2gezaWeCan
Member
- May 1, 2015
- 84
- 21
si mlisema mmetoka Dodoma mkiwa wamoja!?
sasa unalialia nn?
sasa unalialia nn?
Wandungu-
Naomba niseme hivi, kweli nyani haoni kundule. Kipindi cha nyuma ndugu zetu wa CDM waliwashambulia sana ndugu zetu waCUF kwa kuingia katika serikali ya umoja na CCM kule Zanzibar. CUF waliitwa kila aina ya majina mpaka ikapelekea CDM kukataa kuungana nao mjengoni. Sasa mimi najiuliza, kwa wakati ule kosa la CUF lilikuwa ni lipi hasa ukilinganisha na yanaotokea leo?
Hebu sasa turudi yanayotokea leo. Kwa wakati huu tunaona wimbi la MAKAPI ya CCM yakitoka CCM na kuja CDM. Cha ajabu kwa wale MAKAPI vigogo, wengi wao sifa zao walishazidekia matapishi siku nyingi, hawa ni kama wakina Mahanga, Mgenja, Guninita, Ole Medeye n.k. watu hawa hawana thamani kisiasa. Sasa najiuliza, kwa wimbi hili je CDM sio ndio inageuka kuwa CCM B kwakujaza wanacham mareject ya CCM? Kati ya dhambi mbaya iliyofanywa na CUF na hii ya CDM, ipi kweli inafaa kukifananisha chama kimoja wapo na CCM B?
Pamoja na vigogo Makapi, wafuasi wengine wamehama kwasababu walishindwa kwenye kura za maoni. Hili si ajabu kwani hata safari ya Dr. Slaa ilianzia hapo kuja CDM. Sasa najiuliza, ukichanganya na uchafu wa Vigogo waliotimkia CDM, hivi CDM hawadhani ni faida kwa CCM kwa watu hawa kujitoa, zaidi ya CDM kuwapata? Kwa mimi binafsi ningeogopa kama nikisikia kada kama Mwapachu (nimechukua mfano wake kwani yeye ni team Lowasa damu) ameondoka, kwani yeye anaheshima yake nzuri tu. Sio hao wakina Mgenja na Mahanga. Unajua oil chafu kweli inaweza kuwa na faida yake, ila sasa ikiwa chafu sana inakuwa haina nguvu tena yakuua wadudu kwenye mbao.
CDM wasipoaangalia watakuja kujikuta Makapi wote wamehamia kwao-na haita kuwa na tofauti kimuundo na kimtazamo kama CCM. (mfano mzuri tumeona leo Mgenja anahama chama huku akiwa na vazi la CCM).
KOSA KUBWA LA CDM NI KUWA KILA MWANACHAMA/MSHABIKI WAKE NI MJUAJI. Kuanzia viongozi wake, mashabiki wake mpaka Makapi waliowasajili. Mfano tuu mdogo huku JF, watu wanapiga kelele za mapema wakati mechi yenyewe bado. Naomba niseme kwa kingereza, IT DOESN'T MATTER HOW YOU START THE RACE-WHAT MATTERS IS HOW YOU FINISH IT.
Mchuano wa Magufuli na Lowasa nauona ni kama Mayweather na Pacquaio. Nyie wote ni watu wazima mnajua mshindi ni nani. TEAM MONEY. Purukushani zote za CDM kama tunavoziona sasa hivi na kama alizozionyesha Pacquaio hazitawaletea tija.
ok as long as hamchongeshi mafuriko kwa hela. tangu mzee slaa apishe gari bovu kupita ni sanaa tupu huko kwenu.hata kikiwa CCM "Z" wewe unawashwa nini? c utuache?
Huwa tunajibizana bila kufanhamu viwango vya elimu zetu. Sijui umemaliza kidato cha ngapi? Usiniambie una digrii, pse!
Uchambuzi wako haueleweki kabisa! Yaani watu hao wamekuwa makapi baada ya kuhama au walikuwa hivyo?
