Chadema nje wanaalani udikteta lakini ndani ya chama chao kuna udikteta wa kutisha

Kuna watu wana bahati! EPA wamo, Richmond wamo, IPTL wamo, na hii ya Uswiss wamo pia. Yani mpaka raha!
 
Hoja hii inaweza kutoka kwa mtu ambaye anathamini maslahi yake zaidi kuliko maslahi ya Taifa na si vinginevyo.
 
Udikteta wa magwanda mbona uko wazi sana labda kwa alieziba masikio kwa pamba
 
Kama unataka kufukuzwa Chadema pinga mawazo ya Dr Slaa au Mbowe, muulize Kafulila.
 
Hoja hii inaweza kutoka kwa mtu ambaye anathamini maslahi yake zaidi kuliko maslahi ya Taifa na si vinginevyo.

kwanini mkuu,au hampendi kukosolewa.unapaswa kumwelewesha kama kuna mahali kakosea.otherwise hakuna taasisi isiyo na mapungufu,hivyo chadema kama taasisi lazima ina mapungufu yake na hapa mleta mada ameonyesha moja ya mapungufu aliyoona ndani ya chadema.
 
Chadema kila siku mnasema chama chenu ni cha haki wakati kumbe ni madikteta wakubwa, Wasukuma wa Mwanza vijana wenu mliowakuza wenyewe na kuwapa uongozi wamefukuzwa chama.
 
kwanini mkuu,au hampendi kukosolewa.unapaswa kumwelewesha kama kuna mahali kakosea.otherwise hakuna taasisi isiyo na mapungufu,hivyo chadema kama taasisi lazima ina mapungufu yake na hapa mleta mada ameonyesha moja ya mapungufu aliyoona ndani ya chadema.

Uvumilivu anaozungumzia mtoa hoja una thamani katika maslahi yake kwa sababu unadhoofisha CHADEMA kama taasisi. Kuvumilia watu wanaodhoofisha taasisi si uvumilivu, ni uzembe. Nchi yetu imefika hapa kwa sababu ya 'uvumilivu', leo mtu anaweza kufanya kitu chochote bila kuwajibika au kuwajibishwa.
CHADEMA tunataka mabadiliko si tu katika uongozi bali pia katika tabia, fikra na mtazamo wa watu walio katika mfumo wa uongozi. Tunataka viongozi watokanao na chama chetu wasiturejeshe katika zama za 'uvumilivu' unaoangamiza taifa na kuneemesha wachache!!.
 
Chagulani na Matata, nasikia leo wamekwenda mahakamani kupiga kuvuliwa uanachama, Wasukuma wa Mwanza wamejitolea kuwasaidia kuweka mawakili.
 
Chagulani na Matata, nasikia leo wamekwenda mahakamani kupiga kuvuliwa uanachama, Wasukuma wa Mwanza wamejitolea kuwasaidia kuweka mawakili.

tatizo la chagulani ndani ya chama ni majina yake ya mwanzo.matata ameingizwa tu ili kufunika kombe
 
Ritz hivi elimu yako ipoje? unaweza kutusaidia hata summary kidogo tu ya cv yako? Nasema hivi kwa kuwa always unapost upuuzi hapa kwenye jamvi na zaidi ya rejao hakuna anayeekunga mkono, Yaani madiwani wa Arusha waende kinyume na taratibu za chama waonywe wapewe muda wa kujieleza wakatae bado wavumiliwe tu?? CDM huwa inachukua hatua sio sawa na magamba akina Sitta na Nape walianzisha chama (CCJ) wakiwa ndani ya CCM mnawalea hadi leo

,CDM unafukuzwa then ukienda mahakamani ndio penyewe! Kolimba(R.I.P) alisema ccm haina dira yuko wapi leo??
Jumbe alihoji muungano nini kilitokea??Malecela akiwa waziri mkuu aliunga mkono serikali tatu nini kilimpata?hebu tuorodheshee huo udikteta wa CDM?halafu ndani ya CDM hakuna zidumu fikra za mwenyeketi!ukikosea unapigwa chini

Umesema Zitto alitaka kuvuliwa ubunge hebu tupatie minutes za hicho kikao inaelekea unaingia vikao vya cc ya CDM

Elimu yake ni sawa sawa na ya Mbowe lakini Ritz alijiendelezaendeleza hakuishia kujua kusoma na kuandika tu.
 
ritz ukilinganisha chadema na mtikila you are wrong 100% au mrema angalia hoja inayotolewa na mbunge wa chadema serikali yote hailali tumia kichwa vizuri usifuate moyo wako fuata brain.Ndio maana serikali inauwa kila mikutano ya kampeni na mikutano ya chadema kusudi watu wasipate ujumbe wa chadema.Chadema haiwezi kufutwa maana hata Mugabe na udikteta wake alishindwa kufungia TSICHANGALAI,maana ukiifungia chadema hoja itakuwa ni kuimarisha al shabaab na uamsho hivyo mmarekani na mwingereza wataingila kati na hivi kuna gas nchi haitatawalika be careful ccm.
 
chama chochote lazima kiendeshwe kwa nidhamu na hakuna mtu ambaye yuko juu ya chama kitu kinachowagharimuccm mpaka sasa hivi wameruhusu baadhi ya watu kuiwa juu ya chama na kitendo cha kushindwa uwachukulia hatua wale waliokichafua ndio kinawafanya wazidi kupoteza umaarufu ila nawashauri cdm wawape semina na mafunzo wafuasi wao kwani wengi wamepata nafasi bila kujua wajibu wao ndio maana wanafanya mambo yanayopingana na taratibu za chama mfano tumeona mwanza na arusha
 
Huo ni uwajibishaji braza. CCM imeshindwa kuwawajibisha Mafisadi (huenda nawe umo). CDM ndio chama cha Ukweli. Ukifanya mzaha, unakaa pembeni. Kuhusu kutii amri za Polisi, ni zipi??? Unafurahi Polisi kuua?? Ama kweli damu mtailipa!
 
Elimu yake ni sawa sawa na ya Mbowe lakini Ritz alijiendelezaendeleza hakuishia kujua kusoma na kuandika tu.

hongera yake Ritz, vipi kuhusu wewe mama Mingoi, bado unauza supu ya makongoro au nawe wajiendeleza???
 
What you are saying is a great lie.
'A great lie is like a great fish on a dry land: it may fret and fling and make a frightful bother, but it cannot hurt you. You have only to keep still, and it will die of itself. " (George Crabbe)

Prepare for 2015 brother RITZ
 
....Mwenye akili timamu ya kuhoji mambo ya Chadema lakini asihoji yale ya magamba!!!! Kweli weye una akili timamu!!!

Mtu yoyote aliye makini na mwenye akili timamu ni lazima ahoji, serikali iwauwe viongozi wa Chadema kwa sababu ipi na kwa manufaa ya nani?
 
Unadhani maamuzi magumu ni yapi? Hiyo dhambi ya kuvumiliana ndo iliyoifikisha nchi yetu hapa ilipo. Ili kujenga nidhamu na utii lazima kufanya kama wanavofanya CHADEMA, na ndiyo maamuzi magumu. Karibu CHADEMA.
 
Back
Top Bottom