye CCM. Viongozi wa CCM walikiteka chama, wao na mawakala wao wakajigeuza na kuwa "wakoloni weusi". Kupitia kilichoitwa ubinafsishaji wakajimilikisha zilizokuwa mali zilizokuwa za umma na wakaanza kushirikiana na "wakoloni weupe" waliorudi kwa mlango wa nyuma kama "investors. Makosa haya ya CCM na mengine ambayo yameendelea kufanywa katika mambo ya msingi ndio chimbuko la siasa za uanaharakati zinazoendeshwa na CHADEMA hivi sasa. Hapa ndipo siasa za second African Liberation struggle zilipoanza na zilikuwa tu zinamsubiri ni nani aweze kuziendesha. Kutokana na historia ya CCM ya Africa Liberation Struggle,CCM ndio ilipaswa kuendesha siasa hizi za CHADEMA kuelekea katika kupata ukombozi wa pili wa bara la Afrika, kama alivyopata kusema Abdularmani Babu kwamba "Tanzania/CCM was constantly ahead of events" kwa maana ya mazingira ya ukombozi wa bara la afrika. Lakini kwa kuwa CCM waliiacha misingi yao na kuinajisi ile nafasi yao sasa wanajikuta wako pembeni na CHADEMA imesimama pale ilipiostahili kusimama CCM kwa sababu ya historia yake iliyotukuka. Hii imezaa mweweseko mkubwa sana. Mbaya zaidi ni kwamba uelewa wa mwananchi wa kawaida umekuwa na sasa unapewa kasi na makali na hizo siasa za CHADEMA. Inawezekana hayo CHADEMA wanayosema yasifike hata nusu ya ukweli ila kama watoto wako wananjaa tangu jana halafu kwa jirani kuna msosi ni lazima watatoroka waende huko kula.
- Ukiangalia namna CCM wanavyofanya mambo hivi sasa ni kama mtu aliyekunywa mvinyo ukamzidi. Matusi,kebehi,vijembe,mipasho na uongo ndio vimetawala. Hivi ndivyo vitendo ambavyo wana JF na wanamitandao mingine wanalaumiwa na mleta uzi ya kuwa vinaelekezwa kwa CCM na au viongozi wa CCM wanapoleta nyuzi zenye hoja za kujibu hoja na au kashafa. Ukistaajabu ya musa....
- Kuanzia mwezi wa pili(inawezekana ikawa nyuma kidogo) hapa JF kumekuwa na "movement" ya kundi kubwa la watu waliojiunga na ambao nyuzi zao zinaleta ama hoja na kuzijibu ama linajibu hoja zinayoihusu CCM au CHADEMA
- Naona kama 2 na 3 ni "desperate move" ya kutaka kurekebisha hali fulani aidha kwa CCM au CHADEMA. Je katika hali ya sasa kwa kuiangalia na lensi ya siasa za uanaharakati je ni nani kati ya CHADEMA na CCM anayepaswa kuwa "desperate?" Waingereza wanasema "desperate situation calls for desperate action"