1) Msingi wa mgogoro wa Madiwani Arusha ni Uvunjifu wa Kanuni, Taratibu na Sheria zinazoongoza uchaguzi wa U meya katika Manispa ya Arusha. Kamati ya Marando imebaini kuwa "mchakato na utaratibu mzima wa uchaguzi wa Naibu Meya haikuzingatia Kanuni na Taratibu za Chama na Halmashauri" (Marando Kif.4.2). Hivyo, kama Chadema ilipinga ukiukwaji katika uchaguzi wa Meya, haiwezi kamwe kuidhinisha ukiukwaji ambao kwa bahati mbaya ni maradufu zaidi katika uchaguzi wa Naibu Meya.
2) Ni kweli mazungumzo husika yalijulikana kwa ngazi ya Taifa. Mara ya kwanza Makao Makuu yalifahamu document ya mwafaka ya 15/4/2011, kwa kuona document tarehe 29/4/2011 katika Mkutano baina ya viongozi wa Madiwani akiwemo Mwenyekiti wao Mhe. Mallah na Mnadhimu Mkuu wa Kamati ya Madiwani Mhe. John Bayo. Kikao kilifanyika New Safari Hotel, Arusha chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu. Miniti za Kikao hicho zinaonyesha mambo 5 ambayo Katibu Mkuu alibainisha kama msingi wa mazungumzo yeyote kama yatakuwepo. Nayo ni:-
i)Serikali ikiri kosa kuwa kanuni na mwongozo wa uchaguzi wa Meya Arusha mjini zilikiukwa.
ii)Uchaguzi wa Umeya urudiwe kwa vile haukufuata kanuni na Taratibu.
iii)Serikali itoe pole kwa wahangaa tukio la tarehe 5 Januari 2011
iv) Serikali ipitie madai ya msingi ya Chadema ikiwa ni ni kuwawajibisha Mkurugenzi wa Manispaa (kwa sababu ndiye alivunja kanuni) na OCD wa Arusha mjini
v) Kesi ya ya Viongozi wa chama na baadhi ya wananchi haina msingi hivyo ifutwe.
Kisha kikao kilijadili document ya 15/4 na kuona ina mapungufu makubwa. Iliazimiwa ifuatavyo:-
1) Miniti hii ina hila na ni ya unafiki na hivyo isitumike katika kufikia muafaka wa suala la Umeya hapa Arusha mjini.
2) Mwenyekiti wa Madiwani Estomih Mallah na Mnadhimu wa Madiwani Mhe. John Bayo wawajulishe madiwani na Mkuu wa Wilaya kuwa muafaka huu kwa mujibu wa chama una mapungufu ambayo chama hakitaweza kuyaafiki na hivyo usitumike kwa kufikia muafaka wowote.
3) Kwa kutambua kuwa CCM wapo tayari kwa mazungumzo, Mhe. Katibu Mkuu atayapeleka mapendekezo ya muafaka huu kwa wanasheria wa chama ili kuyafanyia marekebisho na mapendekezo hayo yatakuwa ni sehemu ya mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa Chama Mhe. Freeman Mbowe (MB, KUB na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda.
Kwa bahati mbaya, tarehe 20/6/2011 Madiwani waliridhia mwafaka wao kama ulivyokuwa kwenye Hati yao ya tarehe 15/4/2011, na kuendelea na uchaguzi, bila kujali mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Mhe. Mbowe na Waziri Mkuu. Isitoshe utaratibu wa kisheria wa uchaguzi wa Naibu Meya nayo ilikiukwa (kwa mujibu wa Taarifa ya Marando kukiwa na kugushiwa kwa saini ya Katibu wa Wilaya wakati pia hakuna kikao chochote cha Kamati Tendaji kilichojadili na kuteua mgombea wa Chadema). Hiki ndicho kilichofikisha Kamati Kuu kuelekeza Madiwani waliochaguana kinyume na Kanuni wajiuzulu ndani ya siku 3.
Baada ya hapo Madiwani 6 wakiongozwa na Mallah walikata rufaa, kwa bahati mbaya kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama rufaa zao hazikukidhi mahitaji ya Kikatiba na Kanuni. Maswala yote hayo sasa yanarudi mikononi mwa Kamati Kuu ambayo hivi Karibuni itatolea ufumbuzi swala la Madiwani kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.