Jambo dogo unalotakiwa kuelewa ni ubora duni wa wana CCM wengi. Tangu ngazi ya juu hadi ya chini. Walio bora ni wacahache sana. Hiyo ndo siasa za CCM, Walipokwenda Dodoma, ni wachache waliofahamu kinachotokea na kupanga matukio. Waliowengi walikuwa wakisubiri yatokee halafu wanengue.
Mimi nina matumaini makubwa sana na siasa za nchi hii baada ya kuona watu wakihama CCM. Hata kama itagawanyika na kuwa na CCM B that will be very fine with us, Tanzanians. Najua B haitakuwa sawa na A.[/QUO
Ndugu yangu uchambuzi wangu usingekuwa haueleweki usingejisumbua kuujibu kama ulivofanya. Kukandia kuhusu elimu yangu kumeonyesha dhahiri wewe elimu yako haijakukomboa bado. Si lazima mtu awe na elimu ndio awe na hoja. Ingekuwa hivi JF ingebaki wewe na house girl wako. When you read rubbish you don't waste your time to respond. Sio unakandia then unarespond kwa hoja uliyoikandia. Sio lazima kila kitu ucomment kwa mapenzi ya kufata upepo ambayo mimi nayaheshimu.
si mlisema mmetoka Dodoma mkiwa wamoja!?
sasa unalialia nn?
yani jinsi nnavowachukia ccm ata wewe mugisha ukigombea urais kutumia chama cha chako cha CHAWAPUTA(chama cha wapiga puchu Tanzani) mimi ntakuchagua wewe against CCM
Mi nilifikiri utaomba Tibaijuka,Chenge,Muhongo na Ngereja wakatwe sababu ya Escrow kumbe wala hauna wazo hilo.Haya tueleze hawa wafuatao wamekuwa makapi kutokana na nn ? MGEJA,GUNINITA,NANGOLE,MSINDAI maana wao hawakuwa kwenye kinyang.anyilo chochote na nakuhakikishia kufikia kesho kutwa jumamosi na ww utakuwa umehamia cdm kwa maana hakuna aliyekuwa msema hovyo kama Said Nkumba je umeamini kuwa naye yuko cdm ? Tafakari chukua hatua na je UNAANDIKA LAKINI
Ikiwa mtu anahamia mahali fulani na kwa ajili fulani tu na sio sera sahihi basi akihama atakuwa amehama kwa manufaa tu na akienda kule ataenda na yake na kutaka kubadili mambo ya kule alipokwenda na sio kufanya matakwa ya chama husika....hivyo wabunge waliohamia kipindi hiki ndio hao...
Hii sio mimi bali ni sayansi tu ya kawaida...na wote hao watakuja kuwa chadema ileee ya kina mh. Shibu....kukubaliana tena kwa maswala fulani hakutakuwepo...tusubiri wala sio muda mrefu
Haa kumbe tangu uingie Jamii forum una kamwezi sasa sikujua, Siyo mbaya endelea kujifunza. Ukishajifunza tutakukaribisha kwenye mijadala ya mizito ya maslahi ya taifa siyo haya unayotumwa na wenzako huko nje.
Join Date : 11th July 2015
Posts : 125
Rep Power : 330
Likes Received
98
Likes Given
24
Ikiwa mtu anahamia mahali fulani na kwa ajili fulani tu na sio sera sahihi basi akihama atakuwa amehama kwa manufaa tu na akienda kule ataenda na yake na kutaka kubadili mambo ya kule alipokwenda na sio kufanya matakwa ya chama husika....hivyo wabunge waliohamia kipindi hiki ndio hao...
Hii sio mimi bali ni sayansi tu ya kawaida...na wote hao watakuja kuwa chadema ileee ya kina mh. Shibu....kukubaliana tena kwa maswala fulani hakutakuwepo...tusubiri wala sio muda mrefu