Chadema nje wanaalani udikteta lakini ndani ya chama chao kuna udikteta wa kutisha

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,976
32,380
Wanabodi,

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kimekuwa kilaani udikteta lakini inasikitisha wanalaani kwa maneno tu ndani ya chama hiki kuna udikteta wa kutisha.

Ndani ya Chadema hakuna demokrasia hakuna uvumilivu wowote Chadema imewatimua madiwani wa Arusha, Chadema imewatimua madiwani wa Mwanza, Chadema walitaka kumvua uanchama mbunge wao, Zitto Kabwe alipolikataa kusudio lao la kususia hotuba ya rais na kutoka bungeni, Chadema pia walitaka pia kumfukuza John Shibuda alipotofautiana na maagizo yao.

Chadema wameshindwa kuwavumilia hao wanaokaidi maagizo yao na kuwatimua lakini cha achabu wao wanataka wakaidi maagizo ya serikali halafu wasiguswe, je nchi yetu itakuwa nchi ya namna gani endapo Chadema itaachiwa kufanya lolote walitakalo pasipo kufuata sheria za nchi, Chadema kijumla upinzani kwao una maana moja tu ya "antagonism" kwamba serikali ikisema ndio wao ni kusema hapana, ni upinzani usio na manufaa yoyote kwa watanzania.

Chadema wanataka vyombo vya ulinzi vifanye kazi yao kwa matakwa yao badala ya matakwa ya taaluma mpaka sasa hivi hakuna hata kiongozi mmoja wa Chadema aliefungwa kwa sababu za kisiasa halafu wanasema wananyanyaswa..
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya haya maneno: Nidhamu, udalali, udikteta, siku 90 na zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Mtu yoyote aliye makini na mwenye akili timamu ni lazima ahoji, serikali iwauwe viongozi wa Chadema kwa sababu ipi na kwa manufaa ya nani?
 
Ritz,'
Habari za jumatatu? Naona ulipotea kidogo. Kuna thread nyingine kule juu ya utajiri wa Ridhiwani inasubiri mchango wako.
 
Mtu yoyote aliye makini na mwenye akili timamu ni lazima ahoji, serikali iwauwe viongozi wa Chadema kwa sababu ipi na kwa manufaa ya nani?
Ndio munachokitaka kifanyike lakini jiulizeni muitaiweka kwenye ramani ipi nchi yetu mutakapotekeleza amri ya Amiri Jeshi Mkuu ya kuwauwa wapinzani ,angalizo tu
 
Wanabodi,

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kimekuwa kilaani udikteta lakini inasikitisha wanalaani kwa maneno tu ndani ya chama hiki kuna udikteta wa kutisha.

Ndani ya Chadema hakuna demokrasia hakuna uvumilivu wowote Chadema imewatimua madiwani wa Arusha, Chadema imewatimua madiwani wa Mwanza, Chadema walitaka kumvua uanchama mbunge wao, Zitto Kabwe alipolikataa kusudio lao la kususia hotuba ya rais na kutoka bungeni, Chadema pia walitaka pia kumfukuza John Shibuda alipotofautiana na maagizo yao.

Chadema wameshindwa kuwavumilia hao wanaokaidi maagizo yao na kuwatimua lakini cha achabu wao wanataka wakaidi maagizo ya serikali halafu wasiguswe, je nchi yetu itakuwa nchi ya namna gani endapo Chadema itaachiwa kufanya lolote walitakalo pasipo kufuata sheria za nchi, Chadema kijumla upinzani kwao una maana moja tu ya "antagonism" kwamba serikali ikisema ndio wao ni kusema hapana, ni upinzani usio na manufaa yoyote kwa watanzania.

Chadema wanataka vyombo vya ulinzi vifanye kazi yao kwa matakwa yao badala ya matakwa ya taaluma mpaka sasa hivi hakuna hata kiongozi mmoja wa Chadema aliefungwa kwa sababu za kisiasa halafu wanasema wananyanyaswa..

Naona ile kauli yao kwamba nchi "haitatawalika" inawatafuna wenyewe kwa kugeuka kuwa "chadema haitatawalika". Hawa jamaa wanadhihilisha kuwa ni madikteta kwanza muonekano wao wa uvaaji magwanda unalithibitisha hilo, wanadhani timuatimua ndio fundisho la kujenga maadili? Chama chao hakiko imara kwa kupata wanachama wenye interest binafsi na wanaokitumia chadema kubadili hali zao za maisha.

CCM iendelee kueneza itikadi kwa wananchi hasa hasa vijana waliopoteza mwelekeo kwa kuwashabikia hao wafedhuli na waroho wa madaraka. Tutambue jambo moja wana-JF, bila ya CCM madhubuti nchi yetu itayumba.
 
