Jamani mimi ni mtanzania wa kawaida sana, na ninapenda mageuzi ya kisiasa katika nchi yetu, Naomba kama watanzania tusio na ushabiki tujadiliane kuhusu hili swala la viongozi waandamizi kutoka Ccm kuhamia UKAWA je tutakosea kuwaita ukawa ccm B, maana sura zile zile za ccm zinaendelea kuja ukawa, swali la pili je ukawa wana mikakati kuhakikisha watu hawa hawaji na elements zao za huko walikotoka?