Wandungu-
Naomba niseme hivi, kweli nyani haoni kundule. Kipindi cha nyuma ndugu zetu wa CDM waliwashambulia sana ndugu zetu waCUF kwa kuingia katika serikali ya umoja na CCM kule Zanzibar. CUF waliitwa kila aina ya majina mpaka ikapelekea CDM kukataa kuungana nao mjengoni. Sasa mimi najiuliza, kwa wakati ule kosa la CUF lilikuwa ni lipi hasa ukilinganisha na yanaotokea leo?
Hebu sasa turudi yanayotokea leo. Kwa wakati huu tunaona wimbi la MAKAPI ya CCM yakitoka CCM na kuja CDM. Cha ajabu kwa wale MAKAPI vigogo, wengi wao sifa zao walishazidekia matapishi siku nyingi, hawa ni kama wakina Mahanga, Mgenja, Guninita, Ole Medeye n.k. watu hawa hawana thamani kisiasa. Sasa najiuliza, kwa wimbi hili je CDM sio ndio inageuka kuwa CCM B kwakujaza wanacham mareject ya CCM? Kati ya dhambi mbaya iliyofanywa na CUF na hii ya CDM, ipi kweli inafaa kukifananisha chama kimoja wapo na CCM B?
Pamoja na vigogo Makapi, wafuasi wengine wamehama kwasababu walishindwa kwenye kura za maoni. Hili si ajabu kwani hata safari ya Dr. Slaa ilianzia hapo kuja CDM. Sasa najiuliza, ukichanganya na uchafu wa Vigogo waliotimkia CDM, hivi CDM hawadhani ni faida kwa CCM kwa watu hawa kujitoa, zaidi ya CDM kuwapata? Kwa mimi binafsi ningeogopa kama nikisikia kada kama Mwapachu (nimechukua mfano wake kwani yeye ni team Lowasa damu) ameondoka, kwani yeye anaheshima yake nzuri tu. Sio hao wakina Mgenja na Mahanga. Unajua oil chafu kweli inaweza kuwa na faida yake, ila sasa ikiwa chafu sana inakuwa haina nguvu tena yakuua wadudu kwenye mbao.
CDM wasipoaangalia watakuja kujikuta Makapi wote wamehamia kwao-na haita kuwa na tofauti kimuundo na kimtazamo kama CCM. (mfano mzuri tumeona leo Mgenja anahama chama huku akiwa na vazi la CCM).
KOSA KUBWA LA CDM NI KUWA KILA MWANACHAMA/MSHABIKI WAKE NI MJUAJI. Kuanzia viongozi wake, mashabiki wake mpaka Makapi waliowasajili. Mfano tuu mdogo huku JF, watu wanapiga kelele za mapema wakati mechi yenyewe bado. Naomba niseme kwa kingereza, IT DOESN'T MATTER HOW YOU START THE RACE-WHAT MATTERS IS HOW YOU FINISH IT.
Mchuano wa Magufuli na Lowasa nauona ni kama Mayweather na Pacquaio. Nyie wote ni watu wazima mnajua mshindi ni nani. TEAM MONEY. Purukushani zote za CDM kama tunavoziona sasa hivi na kama alizozionyesha Pacquaio hazitawaletea tija.