Hivi kweli nani awahofie watu ambao wamenyimwa kura za kutosha mwaka 2010?
 
Mtu yoyote aliye makini na mwenye akili timamu ni lazima ahoji, serikali iwauwe viongozi wa Chadema kwa sababu ipi na kwa manufaa ya nani?

Hapo kwenye red, Kumbe serikali inapanga kuwaua viongozi wa Chadema ??
Au mauaji ya Iringa yalilengwa kwa viongozi wa Chadema na walipowakosa wakaelekeza hasira zao kwa mwandishi ...
Funguka zaidi Ritz...
 
.....Chadema walitaka kumvua uanchama mbunge wao, Zitto Kabwe alipolikataa kusudio lao la kususia hotuba ya rais na kutoka bungeni, Chadema pia walitaka pia kumfukuza John Shibuda alipotofautiana na maagizo yao...

Ebu turejee kidogo uzi huu kwanza:

Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini juzi alilieleza gazeti hili kuwa msimamo wa kumfukuza Shibuda upo pale pale, kwani kambi hiyo wala Chadema hawawezi kumwacha mbunge anayekiuka sera na kuwadhalilisha viongozi hadharani.

"Shibuda hatafukuzwa kinyemela, lazima taratibu zifuatwe kwa Mnadhimu Mkuu wa kambi yetu kumwandikia barua ya kumweleza makosa yake na yeye kupata fursa yakujibu shutuma hizo, pili ataitwa katika Kamati Kuu ya chama chetu (Chadema), nao watatoa uamuzi wao,"alisema Zitto na kuongeza:

"Chadema si chama cha kihuni kwamba tutakurupuka ni lazima haki itendeke na mimi sipendi mtu aonewe, Shibuda atapata haki zake zote kama mwanachama. Mbunge yeyote wa Chadema anapaswa kujua akienda kinyume na sera ya chama atafukuzwa".

Alisema suala la posho lipo kwenye Ilani ya uchaguzi wa 2010 kwa hiyo ni sera, na kwamba anayepinga atafukuzwa tu na kwamba Chadema wataanza na Shibuda.

Zitto alisema, "Shibuda anajua mie humtetea sana, lakini anapokwenda kinyume na sera ya chama tutamfukuza, aniite majina yoyote tu akienda kinyume na sera nitakuwa wa kwanza kumfukuza."

"Kuna masuala ya nidhamu kwenye Bunge na wabunge wa chama fulani inaitwa' three line whip, masuala ya msimamo wa kitendaji mfano tulipokaidi kwenda Bungeni kutoka nje ya ukumbi wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia bunge (walk out), haya ni ya kawaida na hayana adhabu kali, lakini likiwa la sera adhabu ni kufukuzwa, Shibuda asipaparike," alisema Zitto.

Kina Ritz mnaweza kucheza na akili za Wana-JF Mamboleo na wasio na kumbukumbu sahihi za Siasa za nchi hii lakini miongoni mwao Omutwale SIMO!

Mwenye akili na kumbukumbu sahihi atabaini hii ilikuwa pre-emptive strategy ya mtoa kauli kuwatega viongozi wakuu wa CDM. Ni miongoni mwa matukio ya nadra ya mtoa kauli kuvaa husika wa cheo cha chama chake na kusimama kwa nafsi ya wingi katika umoja (-tuta..., sisi....) japo katika hitimisho anarejesha tabia yake halisi kwa kusema "nitakuwa wa kwanza kumfukuza" Shibuda hakulianzisha hili akiwa punguani na wala aliyetoa msimamo wake akaupa hadhi ya niaba ya chama naye alikuwa na malengo. Halikuwa suala la kulinda misingi bali kuweka mtego sahihi wa kukamilisha lengo. Heko kwa viongozi wakuu-CDM kuwapuuza wote. Kuwapuuza ndiyo imekuwa jibu sahihi lililokwamisha mpango ovu kufanikiwa. Ni dhahiri wote hawa pia si wana-CDM rejea swali walakini wangu toka mwaka 2010 hapa

Ndiba,
Nataka niweke rehani kujaribu udhaifu wa ubongo wangu kwa kubashiri lifuatalo:

  • Zitto Zuberi Kabwe, kabla na baada ya uchaguzi, akiwa ameshinda au ameshindwa SI MWANACHAMA WA CHADEMA
 
Kama hamna hofu hizi kauli zinatoka wapi?

Chadema haitafikisha mwaka-wassira
(hii ni hofu kubwa)
mbona mnatumia nguvu nyingi kupambana na cdm kwa kuwatumia polisi?

Hivi kweli nani awahofie watu ambao wamenyimwa kura za kutosha mwaka 2010?
 
