Madiwani watano wa CDM, waliovuliwa uanachama na Kamati kuu ya chama hicho mwishoni wa wiki iliyopita wanakwenda mahakamani kupinga uamuzi huo.
Diwani wa Kata ya Elerai, John Bayo, alieleza kwa njia ya simu akiwa njiani kutokea Dodoma walipokwenda kuhojiwa kabla uamuzi wa kutimuliwa kufikiwa.
Bayo alisema kabla ya kuchukua uamuzi wowote watazungumza na wapiga kura kwenye kata zao kuwaeleza yaliojiri na kuacha nafasi ya uamuzi wa hatua zinazostahili mikononi mwa umma uliwaamini na kuwapa dhamana yb uongozi.
"Binafsi sina kinyongo na chama changu nimepokea nimepokea uamuzi huo, lakini nakuhakikishia nitaendelea na nafasi ya udiwani hadi uchaguzi mkuu ujao, kuna njia nyingine ya kupinga uamuzi huo kupitia vikao au mahakama" alisema Bayo.
SOURCE:
Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza
8 August 2011