Dr Slaa, hajaufikia hata nusu ya umaarufu aliokuwa nao Christopher Mtikila mwaka mwaka 1992 na chama chake cha DP alipohubiri kwa nguvu ya uzawa akileta msamiati mpya katika siasa wa "magabacho'li" na "walalahoi" mbona hakuuwa...Dr Slaa bana.
 
Mtu yoyote aliye makini na mwenye akili timamu ni lazima ahoji, serikali iwauwe viongozi wa Chadema kwa sababu ipi na kwa manufaa ya nani?

Ritz hivi elimu yako ipoje? unaweza kutusaidia hata summary kidogo tu ya cv yako? Nasema hivi kwa kuwa always unapost upuuzi hapa kwenye jamvi na zaidi ya rejao hakuna anayeekunga mkono, Yaani madiwani wa Arusha waende kinyume na taratibu za chama waonywe wapewe muda wa kujieleza wakatae bado wavumiliwe tu?? CDM huwa inachukua hatua sio sawa na magamba akina Sitta na Nape walianzisha chama (CCJ) wakiwa ndani ya CCM mnawalea hadi leo

,CDM unafukuzwa then ukienda mahakamani ndio penyewe! Kolimba(R.I.P) alisema ccm haina dira yuko wapi leo??
Jumbe alihoji muungano nini kilitokea??Malecela akiwa waziri mkuu aliunga mkono serikali tatu nini kilimpata?hebu tuorodheshee huo udikteta wa CDM?halafu ndani ya CDM hakuna zidumu fikra za mwenyeketi!ukikosea unapigwa chini

Umesema Zitto alitaka kuvuliwa ubunge hebu tupatie minutes za hicho kikao inaelekea unaingia vikao vya cc ya CDM
 
Kumbe kuwaacha mafisadi wanatamba njiani na pesa za uma ndio demokrasia?

Wakiachwa hao unaodhani wanaonewa wewe ndio ungekuwa wa kwanza kusema chadema hawaoneshi kwa vitendo ni wasemaji tu.

Siku hizi umekuwa mike ya zitto?
Lakini omutwale kakuumbua!

Wanabodi,

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kimekuwa kilaani udikteta lakini inasikitisha wanalaani kwa maneno tu ndani ya chama hiki kuna udikteta wa kutisha.

Ndani ya Chadema hakuna demokrasia hakuna uvumilivu wowote Chadema imewatimua madiwani wa Arusha, Chadema imewatimua madiwani wa Mwanza, Chadema walitaka kumvua uanchama mbunge wao, Zitto Kabwe alipolikataa kusudio lao la kususia hotuba ya rais na kutoka bungeni, Chadema pia walitaka pia kumfukuza John Shibuda alipotofautiana na maagizo yao.

Chadema wameshindwa kuwavumilia hao wanaokaidi maagizo yao na kuwatimua lakini cha achabu wao wanataka wakaidi maagizo ya serikali halafu wasiguswe, je nchi yetu itakuwa nchi ya namna gani endapo Chadema itaachiwa kufanya lolote walitakalo pasipo kufuata sheria za nchi, Chadema kijumla upinzani kwao una maana moja tu ya "antagonism" kwamba serikali ikisema ndio wao ni kusema hapana, ni upinzani usio na manufaa yoyote kwa watanzania.

Chadema wanataka vyombo vya ulinzi vifanye kazi yao kwa matakwa yao badala ya matakwa ya taaluma mpaka sasa hivi hakuna hata kiongozi mmoja wa Chadema aliefungwa kwa sababu za kisiasa halafu wanasema wananyanyaswa..
 
Wanabodi,

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kimekuwa kilaani udikteta lakini inasikitisha wanalaani kwa maneno tu ndani ya chama hiki kuna udikteta wa kutisha.

Ndani ya Chadema hakuna demokrasia hakuna uvumilivu wowote Chadema imewatimua madiwani wa Arusha, Chadema imewatimua madiwani wa Mwanza, Chadema walitaka kumvua uanchama mbunge wao, Zitto Kabwe alipolikataa kusudio lao la kususia hotuba ya rais na kutoka bungeni, Chadema pia walitaka pia kumfukuza John Shibuda alipotofautiana na maagizo yao.

Chadema wameshindwa kuwavumilia hao wanaokaidi maagizo yao na kuwatimua lakini cha achabu wao wanataka wakaidi maagizo ya serikali halafu wasiguswe, je nchi yetu itakuwa nchi ya namna gani endapo Chadema itaachiwa kufanya lolote walitakalo pasipo kufuata sheria za nchi, Chadema kijumla upinzani kwao una maana moja tu ya "antagonism" kwamba serikali ikisema ndio wao ni kusema hapana, ni upinzani usio na manufaa yoyote kwa watanzania.

Chadema wanataka vyombo vya ulinzi vifanye kazi yao kwa matakwa yao badala ya matakwa ya taaluma mpaka sasa hivi hakuna hata kiongozi mmoja wa Chadema aliefungwa kwa sababu za kisiasa halafu wanasema wananyanyaswa..

Mbona unajichanganya kaka mkubwa,nakuaminia sana kwa uwezo wako wa kutotereka pindi unaposhambuliwa humu jamvini na wana CDM ila hapa hoja zako hujazipanga.

Ona hapa ''Chadema wameshindwa kuwavumilia''
Ukajijibu bila kujua "Chadema walitaka kumvua uanchama mbunge wao, Zitto Kabwe alipolikataa kusudio lao la kususia hotuba ya rais na kutoka bungeni, Chadema pia walitaka pia kumfukuza John Shibuda alipotofautiana na maagizo yao.''

Kama wangekuwa hawana kuvumiliana basi usingeandika hiyo sentensi hapo juu.

Ona tena mistari yako hii "Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kimekuwa kilaani udikteta lakini inasikitisha wanalaani kwa maneno tu ndani ya chama hiki kuna udikteta wa kutisha."

ukajijibu hapa " Chadema imewatimua madiwani wa Arusha, Chadema imewatimua madiwani wa Mwanza"

Umeyajibu maswali yako mwenyewe bila kujua ,Kapitie upya nini maana ya demokrasia pale ambapo mwanachama/raia/kiongozi anapokiuka masharti /kanuni na sheria walizojiwekea kujiongoza/ziwaongoze anatakiwa afanywaje. Demokrasia haisemi kiongozi anapokosea asihukumiwe bali inatoa mwanya wa kumsikiliza mkosaji ili apewe hukumu stahiki.Hivyo waliofukuzwa walionekana wana makosa na adhabu kulingana na demokrasia ya chama ni kuvuliwa uwanachama,kama ambavyo Shibuda na Zitto walivyohukumiwa kulingana na Demokrasia ya chama.
 
Dr Slaa, hajaufikia hata nusu ya umaarufu aliokuwa nao Christopher Mtikila mwaka mwaka 1992 na chama chake cha DP alipohubiri kwa nguvu ya uzawa akileta msamiati mpya katika siasa wa "magabacho'li" na "walalahoi" mbona hakuuwa...Dr Slaa bana.
Hakuuliwa mrema na saif sharif itakuja kuwa Slaa,unakumbuka hawa walivyo vuma? Vyama vya upinzani ni kama bongo fleva,wanakuja kwa mkwara halafu wanafifia. Wanaendelea kuwepo lakini hawavumi.
 
Kumbe dr-slaa ndio aliwatuma polisi wamtoe utumbo mwangosi?
Dr -slaa ndio alimuagiza kamanda aangalie tukio la mauaji bila kufanya kitu!

Dr Slaa, hajaufikia hata nusu ya umaarufu aliokuwa nao Christopher Mtikila mwaka mwaka 1992 na chama chake cha DP alipohubiri kwa nguvu ya uzawa akileta msamiati mpya katika siasa wa "magabacho'li" na "walalahoi" mbona hakuuwa...Dr Slaa bana.
 
Chadema ni watu wa porojo Dr Slaa, hajafikia msimamo mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema, mwaka 1995.
 
Ritz hivi elimu yako ipoje? unaweza kutusaidia hata summary kidogo tu ya cv yako? Nasema hivi kwa kuwa always unapost upuuzi hapa kwenye jamvi na zaidi ya rejao hakuna anayeekunga mkono, Yaani madiwani wa Arusha waende kinyume na taratibu za chama waonywe wapewe muda wa kujieleza wakatae bado wavumiliwe tu?? CDM huwa inachukua hatua sio sawa na magamba akina Sitta na Nape walianzisha chama (CCJ) wakiwa ndani ya CCM mnawalea hadi leo

,CDM unafukuzwa then ukienda mahakamani ndio penyewe! Kolimba(R.I.P) alisema ccm haina dira yuko wapi leo??
Jumbe alihoji muungano nini kilitokea??Malecela akiwa waziri mkuu aliunga mkono serikali tatu nini kilimpata?hebu tuorodheshee huo udikteta wa CDM?halafu ndani ya CDM hakuna zidumu fikra za mwenyeketi!ukikosea unapigwa chini

Umesema Zitto alitaka kuvuliwa ubunge hebu tupatie minutes za hicho kikao inaelekea unaingia vikao vya cc ya CDM

Nini maana ya elimu.
 
Back
Top Bottom